Habari wakuu wanajukwaa hili la siasa
Kuna tetesi zimezagaa mtaani kwetu ya kuwa,kuna kiwanja cha soko eneo la KIBAGA kama unaenda katika mitambo ya songas kimeuzwa na walionunua wanaanza kujenga,
Inasemekana diwani wetu kupitia CHADEMA ameshindwa kukipigania eidha amepewa kitu kidogo ama anawaogopa walionunua au kuuza.
Kama chama kinavyojinasibu juu ya maslahi ya taifa,tunaomba mumsaidie kufuatilia diwani wetu GREYSON na ikiwa ni kweli basi wapiganie wakirudishe kiwanja hicho kama kilivyorudi kiwanja cha wazi katika shule ya msingi Kinyerezi.