Mkuu MK254.
Kama unataka kusafiri bila matatizo ya kuomba viza, fanya kazi kwa bidii ili ununue uraia wa nchi zenye vikwazo vidogo vya kusafiri.
Kuna scheme nyingi tu za kununua uraia wa Bulgaria, Ugiriki, Spain na Malta kwa kununua nyumba ya $500,000. Viza unayopewa ya kuishi inakupa haki ya kuomba uraia baada ya miaka mitano.
Kama huna muda, kuna nchi zenye pasipoti zinazoheshimika huko Caribbean wanaziuza bila hata ya kuishi huko. Wapalestina na Wasomali matajiri huwa wanazinunua kihalali ili waweze kusafiri bila ya vikwazo.
Hata wanasiasa wanaonyanganywa uraia wananunua pasi hizi ili waweze kusafiri hihalali.
Mmoja wao ni Waziri wa Zamani wa Thailand aliyopinduliwa na wanajeshi, Thaksin Shinawatra. Inasemekana bilionea huyu ana pasi za nchi sita, zote kanunua kwenye mtandao.
Kama huna hela, soma. Kanada na Australia wanakupa uraia chini ya miaka minne wakikukubali kukupa viza kwa kutumia elimu yako.
Dunia ya leo, pasi ni biashara, matatizo ya kusafiri na vikwazo ni kwa walalahoi tu. Wenye pesa na elimu haiwasumbui.