Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 752
- 1,810
Chama cha wafanyabiashara Mkoa wa Arusha TCCIA, Kimeunga mkono jitihada zinazofanywa na halmashauri ya jiji la Arusha kwa kuyaboresha maeneo yote yenye uoto wa asili ili kukuza kivutio cha utalii katika jiji la Arusha.
Akiongea wakati wa zoezi la kuboresha mazingira hayo lililoratibiwa na jiji la Arusha na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa mazingira Mkoani hapa afisa wa TCCIA Mkoa wa Arusha, Charles Makoi alisema chama hicho kimekuwa mdau mkubwa mazingira.
Alisema kuwa chama hicho kupitia Mradi wa kuboresha na kukuza utalii jiji la Arusha kimekuwa kikiwezesha halmashauri hiyo pamoja na kuhamasisha wadau wengine kuweza kushiriki zoezi la kustawisha mazingira kwa kuotesha Miti.
"Leo tumeshiriki zoezi wa kufanya usafi na kuotesha Miti zaidi ya 1500 sisi Kama TCCIA jukumu letu ni kushirikiana na halmashauri ya jiji la Arusha kustawisha mazingira ili kukuza kivutio cha utalii "alisema
Kwa upande wake meya wa jiji la Arusha Maximilian Iranghe ambaye aliongoza mamia ya wakazi wa jiji hilo kufanya usafi maeneo ya mto Naura na Ngarenaro na kupanda miti katika eneo la Themi, alisema jambo hilo ni mpango wndelevu unaolenga kutunza mazingira na kuibua vivutio vya utalii vilivyoko katika jiji la Arusha.
"Zoezi hili la Upandaji miti na kusafisha Mito linalengo la kuvutia utalii na kufanya jiji la Arusha liendelee kuwa kitovu cha utalii"alisema Iranghe.
Alisema jiji la Arusha lina vivutio vingi vya utalii kama mito na milima lakini vilisahaulika ila mkakati uliopo kwa sasa ni kuyaboresha maeneo hayo ili yaweze kutumika kama kivutio cha watalii na kuongeza kipato kwa halmashauri.
Zoezi hilo la kuboresha mazingira ambalo ni endelevu limeshirikisha madiwani kadhaa wa jiji la Arusha, bonde la maji la mto pangani, Viongozi mbalimbali wa CCM pamoja na vikundi vya vijana ambao wamejitolea kupanda Miti na kufanyiwa usafi moto ili kupata hewa nzuri ya kupumzikia kwa wageni.
Ends....