Habari wakuu!!
Nianze kuzungumza kwa masikitiko makubwa sana kwa jinsi suala la Paul Makonda lilipofikia!Nimeanza kushikwa na moyo wa huruma baada ya kuona video na picha zikimuonesha Paul Makonda akilia kwa uchungu....Lakini hakuna namna inabidi tu atenguliwe na ashtakiwe kwa mujibu wa sheria ambapo adhabu yake ni miaka saba bila faini
Dhahma ya Mh.Makonda inadhihirisha haja ya kupekua wateule kabla ya kuwadhibitisha. Wakati rais Magufuli anatangaza wateule wake ngazi ya Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri,tulisema wazi kwamba haikufanyika vetting kwa maana ya upekuzi
Tulisema haukufanyika upekuzi kwa kuwa tulishangazwa na uwepo wa baadhi ya majina katika orodha ya uteuzi. Ukiacha wale tuliokuwa tunawafahamu kama kina Makonda, Mtela Mwampamba,wengi wa wateule walikuwa ni wagombea wa ubunge CCM katika kura za maoni.....Kwa hiyo wale walioshindwa katika kura za maoni CCM walikuja kumwagwa kwenye ukurugenzi,uDC na uDAS bila kuwachuja wasio wa uwezo
Jamani sisi tuliohuku tunawapa ukweli wengi wao kazi wanazozifanya hawazijui,zaidi mikwara na siasa.
Lakini kubwa zaidi ni hili la Makonda,kama ingefanyika upekuzi yakinifu Mh.Makonda asingeweza kuwa Mkuu wa Mkoa, kwa sababu si tu hana ethics bali uwezo wake pia ni mdogo sana. Kuna kazi zingine angeweza kufanya lakini si ya ukuu wa mkoa.
Nitoe mwito kwa Rais Magufuli kufanya retrospective vetting kwa wateule wake kuanzia mawaziri mfano kina Dr.Mwakyembe mpaka maDAS ili kuwaondosha wateule wote wasio na uwezo na elimu za ujanja ujanja
Juma Pinto na Kinjekitile Mwiru ni watu waliogharimu maisha ya vijana wengi kutokana na biashara zao za Mihadarati. Kinjekitile Mwiru siyo jina geni kutajwa katika biashara ya mihadarati. Ni aibu kubwa sana na fedheha kwa Rais kwa kitendo cha Paul Makonda kukimbilia South Africa tena na kupokelewa na DON mkubwa wa MADAWA ya kulevya ndugu Kinjekitile Mwiru.
Sasa kutokana na uhusiano huu kuna uwezekano mkubwa sana kuwa vita ya MADAWA ya kulevya iliyotangazwa na Rais Magufuli na kuendelezwa na Paul Makonda kwa upande wa Paul makonda inaonekana hapa aliamua kushupalia swala la MADAWA ya kulevya ili kuwadidimiza kibiashara washindani wakuu wa biashara ya mihadarati wa Kinjekitile Mwiru na kumpa kinga ili asifikwe na Mkono wa sheria.
Ushauri: Ninaomba serikali Kali kabisa ya mhe. Magufuli iweze kuchunguza kwa undani sana washirika wakuu wa Paul Makonda ambao wanatajwa kujihusisha na biashara ya mihadarati wakiwemo GSM. Sambamba na hilo swala la Kughushi cheti lipewe kipaumbele ili mkondo wa sheria uchukue nafasi yake. Naimani serikali sikivu ya Mhe.Magufuli itafanya na inaendelea kufanya ili kuweka mambo sawa.
NB: Mhe. Rais una nia nzuri na watanzania ila ulikosea kuwachagua kimkakati zaid(ili kuua upinzani bila vetting).