Tengeneza mkakati leo kwa ufanisi wa biashara yako

girl-shopping.jpg

Mteja;
"Siku hizi huduma zenu si nzuri kama ilivyokuwa mwanzo"

Uongozi; "Samahani, kila mtu ana siku yake (good and bad day), tutafanya juhudi kukuridhisha, japo hatuwezi kuwa wakamilifu kwa kila kitu"

Mteja; "Kwanini inanichukua muda mrefu kupata huduma zenu? "

Uongozi; " Samahani, kupata huduma zetu zilizo bora, huna budi kusubiri, na hata wateja wetu wanalifahamu hilo"

Ni kawaida katika biashara kukutana na mazingira ambayo wewe kama mteja yatakusuma kuja na maswali au malalamiko (complaints) kama tuonavyo hapo juu, na mara nyingi kwa baadhi ya kampuni/biashara; uongozi huja na majibu kama baadhi tuyaonayo hapo juu.

Mkakati (Strategy); ni nguzo muhimu sana katika makuzi ya biashara/kampuni, hususani katika mazingira ya sasa yaliyo na ushindani madhubuti. Katika orodha ya kampuni 100 bora na zenye mafanikio (Forbes 100) ya mwaka 1917, ni kampuni 13 tu zimeendelea kuwepo mpaka leo, na hii imetokana na kampuni hizi kuwa na Mikakati madhubuti iliyoisaidia kukabiliana na ushindani sokoni. Hivi karibuni kampuni ya McKinsey & Company walifanya "survey" kwa CEOs 800 wa makampuni mbalimbali duniani, zaidi ya asilimia 90 ya hawa CEOs walikiri faida ya utumiaji wa Mipango Mkakati katika ushindani sokoni.

Mpango Mkakati hutekelezwa kwa kutumia "tools" mbalimbali; miongoni mwa "tools" hizo; ambazo ndizo za msingi kabisa ni;
  • Programs/miradi
  • Bajeti (Budget)
  • Taratibu (Procedures)
Baada ya program/miradi na bajeti kupitishwa katika utekelezaji wa Mpango Mkakati, kampuni, au biashara hupaswa kuzingatia/kuangalia taratibu ambazo huongoza watendaji wa kampuni/biashara katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku, taratibu hizi kitaalamu hujulikana kama; Standard Operating Procedures (SOPs)
Taratibu hizi hupaswa kuhuishwa (be updated) na hata kubadilishwa ili ziweze kuendana na matakwa ya Mkakati husika unaotekelezwa. Taratibu (procedures) zilizo andaliwa kikamilifu na kiustadi (well planned procedures), husaidia kuondoa hali dhaifu ya utoaji wa huduma (poor service delivery), kwa kuwalazimisha watendaji wa kampuni/biashara kufanya shughuli zao kwa tabia maalum (behavior created by imposed procedures) hivyo kutotumia visingizio katika kuhalalisha utendaji wao mbovu dhidi ya wateja.
Kwa kufanya hivi wateja watakuwa na ridhiko (satisfaction) juu ya huduma za kampuni /biashara husika, hivyo kutosikika malalamiko toka kwa wateja kama miongoni mwayo yalivyoainishwa hapo juu, hali hii itaitengenezea kampuni/biashara husika faida kiushindani (competitive advantage) na hatimaye kuweza kuwapiku washindani wake sokoni.

Ahsante

The Consult; + 255 719 518 367 (Call for service need)
Dar es Salaam

Project Management, Strategic Management & Brand Management
Choose It, Embrace It, Love It.
 
Ahsante sana kwa elimu@The consult,ila naomba kuelimishwa kdogo kuhusu vigezo zinavyotumika kuanisha(Identify) au kujua kama kampuni "A" kama imefikia ngazi ya Corporate level,Business level au functional level?
 
Ahsante sana kwa elimu@The consult,ila naomba kuelimishwa kdogo kuhusu vigezo zinavyotumika kuanisha(Identify) au kujua kama kampuni "A" kama imefikia ngazi ya Corporate level,Business level au functional level?
Mkuu@Equity utokeaji wa levels (Corporate, Business & Functional level) si lazima uwe kwa hatua, mara nyingi hutokea kwa wakati mmoja, na HUTEGEMEA KAMPUNI INAVYOENDESHWA (Strategic Management).

Kampuni inayoendeshwa KIMKAKATI bila kujali kiasi cha mtaji; ngazi hizi hutokea, ambapo ngazi ya CORPORATE LEVEL itakuwa na majukumu ya;
-Kuangalia overall direction ya kampuni.
-Ku-deal na strategies kama STABILITY, GROWTH na RETRENCHMENT.

BUSINESS LEVEL, itapaswa kuwa na majukumu ya;
-Kuangalia muelekeo wa biashara (Huduma au bidhaa husika) zinazozalishwa na kampuni. Kwa mfano; CLOUDS TV hii ni service iliyo katika business level chini ya corporate level ambayo ni CLOUDS MEDIA GROUP. Mara nyingi strategies ambazo hutumika katika ngazi hii ni USHINDANI (competitive) au UBIA (cooperative)

FUNCTIONAL LEVEL, itapaswa kuwa na majukumu ya;
-Kuangalia uelekeo na utendaji wa idara chini ya business level, mfano Idara ya Uhasibu n.k
 
Back
Top Bottom