Tulidanganywa kutakuwa na mabasi yanayoenda Kasi

Hili limeniuma sana. Serikal ilisema kutakuwa na mabasi yanayoenda kasi. Nmepanda haya mabasi zaidi ya mara 10 wala hayaendi kasi. Hayo ya kasi watatuletea lini?
Haya si haba hayasimami vituo ving sana kama daladala na hayana traffic jam but hayana kasi ambayo nlidhania yangekuwa nayo kama yanavyoitwa.
Kwa wale tulioenda nje ya nchi nadhan tunafaham train za kasi... Nlidhan at least hata kwa asilimia 40 tungekuwa na basi za namna hiyo. Kwa nini mlitudanganya?

We mzima kweli...Hata kidogo huwezi kulinganisha electronic train za nje na basis.
 
Tukitaka kumaliza tatizo la foleni Dar ni lazima kuitangaza Dar kama mji wa kijamaa, na mfumo wa usafiri umilikiwe na uma kwa maana ya kutoruhusu watubinafsi kutumia miundombinu ya bara bara, magari binafsi mwisho iwe maili moja!

Ukisema hivyo ni sawa na kupanga bila malengo. Barabara za mwendo kasi ni sehemu ndogo sana ambayo imetengenezwa unachosema kingewezekana endapo endapo hizi barabara zingejegwa kila sehemu hivyo bado asilimia 99.9% wanatumia daladala na magari binafsi.
 
Ujamaa ndio mfumo pekee wa kumaliza foleni?
Ideology ya Mwalimu ya ujamaa haikutambua kwamba siku moja mwananchi mmoja mmoja atakuja kumiliki gari hivyo hapakuwa na umuhimu wa kutengeneza miundombinu ya kukabiliana na mfumuko wa magari...yeye aliamini kama wewe ni mtumishi wa TANESCO utabebwa na gari za Tanesco, Jeshi, Polisi, TTCL n.k ndiyo maana nashauri tutanzishe Dar es Salaam nyingine ya kibepari hii ibaki ya kijamaa tu ili kukidhi malengo ya mwasisi!
 
Unafikiri hiyo speed yanayoenda hayo mabasi, wakisema coaster zipite kwenye hizo barabara zitashindwa kwenda hiyo Kasi yanayoenda? Wameingia gharama bure, hats UDA zingeweza kipita kwenye hizo barabara kama speed yenyewe ndo hiyo!
 
Hiyo mwendo kasi umeisema wewe, haijawahi kusemwa hata mara moja kuwa haya mabasi yatakuwa ya mwendo kasi. Siku zote wamekuwa wakisema mabasi yaendayo haraka na na sio yaendayo kasi

KUNA tofauti ya HARAKA NA KASI
 
Tatizo ni kutokana na mpangilio wa mji barabara za mwendo kasi tungezuweka wapi?

Nibora wangewekeza kwenye treni maana huu mradi unaonekana sio rafiki kwa mazingira ya Dar kutokana na maeneo finyu haya ni matatizo ya kuwa na masilahi binafsi kwenye miradi ya Taifa ndio maana wananchi ndio wanaishia kuteseka.
 
Treni haina maslahi binafsi?

Ngoja tumuulize Mwakyembe.
 
Eti kwa wale tulioenda nje. Ss basi ni sawa na train? Unataka basi litembee na 120 mjini? Huko nje hata sisi tumeishi mabasi hayatembei kasi kubwa. Sidhan km mtu mwenye exposure ya public transport ya ulaya atategemea bus liende km train. Watanzania bana. Hata muishi mwezini mtabaki kulalamikia nonsense
 
Hatukudanganywa ila neno lililotumika kutafsiri BRT lilikosewa na wanaojiita wasomi huko ofisini! Rapid Bus Transport ni usafiri wa basi ziendazo haraka na si ziendazo kasi!
Haya ni matokeo ya kuajiri vihiyo hadi upotoshaji unajitokeza na ofisa mwenye dhamana yupo tu. JPM hebu fanya suprise inspection ya vyeti katika moja ya idara au agency uone.
 
Kama unapenda kwenda kasi kapand NGORIKA au BUFFALO EXPRESS
1463165404930.jpg
1463165412045.jpg
,au apande kitu Kisbo njia ya Mwanza/Kahama na Dar
 
Kweli mkuu waliotudanganya wabadili kauli zao. Sio mabasi ya kasi ni ya mwendo wa kawaida ila yana barabara zake na kupungiza vituo.
Mwanasiasa mmoja aliuliza wakati wa kampeni zilizopita k uwa, tatizo ni gari zilizopo kukosa kasi au ni tatizo LA barabara linaloaababisha msongamano?
 
Hiyo mwendo kasi umeisema wewe, haijawahi kusemwa hata mara moja kuwa haya mabasi yatakuwa ya mwendo kasi. Siku zote wamekuwa wakisema mabasi yaendayo haraka na na sio yaendayo kasi

KUNA tofauti ya HARAKA NA KASI
Asante kwa kunikosoa inawezekana huku kwetu Tandahimba redio yangu ya mkulima inanidanganya,nitaenda kwa mjumbe kila nikisikia mwendo haraka inaongelewa ili nisidanganye na redio hii,nimechoka kudanganywa!

Nikishindwa nitaomba kuhamia Dar es Salaam.
Kwani mkulima haamishwi na serikali ili kuja kupanda magari ya haraka haya ili tupande bure!
 
Hili limeniuma sana. Serikal ilisema kutakuwa na mabasi yanayoenda kasi. Nmepanda haya mabasi zaidi ya mara 10 wala hayaendi kasi. Hayo ya kasi watatuletea lini?
Haya si haba hayasimami vituo ving sana kama daladala na hayana traffic jam but hayana kasi ambayo nlidhania yangekuwa nayo kama yanavyoitwa.
Kwa wale tulioenda nje ya nchi nadhan tunafaham train za kasi... Nlidhan at least hata kwa asilimia 40 tungekuwa na basi za namna hiyo. Kwa nini mlitudanganya?
Panda Bodaboda utaenda kasi mpaka kaburini! Hatuna shukrani kabisa!!!
 
Mtoa mada umenichekesha sana.Yaani unataka haya mabasi yaende mwendo wa treni za ulaya.!!?
Basi ni basi na litabaki kuwa tofauti na treni.

Hata hivyo, kwenda Kasi si lazima kuumanishe kwenda haraka tu.Kwenda Kasi kwaweza kumaanisha kutumia muda mfupi kufika kwenye uelekeo kulinganisha na hapo awali.

Wewe waweza kutuambia kama ukitumia hayo mabasi unafika mapema kuliko hapo awali.
 
Back
Top Bottom