libeva
JF-Expert Member
- Mar 25, 2015
- 4,446
- 3,593
Sheria ikutungwa na bunge likapitisha na rais akasaini kuna shida?Sifa na kukurupuka kutatugharimu walipa kodi wa nchi hii!
Sheria ikutungwa na bunge likapitisha na rais akasaini kuna shida?Sifa na kukurupuka kutatugharimu walipa kodi wa nchi hii!
Hawa TUCTA hawajitambui, badala ya kumtetea mlala hoi wanahangaika na watu walioridhika na maishaHao TUCTA wameshindwa kutetea kima cha chini; ila wanalalama na watu wanaolipwa 40m/=
Akili zao ndogo sana hawa;
Kaduguda milioni 40 sio hela ndogo kwa mwezi halafu,wengi wao walipewa ili walinde maslahi ya mtu alie wapa.Unafikiri Rais anavyosema ataipunguza hiyo mishahara haelewi huo mchezo??M 40 kwa kazi gani bhana.
Nchi zetu hizi ukisema kufuata shria hufiki
Kweli kabisa Mamndenyu haya majamaa ya TUCTA keshokutwa Mei Mosi yatajichekesha kwa Rais Magufuli yakitaka mishahara juuHao TUCTA wameshindwa kutetea kima cha chini; ila wanalalama na watu wanaolipwa 40m/=
Akili zao ndogo sana hawa;
Katiba ni MWONGOZO wa jamii starabu. Iwe iwavyo,tukiidharau Katiba. Viongozi wetu wasipoongozwa na Katiba, tutakuwa na Jamii isofuata utaratibu. Ni habari ya "mwenye nguvu porini" ndiye atawalaye...unajua siku zote mimi huwa siupendi kabisa usiginaji wa katiba hata kama unanibeba .
Na miye nasubiria kwa hamu jibu la swali hili!Samahani kwa wanaojua; hivi menejimenti, na watendaji wakuu wa taasisi na idara mbalimbali za serikali ni wanachama wa vyama vya wafanyakazi?
Nakubaliana na wewe Lavan Island kwamba ni hela ndefu kwa maisha ya Ki-Tanzania lakini si hela nyingi ukilinganisha na posts za hao watu nje ya Tanzania. Kwa exchange rate ya leo USD 1=TZS 2200 hivyo basi kwa TZS 40M inakaribia ~ USD 18200.00 kwa mwezi. Hii ni hela ndogo sana kwa nchi za wenzetu.
Kuhusu kulinda maslahi ya mtu aliyewapa hizo nafasi, napata kigugumizi ktk hilo. Nina uhakika wengi walipitia mchakato wa Bodi kabla ya kupewa hizo nafasi. Na kama kulikuwa na uchakachuaji, hapo wa kulaumiwa ni Bodi zetu kwa uzembe na kubeba wasiofaa kwenye hizo nafasi. Kama ni majipu ya kutumbuliwa sio mishahara bali ni hizo bodi za hayo mashirika na waliokubali kupitisha muundo wa hiyo mishahara ikiwamo Hazina yenyewe.