wana JF
Salaam
Siku moja baada ya madhara ya mvua kubwa iliyonyesha na kuonekana katika mikoa ya Daresalaam, Pwani, Morogoro, Ruvuma, Iringa na maeneo kadhaa ya nchi na watu kadhaa kuathirika na mvua, Serikali kupitia mamlaka zake za mikoa itaanzisha operesheni ya kuwaondoa wakazi wanaoishi mabondeni mikoani hasa mabonde ya Msimbazi na jangwani jijini Daresaalam ambayo ndiyo yanayoathirika zaidi kila mwaka, mojawapo ya madhara yaliyoletwa na mvua hizo ni watu kukosa sehemu za kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa na maji ya mvua kubwa vilevile kupoteza thamani zao za ndani na mifugo kwa ujumla,aidha watoto kukosa kwenda shule kutokana na maji kujaa kila maeneo ya nyumba zao
Chanzo: Nipashe