Habari wanajamvi,
Baada ya pilau langu la idd leo nimewaza jambo fulani, kwamba haya anayofanya rais wetu ni wakati muafaka, kuna watu tuliishi jehanam na wengine peponinhali ya kuwa sote ni raia wa nchi hii.
Namshauri Rais akaze buti maana hata usawa umeoneka kwenye hii sikukuu, wote tumeambulia pilau kama watoto wa uswahilini.Hiyo Demokrasia tunayotaka aifuate ndio imetufikisha pale tulipokuwa, kulikuwa na harufu ya ufisadi kila idara na huduma ziliendelea kuzorota siku hadi siku.
Ushauri wangu kwa rais;
1.Endelea na kasi hiihii, sisi walala hoi tuko pamoja na wewe.
2.Hawa UKAWA waachie platform yao wakushauri na hata kukuchallenge maana ndio kazi ya opposition.
3.Bunge liache lifanye kazi zake maana ndio chombo kitakachokusaidia kuisafisha system ambayo unaijenga.
4.Wabane wateule wako ili hii 40% ya fedha za maendeleo kwenye bajeti ikalete tija kwa wananchi huko vijijini.
5.Bado Naamini tuna rasilimali za kutosha kutuvusha hapa,tumia safu yako imara ya wachumi tulionao kuona namna hizi fursa zitakavyoinua maisha ya hawa walala hoi.
Asante