ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 620
- 1,543
CHAMA CHA ACT WAZALENDO
---------------------------------------------
KAMATI YA BUNGE NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA MUHIMU KWA UMMA.
Ndugu wanahabari na watanzania kwa ujumla.---------------------------------------------
KAMATI YA BUNGE NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA MUHIMU KWA UMMA.
Mtakumbuka kwamba jana tarehe 13,04.2016 mmoja wa vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) bwana Augustine Matefu alizungumza na waandishi wa habari na kuzungumzia masuala kadhaa huku akirusha tuhuma kwa wabunge na wafanya biashara mbali mbali mbunge na kiongozi wa chama chetu cha ACT-WAZALENDO ndugu Zitto Ruyagwa Kabwe.
Tuhuma zake zisizo na msingi bwana Matefu zinaweza zikatafsiriwa katika makundi makuu matatu kama ifuatavyo
i. Hofu ya rais wa Chama chake kushindwa kuongoza na hivyo kuandaa mazingira ya kuogopa kupingwa na kwamba kila atakayemkosoa basi atakuwa ametumwa.
ii. Kujipendekeza kwa viongozi wa chama chake kama wanavyofanya vijana wenzake wa CCM kipindi hiki wanachojiegemeza na viongozi wa Serikali kusubiria uteuzi wa Ukuu wa wilaya (U-DC) na hivyo kujitia upofu hata kwa vitu vilivyo wazi na kuonekana kabisa.
iii.Kujitwisha utetezi wa tuhuma za ubadhilifu zinazomkabili Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Bwana Charles Kitwanga za zaidi ya Shilingi Bilioni 34 kupitia kampuni yake ya Infosys iliyoshirikiana na Kampuni ya Lugumi katika mkataba wa Kifisadi walioshindwa kuutekeleza kama ilivyoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari hivi karibuni.
Kwa msingi huo basi, kwa niaba ya Kamati ya Vijana ya Chama cha ACT-WAZALENDO. Tunamtaka ndugu Matefu na vijana wengine wote wa UVCCM na vyama vingine, ambao wameamua kujitwisha usemaji na utetezi wa wanasiasa,wafanyabiashara na taasisi mbalimbali kwa kuanzisha majina na ama majukwaa ama viji taasisi vya uongo na kweli ili kujipatia pesa na fursa (kama matefu alivyofanya) . waache mara moja kumuhusisha Kiongozi wa chama chetu na tuhuma zote zinazoendana na misingi ya chama chao (Chama cha mapinduzi).
Sio hulka wala mwenendo wa kiongozi wa Chama cha ACT-WAZALENDO kujihusiah na vitendo vyovyote vya matumizi mabaya ya ofisi, kuomba ama kupokea rushwa, na mengine yanayofanana na hayo. Na tabia hii kwa miongo kadhaa sasa imekuwa ikifanywa na viongozi na wanachama wa chama cha mapinduzi CCM (mifano ipo wazi).
Pamoja na mambo mengine. Tunahitaji kuona ifuatavyo
i. Rais John Magufuli, aache kuogopa kivuli chake kwa kuhisi kuna watu wana mpango wa kumuhujumu, mbunge wa chama chetu hatujamtuma kwenda bungeni kumuhujumu Magufuli, tumemtuma kwenda kuwasimamia na kuwapigania watanzania kwa kufuata misingi na itikadi ya ACT-WAZALENDO. Hivyo hatutarajii wala yeye hatarajii kuwa mtetezi wa Rais. Magufuli hata kama serikali yake itapeleka bungeni mapendekezo ya Hovyo.
ii. CCM na Serikali yake itambue kuwa Zitto Ruyagwa Kabwe ni Kiongozi wa chama cha siasa cha Upinzani kilichojipa wajibu wa kuwatetea watanzania, hivyo kamwe hatakuja kuwa mtetezi wa madudu yoyote yatakayofanywa na Magufuli na Serikali yake. Ni wajibu wa Zitto Ruyagwa Kabwe kuhakikisha CCM na Serikali yao inatoka Madarakani sio kuwatetea. Hivyo waache hofu.
iii. Tunamtaka Waziri wa mambo ya Ndani CHARLES KITWANGA aache kujificha kwenye koti la Rais MAGUFULI hasa kwenye hizi Tuhuma zinazomkabili za Kampuni ya INFOSYS kampuni yake binafsi yeye na Rafiki yake Mkurugenzi Mkuu wa NIDA la kuitia hasara serikali zaidi ya Bilioni 34 baada kushirikiana na kampuni ya LUGUMI na kushindwa kukamilisha zabuni waliyopewa. Na Badala yake ajitokeze hadhani na atoe ufafanuzi wa kwanini asipandishwe mahakamani kama wahujumu uchumi wengine walivyofanya.
iv. Tunamtaka Rais. John Magufuli, amchukulie hatua za kinidhamu haraka iwezekanavyo Waziri huyu anayediriki kutumia madaraka yake kusimamia kampuni zake binafsi za kibiuashara na kuitia hasara serikali huku ukizingatia inatumika pesa za walipa kodi masikini. Mpaka sasa Kitwanga anafanya mchezo huu.
Imetolewa leo
14.04.2016 na:-
Wiston A. Mogha
Kaimu Msaidizi wa Katibu Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa
ACT – WAZALENDO