Amani na iwe kwenu,
Baada ya Nacte kutangaza rasmi kuwa wameachia jukumu la kuratibu udahili wa wanafunzi isipokuwa kwa vyuo vya afya na ualimu vilivyopo chini ya serikali, ni muda maalum sasa wa kupeana ujuzi na uzoefu wa vyuo mbalimbali hapa nchini. Huu utakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wanaotegemea kutuma maombi katika vyuo vya kati.
Pia ni ombi langu kwamba kama kuna wahusika wa vyuo mbalimbali humu watusaidie kujitangaza na kutoa maelekezo na ushauri juu ya usajili katika vyuo vyao.
Pia ni vyema mwenye ujuzi wa vyuo mbalimbali vinavyotoa kozi zinazofanana watupatie takwimu kwa ubora (ratings)..
Naamini katika jukwaa hili kuna wengi wapo katika mchakato wa kutuma maombi vyuoni..
Karibuni tuulizane maswali na tuyajibu kadri ya ujuzi na uzoefu.