Tuma kwenye namba hii wamemdondosha mzee Thomas

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
2,965
4,577
Mzee Thomas Ayo mwenye umri wa miaka 67 mkazi wa Kata ya Kiutu wilayani Arumeru mkoani Arusha amefariki dunia ghafla (nje ya duka la wakala wa fedha ) mara baada ya kupata mshtuko alipobaini ametapeliwa kiasi cha fedha shilingi laki nne na tisini na nane (498,000) alizotuma kwenye namba iliyodhaniwa kuwa ni matapeli wa mtandaoni.

View: https://www.facebook.com/EastAfricaTV/videos/1045782983693067/?mibextid=rS40aB7S9Ucbxw6v

Wapuuzi wa tuma kwenye namba hii mnaendelea kuwatoa uhai wazee wetu kipuuzi tu. Ni kwamba serikali imeshindwa kuzuia kweli hii kitu kiasi kwamba watu wanapoteza maisha namna hii.

Huyu ni mtu wa nne sasa hivi napata kusikia amepata mshtuko wa moyo kisa kikiwa hiki hiki?!
 
Walichukua alama zeru za vidole na namba ya nida kwa ahadi kwamba watakomesha utapeli wa aina yoyote ile. Lkn cha ajabu utapeli ndiyo umeanza upya. Mimi ninachoomba ni kunirudishia namba yangu ya nida na alama zangu za vidole.
 
Nenda kwenye kampuni, au kwa wakala wa kampuni, uliyosajilia laini yako ufute usajili. Ni bure kabisa.
 
Siku hizi utapeli umekuwa kama ni jambo tu la kawaida. Hakuna hatua zozote zile za kueleweka, zinazochukuliwa ili kukomesha hii hali. Ni kama vile mamlaka husika zimezidiwa maarifa na hao matapeli.
 
Walichukua alama zeru za vidole na namba ya nida kwa ahadi kwamba watakomesha utapeli wa aina yoyote ile. Lkn cha ajabu utapeli ndiyo umeanza upya. Mimi ninachoomba ni kunirudishia namba yangu ya nida na alama zangu za vidole.
Zilikuwa ni njia za upigaji tu
Unadhani imekula kiasi gani na wamepiga mgapi
 
Utapeli kwenye simu usikilize kwa makini neno la kwanza tu utajua huyu ni tapeli. Tuma kwa hii namba jina litakuja chungwa nanasi tapeli anaotea kuwa kuna mtu utamtumia hela katumia namba mpya au ya mtu mwingine kukujulisha utumie hiyo namba kutuma. Kwa harakahara unaweza kutuma tu kumbe umetuma kwa tapeli
 
Utapeli haujawahi kuisha mahali popote pale duniani. At the end of the day ni jukumu la muhusika mwenyewe kuchukua tahadhari zote. Apumzike kwa amani
 
Walichukua alama zeru za vidole na namba ya nida kwa ahadi kwamba watakomesha utapeli waaina yoyote ile. Lkn cha ajabu utapeli ndiyo umeanza upya. Mimi ninachoomba ni kunirudishia namba yangu ya nida na alama zangu za vidole.
Mchezo huu unachezwa na wasajili ya hizi line dawa ni kukamata wasajili waliosajili line
 
Vitengo vyetu jamani nawaita mara tatu.

Pesa inaacha kabisa paper trail aasa inashindikanaje kuwapata
 
Back
Top Bottom