TRC: Tunaendelea kusitisha safari za Treni kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,709
13,461
4729696a-849d-43d7-88c1-1d2b9f59be1b.jpg
Dar es Salaam, Tarehe 30 Januari 2024


Shirika la Reli Tanzania - TRC linautaarifu umma kuwa linaendelea kusitisha huduma ya usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam kuelekea mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Katavi, Kigoma na njia ya Kaskazini kuelekea mkoani Tanga.

Shirika limesitisha huduma kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo. mbalimbali nchini na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya reli kati ya Stesheni ya Morogoro na Mazimbu, Munisagara na Mzaganza wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro na Godegode na Gulwe wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma pamoja na eneo la Wami, Ruvu mkoani Pwani na Mkalamo mkoani Tanga.

Wahandisi kutoka TRC wanaendelea na matengenezo katika maeneo yaliyoathiriwa na mvua zinazoendelea. Taarifa ya kurejea kwa huduma ya usafiri wa treni itatolewa mara baada ya kukamilika kwa matengenezo ya miundombinu ya reli.

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na linawasihi wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi cha matengenezo kuhakikisha usafiri unarejea katika hali ya usalama.
 
Back
Top Bottom