TCRA inachunguza mabadiliko ya mabando ya simu yaliyofanyika kimyakimya

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,661
6,395
Bando.JPG
Baada ya malalamiko mitandaoni kuwa kampuni za mawasiliano ya simu Nchini Tanzania zimefanya mabadiliko ya kushusha vifurushi vya huduma za intaneti (mb's) pasipo kutoa taarifa kwa wateja wao, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema inafuatilia.

TCRA imesema: “Tumeona malalamiko kutoka kwa wadau mtandaoni kuwa watoa huduma wa mitandao ya simu wamebadilisha vifurushi kimyakimya, endapo kuna mtumiaji amenunua kifurushi, halafu akapata tofauti na kile alicholipia, awasiliane nasi.

“Mamlaka inafuatilia suala hili kwa watoa huduma ili kuweza kubaini ukweli.”

Yaani kilichofanyika ni kuwa kwa fedha ileile unapata MB chache tofauti na ilivyokuwa awali, mfano unanunua kifurushi cha Tsh 2000 ulikuwa unapata GB 1, sasa hivi ukinunua kwa gharama ileile unapata MB 900 Aau MB 800.
 
Yaaan mitandao ya simu wanatupatia huduma kama vile wanatupatia bure

Yaani wakiamua hata kukata internet wanakata na hakuna hata hatua wanazochukuliwa

Mfano Tigo wapo vizuri kwa kwenda emergence ila sasa sijawah kuona hata wakipewa onyo na sisi wananchi tukajua

Nchi kama SA mitandao hupigwa faini kubwa kubwa ili wajifunze kuheshimu wateja

Mabando gharama ila bdo na kuisha yanaisha bila mpangilio wa kueleweka.
 
Tuulizane kwanza wakuu

Kwan Wao tcra wanatumia mitandao ya simu tofaut had SS tuwatumie ujumbe wao wenyewe wakinunua wanaona mabadiriko kabisa kuwa bando zimepanda

Nchi hii mwenye mamlaka hajui afanye nn

Wanajua Sana sema kampun za simu zimewaweka kwapani hawafurukuti kabisa hata miez sita haijafika wamebadili tena hawaigop serikali

,,,WANGEFANYA HAYA ENZ ZA MAGU,,,,

rostam aziz anamilik tigo na zantel Nan anaweZA MNYOSHEA KIDOLE Kama anafadhiri had safari za mkuu wa nchi
 
"endapo kuna mtumiaji amenunua kifurushi, halafu akapata tofauti na kile alicholipia, awasiliane nasi."

Hii inaonesha kbsa TCRA hawapo serious tangu lini mtu ununue MB 800 afu ukapewa MB700. Yaan wanatoa mianya ya upigaji hadi mda waliopanga wenyewe.
 
wapuuzi sana yani wanatuona sisi mafalaaa... kesi sio kupewa kifurushi tofauti kesi ni vifurushi vimebadilishwa.
 
Nimeshangaa huyu waziri kug'aka kuwa Dar Mpya wameripoti uzushi juu ya mabando ya intaneti kupungua. Mfano Tigo walikuwa na kifurushi cha Sh 1500 na ulikuwa ukipata Gb 1 kwa wiki. Lakini sasa ni Mb 900 kwa bei ileile.

Voda wao walikuwa na Gg 1 kwa elfu mbili kwa wiki lakini sasa ni Mb 800.

Sasa Darmpya wana kosa gani kuripoti hii kadhia mpaka unag'aka?

👇View attachment 2208778
Jibu :Hii inchi ina mambo ya hovyo
 
Baada ya malalamiko mitandaoni kuwa kampuni za mawasiliano ya simu Nchini Tanzania zimefanya mabadiliko ya kushusha vifurushi vya huduma za intaneti (mb's) pasipo kutoa taarifa kwa wateja wao, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema inafuatilia.

TCRA imesema: “Tumeona malalamiko kutoka kwa wadau mtandaoni kuwa watoa huduma wa mitandao ya simu wamebadilisha vifurushi kimyakimya, endapo kuna mtumiaji amenunua kifurushi, halafu akapata tofauti na kile alicholipia, awasiliane nasi.

“Mamlaka inafuatilia suala hili kwa watoa huduma ili kuweza kubaini ukweli.”

Yaani kilichofanyika ni kuwa kwa fedha ileile unapata MB chache tofauti na ilivyokuwa awali, mfano unanunua kifurushi cha Tsh 2000 ulikuwa unapata GB 1, sasa hivi ukinunua kwa gharama ileile unapata MB 900 Aau MB 800.
Jibu litakuja "vita vya Ukraine na Urusi"

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom