The SGR War: Wakati Kenya wakisuasua, Uganda wameamua kujenga SGR. Hii ni fursa kwa SGR ya Tanzania. Is it viable? Tuichangamkie?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,685
119,325
Wanadodi,

Leo nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu za kwa Maslahi ya Taifa, leo nikianzia kuibuka kwa fursa mpya kwenye reli ya SGR ya Tanzania, karibu.

Wakati Tanzania tukiendelea na ujenzi wa reli yetu ya SGR, shughuli nzito kwenye SGR sio ujenzi, bali ni kuiendesha kwa faida. Ili SGR iendeshwe kwa faida, ni lazima iwe na kitu kinachoitwa linkages, yaani muunganisho kati ya nchi moja na nyingine, ili hiyo SGR ipate mzigo wa kushiba na ku operate kwa faida.

Kwa nchi za Afrika Mashariki, Kenya ikitumia mtindo wa "ujanja kuwahi", ikawa ndio nchi ya kwanza kuchangamkia fursa hivyo ikajenga SGR ya Mombasa-Nairobi-Naivasha-Malaba, ili mzigo wa Uganda na Rwanda upitie bandari ya Mombasa, na Uganda ingejenga SGR kupokea mzigo wake na wa Rwanda na kuufikisha Kigali. Hivyo the linkaje ya mzigo wa Uganda na Rwanda, ndio roho ya SGR ya Kenya, Mchina kupitia benki yake ya EXIM akakubali kugharimia kila kitu.

Kumbe "ujanja nsi kuwahi, ni kupata", JPM baada tuu ya kuchaguliwa,ziara yake ya kwanza nje ya nchi, ni kutembelea Rwanda, wakakubaliana SGR ya Tanzania itaungana na ya Rwanda. Hivyo kitendo tuu cha kukubaliana SGR ya Tanzania itajiunga na Rwanda, ile linkages ya SGR ya Uganda kwenda Rwanda, ikakatika, hivyo SGR ya Kenya kuunga Uganda haitakuwa na faida, hali hiyo ikikapelekea mfadhili kujitoa kuendeleza SGR ya Kenya sasa itaishia Naivasha, na hakuna funding tena ku fund SGR ya Uganda!.

Baada ya mchina kugoma kugharimia SGR ya Uganda, MU7, nae kaamua kumfuatilisha JPM kwa kuamua kujenga SGR ya Uganda hata kama Kenya anasuasua. Uamuzi huu wa Uganda kujenga SGR yake bila kuitegemea Kenya ni fursa nyingine kubwa kwa SGR ya Tanzania na Bandari ya Dar es Salaam kubeba mzigo wote wa Uganda.

Ili sisi Tanzania kuweza kuichangamkia fursa hii mpya, sasa hapa ndio "ujanja kuwahi", kwa kujenga SGR ya Mwanza fasta, ili mzigo wa Uganda ushuke Dar, ukimbizwe Mwanza, uvushwe ziwa Victoria hadi Uganda. Hili likifanyika, sio tuu, Bandari ya Dar itabeba cargo ya Uganda tuu, bali cargo kutoka South Sudan na North Eastern DR Congo itapitia bandari ya Dar es Salaam kupelekwa Mwanza. Changamoto pekee, in umbali wa route hii, kama italipa, na changamoto ya hatari zaidi, ni bada ya MU7 kuamua kujenga SGR, Kenya anaweza na yeye kuamua kukijenga kipande cha Naivasha-Malaba.

Background.
Taarifa za Uganda kujenga nmezisoma hapa Uganda plans to go it alone and build 2,700km-long standard gauge railway.

SGR ndio kipimo cha the economic super power of EAC, hivyo ni vita kubwa.




My Take
Kama tumeweza kuwapiga Tanchi kwenye SGR ya kuunganisha na Rwanda, kisha tukawapiga Tanchi kwenye bomba la mafuta la Uganga, Tanzania tukifanikiwa kuifikisha SGR yetu, Mwanza, hadi Kigoma, na pia tukajenga SGR to Tunduma, Tanzania ndio itakuwa the super power of EAC Region, na kama tukiifanya Dar Port kuwa a free port kwa baadhi ya bidhaa, with The AfCFTA in place!, Tanzania will fly!, no one will catch us!.

Nawatakia Jumapili Njema.

Paskali
 
Utajikomba sana mwaka huu lkn hupati uteuzi hata wa mjumbe wa nyumba kumi.

Kwa taarifa yako Kenya SGR tayari ishaanza kuingiza kipato,wananchi wa Kenya wamesha anza kuonja manufaa ya SGR .

Tangu mwezi wa November SGR ilikuwa imeshajaa hadi januari kwa wingi wa abiria.
 
Inategemea nano yuko madarakani na mahusiano yao yakoje kwa wakati husika, hivyo hiyo fursa hata kama ipo, sio reliable kutegemea na mahusiano ya nchi na nchi kwa wakati husika.

Kwa nchi zetu hizi, akija mtawala X anavuruga kila kitu na kuanzisha analoona linafaa na mnabaki kumuangalia tu mpaka muda wake uishe.
 
Umezungumzia suala la Tanzania kuwahi lakini swali la msingi sijaona mahala ulipozungumzia, je, Tanzania kama nchi tuna uwezo wa kujenga SGR peke yetu au mpaka mkopo? na huo mkopo hautakuwa na masharti, au yakiwepo yatakuwa ya aina gani?

Tunaweza kukimbilia kujenga SGR just for the sake of it, lakini mwisho wa siku asilimia kubwa ya mapato yake yakarudi kwa mfadhili kama sharti la uwekezaji uliofanyika kwa mgongo wake, na hiki ndicho kinachowaumiza wakenya, asilimia kubwa ya walioajiriwa kwenye huo mradi ni wachina, na hata hao waganda nao wakiingia kichwa kichwa wataishia huko huko.
 
Umezungumzia suala la Tanzania kuwahi lakini swali la msingi sijaona mahala ulipozungumzia, je, Tanzania kama nchi tuna uwezo wa kujenga SGR peke yetu au mpaka mkopo? na huo mkopo hautakuwa na masharti, au yakiwepo yatakuwa ya aina gani?

Tunaweza kukimbilia kujenga SGR just for the sake of it, lakini mwisho wa siku asilimia kubwa ya mapato yake yakarudi kwa mfadhili kama sharti la uwekezaji uliofanyika kwa mgongo wake, na hiki ndicho kinachowaumiza wakenya, na hata hao waganda wakiingia kichwa kichwa wataishia huko huko.
Naona mkuu Pascal Mayalla analeta siasa kwenye mambo makubwa ya uchumi.
 
Paskali nahisi umemka umelewa, umeamka na mada za propaganda si propaganda bali vichekesho vitupu. SGR yetu kipande cha Dar-Moro tuliambiwa mwezi wa Nov 2019 kitakuwa kimekamilika, hadi sasa hakijakamilika na tunaambiwa kitakamilika Aprili 2021! Na kuna tetesi kuwa fedha zinasumbua kwenye huo mradi ndio maana simu ilipigwa kwa rais wa China. Unazungumzia mradi kufika Mwanza huku hata kipande cha 300km kimechekua zaidi ya 3yrs na bado hakijamilika!

Hao Uganda wana mradi wa bomba la mafuta, ilisainiwa toka 2017, na matarajio ingekamilika 2020. Lakini mpaka sasa haujaanza na hata kama ni kuanza ni kwa kusuasua. Sasa hapo unaoongelea mambo ya mradi wa SGR si vichekesho hivyo? Nikikumbuka ule utapeli wa sarafu ya pamoja ya E. Africa, kisha nikiona hizi mada zako kuhusu hawa matapeli, nacheka kwa nguvu.
 
Back
Top Bottom