ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,417
- 9,603
Ndege hii iliyotengenezwa kwa usiri mkubwa ni moja ya fahari ya jeshi la Marekani na inajulikana sana kutokana na umbile lake kufanana na Popo. Ilianza kutengenezwa kipindi cha vita baridi na hadi sasa ndiyo ndege vita ghari kuwahi kutengenezwa duniani ikigharimu dola 2.1 kwa ndege moja(hii ni kwa rate ya dola ya mwaka 1997)
Upekee wa ndege hii ni kwamba sio rahisi kuonekana kwenye rada ya adui kutokana na mfumo wake wa utenengenezwaji kuvuruga mawimbi ya rada za adui,pia ina mfumo wa kisasa wa kieletroniki kushambulia pamoja na kuona kila kilichopo ardhini.
Ndege hii ina uwezo mkubwa wa kubeba silaha kama vile mabomu,makombora(mpk 18000kg)pia ina uwezo wa kubeba mabomu ya nyuklia mpka 16 pamoja na makombora ya masafa marefu ya nyuklia. Ina uwezo wa kwenda umbali wa zaid ya 12000km bila kujazwa mafuta huku ikipaa umbali wa hadi futi 50,000 angani na kushambulia pasipo kuonekana kwenye rada za adui.
Pia ndio ndege pekee ndani ya jeshi la Marekani yenye uwezo wa kubeba mabomu makubwa kwa ajili ya kuharibu ngome za adui zilizopo chini ya ardhi yajulikanayo kama Massive Ordinance Penetrator(MOP).
Hii ndiyo ndege vita nzito kuliko zote duniani ikiwa na uzito wa tani 275.Ndege hii ina uwezo wa kubeba silaha za kivita ikiwemo mabomu, makombora ya masafa marefu na hataa zile za nyuklia yenye uzito wa tani 40,ikiwa ndiyo ndege inayobeba mzigo mkubwa wa silaha kuliko zote ulimwenguni.
Ina uwezo wa kutembea umbali had 14500 km bila kujazwa mafuta. Ina uwezo wa kukimbia kwa 2220km kwa saa.Ina uwezo w kubeba makombora ya masafa marefu kama vile Kh-55,Kh-101,nk.
Kutokana na gharama za utengenezaji na uendeshaji wake inasadikika mpaka sasa jeshi la Urusi lina ndege hizi 16.
Ndege hii ilianza kufanya kazi mwaka 1986 ikiwa na matarajio ya kuchukua nafasi ya B-52.Ina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia.Sifa nyingine za ndege hii pia imeongezewa uwezo kidogo wa kutokuonekana kwenye rada japo sio mkubwa ukilinganiasha na ule wa B2.
Ina uwezo wa kubeba silaha kama vile makombora, mabomu yenye uzito wa hadi Tani 34(34000kg).Hii ndiyo ndege inayobeba mzigo mkubwa wa silaha kuliko zote ndani ya jeshi la Marekani.
Jumla ya ndege hizi 100 zilitengenezwa ila mpk sasa inaarifiwa zipo 70 ndani ya jeshi la Marekani. Inaarifiwa kwamba ndege hiz zitaendelea kufanya kaz hadi mwaka 2030 ambazo nafasi yake itajazwa na ndege nyingine.
Ndege hii ilitengenezwa kwa ajili ya kubeba silaha za nyuklia.Ilianza kufanya kaz ndani ya jeshi la Marekani tangu mwaka 1955.Jumla ya ndege hiz 744 zilitengenezwa zikiwa ni za aina(versions) tofauti tofauti. Mpaka sasa jumla ya ndege hiz 85 zinafanya kaz ndani ya jeshi la Marekani na zinaarifiwa kuendelea kufanya kaz hadi mwaka 2044.
B52 ilimetumika kwenye vita mbalimbali ikiwemo ya Vietnam japo huko kote ilikua ikifanya mashambuliz ya kawaida tu na si ya nyuklia.
Ndege hii ina uwezo wa kubeba mzigo wa silaha hadi tani 32(32000 kg) ikiwemo mabomu, makombora ya aina mbalimbali kama yale ya Cruise na mabomu ya GPS. Ina uwezo wa kwenda umbali had 18500km bila kujazwa mafuta.
Ndege hii inayoendeshwa kwa mapanga boi bado imebaki kama uti wa mgongo kwa taifa la Urusi kwa ajili ya mashambuliz ya masafa marefu.Dhumuni la kutengenezwa kwa hii ndege ni kufanya mashambuliz ya nyuklia moja kwa moja ndani ya Marekani kutokea Urusi.
Ina uwezo wa kubeba mzigo wa silaha hadi tani 15(15000kg) huku ikiwa na uwezo wa kwenda umbali wa hadi 12000km bila kujazwa mafuta japo kuna ndege nyingine za aina hii zilizoboreshwa zinaweza kwenda umbali wa had 15000km bila kujazwa mafuta.
Jumla ya ndege hiz 500 zilitengenezwa ingawa mpk sasa zilizopo ndani ya jeshi la Urusi ni ndege 60.
Ilianza kufanya kaz tangu mwaka 1984 huku ikitegemewa kuendelea kubaki ndani ya jeshi la Urusi hadi mwaka 2040.
Ndege hii ina uwezo wa kubeba mzigo wa silaha had tani 24(24000kg) ikiwemo mabomu na makombora tofaut tofaut. Pia ina uwezo wa kwenda umbali wa had 7000km bila kujazwa mafuta.Ina uwezo wa kukimbia kwa speed had 2300 kwa saa.
Zaid ya ndege 570 za aina hii zilitengenezwa huku mpaka sasa jeshi la Urusi inaarifiwa kwamba ina ndege hiz zaid ya 90.Pia ndege hizi zipo kwenye jeshi la India.
Ndege hii zilitengenezwa kutokana na ndege za kirusi aina ya Tu-16 kwa kukatiwa leseni.
Jumla ya ndege hizi 150 zilitengenezwa.Ina uwezo wa kubeba mzigo wa silaha hadi tani 9(9000kg) ikiwemo mabomu na makombora mbalimbali.
Ina uwezo wa kutembea umbali wa had 3200neutical miles(6000km) bila kujazwa mafuta.
Elungata Chenchele Dotworld MASAMILA izzo nankumene MURUSI SirChief mohamedidrisa789
MTOTO WA KUKU
Bukyanagandi
Sexer