Bila shuka
JF-Expert Member
- Oct 14, 2014
- 596
- 294
Wameipenda wenyewe wacha ishuke tu hakuna namna
Waingizaji wakubwa wa dollar nchini mwetu ni utalii na mauzo ya dhahabu. Bidhaa hizo zote mbili zinauzwa kwa dollar na siyo shilingi. Kama unauza kwa dollar, kuanguka kwa shilingi kutasaidia vipi exports?
Mkuu una takwimu tuna export nini na kiasi gani?
Mimi nadhani kukosekana kwa exports za uhakika ni factor mojawapo ya kudorora kwa shs kulingana na dola hadi kudorora kwa uchumi.
Mkuu ahsante sana sana kwa mchango wako.Takwimu za export na imports zinapatikana kwenye tovuti mbalimbali na sitajaza server ya JF kwa kibarua cha copying and pasting. Takwimu hizo wala sio siri, tovuti ya EAC, World Bank, IMF, na wizara husika kama vile uchumi na fedha utapata hizo takwimu.
Sijui mwenzangu unapoongelea EXPORTS ZA UHAKIKA una maanisha nini haswa! Volume au quality au types?
Upo sahihi demand ya exports zetu ndio zinazoipandisha au kuishusha shilingi yetu. Sasa mada inasema shilingi yetu inaposhuka uchumi unaharibika, na mimi hoja yangu ni kwamba sio kila sarafu inaposhuka uchumi unaharibika. Sarafu ikipanda sana nalo ni tatizo kwasababu exports zinakuwa za bei mbaya. Nchi za wenzetu sarafu yao ikipanda kunakuwa na jitihada za makusudi kuiteremsha.
Kwa nchi masikini kama Tz yenye exports zinazofanana na exports za nchi nyingine za Africa manake sisi ni price takers tu ambao tupo kwenye competitive international market. Hatuna nguvu ya kuongeza bei ya exports zetu na badala yake tunaweza kuongeza kipato kwa kuongeza volume ya exports zetu. Mtihani unakuja pale tunapolazimika kuongeza exports kwa kuongeza imports of machineries and agro-industry machines kwa mfano. Sasa, kwasababu sarafu yetu haina nguvu ku-command imports uwezo wa kuongeza exports nao unakuwa mdogo. Sasa swali linakuja: tu import bidhaa gani? Je hizo bidhaa ambazo tunaweza kuzipotezea tunazizalisha efficiently? Maswali haya ndio yanatufanya tuwe kwenye mfumo wa yai na kuku au gurudumu la umasikini ambalo hata mwagwiji wa uchumi duniani wameshindwa kutukwamua na hakuna dalili ya kukwamuliwa. Of course yapo mengine ya kando ambayo tunayasababisha wenyewe.
Suala la athari za kuteremka kwa sarafu katika uchumi sio suala linalojibika kwa urahisi hasa katika nchi masikini kama Tz. Na tunapojadiri suala hili lazima tuwe makini kutofautisha UCHUMI (unaopimwa kwa GDP) na MAENDELEO ya watu (yanayopimwa kwa kutumia vipimo kadhaa). Kwasababu, sarafu inaweza kushuka na uchumi ukakuwa na maendeleo yakapatikana. Vilevile sarafu inaweza ikapanda, uchumi ukashuka, na maendeleo yakapatikana. Pia inawezekana uchumi ukashuka, maendeleo yakapatikana au kutopatikana. Hivyo sarafu haina uhusiano wa moja kwa moja na kukua kwa uchumi na hivyo kupatikana kwa maendeleo.
Mkuu ahsante sana sana kwa mchango wako.
1. Je serikali ina mkakati unaoweza kubadirisha hali hii ya kuporomoka kwa shilingi kulingana na dola (kama unafahamu)? Mifano usimamizi wa ubadirishaji pesa kwenye bureau de change; makampuni ya utalii yanayolipwa nje ya nchi na watalii
2. Uzoefu wangu kwenye kilimo cha mkulima mdogo zamani (60s-70s) kulikuwa na uhakika wa soko hata kwa debe moja la mazao. Sasa hivi ni shiida. Watawala hawaoni fursa ya kutuhusisha wakulima kwenye uhakika wa masoko ya uhakika ya mazao yetu? Naamini hapa nasi tutakuwa tunashiriki kwenye uchumi wa taifa na kufaidika na mzunguko wa fedha.
3. Zamani kulikuwa na maafisa wataalamu wa kilimo ufugaji uvuvi waliokuwa kwenye vijiji vyetu. Hawa walikuwa wanasimamia nyenzo katika eneo husika km mtrekta pampu za maji mizinga. Mbona sasa kila mtu na lwake hadi uzalishaji umeshuka? Hii si inachangia kushuka kwa uzalishaji na kushuka kwa kipato hata cha kujikimu. Najua kuna nchi waliweka mkakati wa kujitosheleza soko la ndani. Je sisi tunajitosheleza kiasi gani kwa soko la ndani kwa mahitaji yote? Bidhaa za viwandani na vyakula.
Hoja ziendelee