Nianze hivi,
Jana nimepoteza au niliibiwa simu yangu yenye line ya tigo na voda ndani yake. Bahati nzuri niligundua kua nimepoteza/nimeibiwa simu hiyo muda mfupi tu kwani nilikua nayo kwa mara ya mwisho muda si mrefu kabla ya kugundua sinayo. Muda huohuo nikaomba simu ya jamaa yangu nikawapigia tigo na voda kuwataarifu. Waliniuliza namba yangu ni ngapi, salio lililoko na watu ninaowasiliana nao ili wahakikishe kua mimi ndio mwenyewe mmiliki wa hiyo namba.
Cha ajabu kilichonifanya niandike uzi huu ni kua walinijibu kua wao watafunga au ku-block ile tigopesa tu, lakini mawasiliano watayaacha kama walivyo, yaani yule mwizi alie nayo anaruhusiwa kufanya mawasilano yoyote ya call, SMS, whatsapp, etc kwa kutumia simu yangu kasoro tu tigopesa ndio hatakiwi kugusa!!!!! Hizi call, SMS, whatsapp etc zote hazihitaji password kutumia, badala mnge block hizi, eti mme block tigopesa ambayo inatumia password.
Nimewaombeni chondechonde huyu mwizi anaitumia simu yangu vibaya kuomba pesa kwa ndugu zangu akijifanya ni mimi, please ifungieni hiyo simu mmekataa. Hivi navyoandika hapa nadaiwa kiasi cha tshs 540,000/= ambazo ndugu na rafiki zangu walituma kwa maelekezo kutoka kwenye simu yangu ambayo mlikataa kui-block, this is unfair.
Nilipiga pia simu voda kuwaomba waifunge mawasilano yote wakakubali, mbona wao hawakuona hizo sababu mlizoziona nyinyi?? Kweli nyinyi ni Jipu au lah basi mnalea majipu.