TRAB wameitupilia mbali rufaa ya VIP kupinga malipo ya kodi ya ongezeko la thamani kwenye dili lao la kifisadi na PAP. Hili dili ndio bado linawanyonya watanzania vibaya sana hadi leo hii.
Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited ilikata rufaa kwenye bodi ya rufaa ya mapato(TRAB) dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kuzidishiwa kodi ya dola za kimarekani 23,629,434.75, baada ya kuuza hisa zake kwa IPTL.
Katika rufaa iliyokuwa imewasilishwa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, Kampuni ya VIP iliitaka bodi hiyo kuifuta hiyo kodi na kuiamrisha mamlaka TRA kurudisha dola za kimarekani 17,980,934.75.
MY TAKE: Je kesi yake ya kufisadi viongozi waandamizi wa serikali ya CCM na jamii, ni vipi mzee Mlowola wa Takukuru hapo umekaa mkao wa kula nao sahani moja?