TRA bado Trilioni mbili kufikia lengo la makusanyo!!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,950
29,532
Wale wasiopenda kusikia mafanikio ya Serikali ya #Hapakazitu waipate taarifa hii.

TRA imebakiza miezi chini ya miwili ili kumalizia mwaka wa fedha...na imebakiza Tsh Trilioni mbili na point chache ili kufikia lengo.
 
Hizo pesa zimekisaidia nini wew....ushauliza kwanini kitaa watu wanalia njaa huku magufuli anatangaza kukusanya mabilioni ya pesaa! #HapaWIziTu
 
TRA Yabakiza Tshs. Trilioni 2.363 Kufikia Lengo Lao




Na Ally Daud- Maelezo.
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imebakiza Tsh. Trilioni 2.363 ili kufikia lengo waliojiwekea la kukusanya mapato ya trilioni 12.363 katika mwaka wa fedha 2015/16, ambapo hadi sasa imekusanya kiasi cha Tsh. Trilioni 10.
Hivyo TRA inatakiwa kukusanya kiwango hicho kwa mwezi Mei na June,2016 ili kutimiza lengo la makusanyo ya mwaka wa fedha 2015/2016.

Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (katikati) akionesha kitabu cha mtaala mpya wa mafunzo kwa wafanyakazi (TRA) watakaopata fursa za kusoma katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA), kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Prof. Isaya Jairo na kushoto na kushoto ni Kaimu Mkurugugenzi Rasilimali Watu na Utawala Bw. Victor Kimaro.

Baadhi ya washiriki waliohudhuria katika uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango wa mafunzo ya kuhitimu kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa za ajira Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliofanyikia jijini Dar es salaam.

Baadhi ya washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni Rasmi Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata
 
Hizo pesa zimekisaidia nini wew....ushauliza kwanini kitaa watu wanalia njaa huku magufuli anatangaza kukusanya mabilioni ya pesaa! #HapaWIziTu
Ulitaka zigawanywe kama pipi?
 
Hizo pesa zimekisaidia nini wew....ushauliza kwanini kitaa watu wanalia njaa huku magufuli anatangaza kukusanya mabilioni ya pesaa! #HapaWIziTu
Tuliza mzuka Fedha zitakuja tu...nakushauri ufanye kazi ili kupata fedha
 
Wale wasiopenda kusikia mafanikio ya Serikali ya #Hapakazitu waipate taarifa hii.

TRA imebakiza miezi chini ya miwili ili kumalizia mwaka wa fedha...na imebakiza Tsh Trilioni mbili na point chache ili kufikia lengo.
Sina tatizo na mafanikio ya awamu hii ya JPM.

Shaka yangu ni kuhusu hicho kiwango cha lengo linalotakiwa kufikiwa by the end of this fiscal year.

Kwa mfumo uliokuwepo wa ukusanyaji wa kodi uliokuwa umegubikwa na rushwa ya kiwango cha juu, misamaha ya kodi isiyo ya lazima, ukwepaji wa kodi, na kutofuatilia baadhi ya kodi na mengineyo, ni wazi kwamba lengo lililowekwa muda mfupi kabla ya kuanza mwaka wa fedha 2015/2016 lilikuwa la chini sana. Hivyo kwa sasa tunaweza kufurahi kwamba tumefanikiwa au tutafanikiwa kufikia lengo kwa vile waliotuwekea hilo lengo walijua kuwa fedha nyingi iliyotakiwa kukusanywa inapotea kwa aidha kuliwa na wachache au kutofuatiliwa. Hii ni sawa na muuzaji wako wa dukani anaekuibia kila siku na kukupa Tshs. 50,000/=kama mauzo ya kila siku. Baadae huyo muuzaji akakuambia kuwa atajitahidi awe anakuletea 60,000/= (pamoja na wizi wake ambao hakuambii) ambapo mwisho wa mwezi atakuwa amekukabidhi 1,800,000/=. Sasa wewe mwenye duka ukijisifu kwamba muuza duka wako anafikisha lengo unakuwa unajidanganya kwa sababu alikuwekea lengo la 60,000/= kwa siku akijua kuwa fedha nyingine atakuwa anaweka mfukoni mwake.

Kwa kusema hivyo sina maana ya kubeza juhudi za serikali yetu katika kukusanya mapato. Lakini pengine ujivuni wetu uje baada ya TRA ya sasa chini ya management mpya na ufuatiliaji wa karibu wa rais wetu JPM kuweka lengo ambalo limezingatia uzibaji wa mianya yote ya rushwa na ukwepaji kodi na kisha kipindi kama hiki mwakani ndipo tuweze kupima vizuri mafanikio yetu katika kufikia lengo.
 
Jamaa smart sana ... January, February, March wametangaza kwa majidahi kabisa matrilion waliyoyapata.... miezi iliyofuata kimya ..wakaja kivingine ..tunakaribia lengo hehe.
 
Wale wasiopenda kusikia mafanikio ya Serikali ya #Hapakazitu waipate taarifa hii.

TRA imebakiza miezi chini ya miwili ili kumalizia mwaka wa fedha...na imebakiza Tsh Trilioni mbili na point chache ili kufikia lengo.
 
kama lengo lilikuwa hizo trilion 12 sasa ongezeko la makusanyo linalozungumzwa limetoka wapi? Worse ni kwamba bajeti ya serikali ya mwaka huu ambapo imebakiza siku 45 ilikuwa ya hovyo sana maana hakuna wizara iliyopata ziadi ya asilimia 40% na nyingine hazikupata kabisa. Halafu zaidi ya yoote mwaka kesho tumeambiwa ni tril 32 na tunajitegemea wakati hata sukari hakuna. nchi ya kusadikika hii
 
Hii financial year ni ya Kikwete
 
Tusubiri juni tuine kama lengo litavukwa au la...THINK POSITIVELY!

KUHUSUSUKARI TAYARI BODI YA SUKARI IMEAGIZWA KUFANYA KAZI YAKE IKIWA NI PAMOJA NA KUAGIZA SUKARI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…