TBC kutorusha matangazo ya Bunge live, UKAWA wameshindwa kuwatetea Watanzania?

Taarifa ya habari jana usiku saa 2 ilisema TBC watarusha tu matangazo bunge ya maswali na majibu asubuhi na yale mengine yatatafutiwa kipindi maalum. Huu utaratibu mpya ulipotangazwa bungeni na wazari mwenye dhamana UKAWA walikataa na kudai watahakikisha wananchi wanapata matangazo ya bunge live. Leo bunge linaanza tena na ni bunge la muhimu sana kwani ni la bajeti, sasa wananchi tunakosa fursa ya kuliona na kusikiliza kinachoendelea bungeni. Ukawa mnasemaje kuhusu bunge kutorushwa live? UKAWA mmeshindwa kutetea wananchi wapate haki zao za msingi kama katiba inavyodai kila mtu ana haki ya kutoa na kupata habari?

imebidi nicheke sana mana kuna wabunge wengine wapo kwa ajili ya kuitetea serikali yani wa kutoka ccm na katiba itakuwa inawatambua kama wao watetezi wa serikali .. NA UKAWA WAPO KWA AJILI YA KUTETEA WANANCHI MNAONA UMUHIMU WA UKAWA KTK MATUKIO NA BADO KURA MNAMPIGIA MKOLONI MWEUSI HIVI MNAFIKIRIAGA KABLA YA KUANDIKA NA KUPOST?

SAIV TBC RADIO WAMEKATA MATANGAZO YA BUNGE WAMEHAMIA KTK UZINDUZI WA DARAJA LA KIGAMBONI CCM BANA.
 
Kwan Tanzania nzima wabunge wote ni waukawa? Au nikutaka kukejeli tu,au bunge linaongozwa na ukawa? Ccm wao mbona huwasemei au wao ni wanamwakilisha Nani pale Bingen?
 
Kama wamesema watatafutia kipind maalum sio mbaya tusubiri. Lakin kama wewe mtoa mada tukiangalia bunge mda wote tupo kideon kuanzia asubuh mpka litakapoisha kazi tutazifanya saa ngapi? Mbn hakuna tofaut na wacheza pooltable. Napenda tuangalie recorded tena muda iwe kuanzia saa 1 jion.haya ndo maon yangu
saa moja jioni sisi wengine tupo kazini na wengine wanaangalia mpira live
 
Mimi sio UKAWA lakini ntawashangaa wabunge wa CCM wakikubali huu uamuzi, kwa nini wanafanya mambo kisiasa namna hii, maana hata Tv binafsi wamekatwazwa kurusha live isipokuwa kwa kupitia studio ya bunge. Tusikubali ubakaji huu..
Mbona Startv inaonyesha Bunge jamani!
 
Taarifa ya habari jana usiku saa 2 ilisema TBC watarusha tu matangazo bunge ya maswali na majibu asubuhi na yale mengine yatatafutiwa kipindi maalum. Huu utaratibu mpya ulipotangazwa bungeni na wazari mwenye dhamana UKAWA walikataa na kudai watahakikisha wananchi wanapata matangazo ya bunge live. Leo bunge linaanza tena na ni bunge la muhimu sana kwani ni la bajeti, sasa wananchi tunakosa fursa ya kuliona na kusikiliza kinachoendelea bungeni. Ukawa mnasemaje kuhusu bunge kutorushwa live? UKAWA mmeshindwa kutetea wananchi wapate haki zao za msingi kama katiba inavyodai kila mtu ana haki ya kutoa na kupata habari?

umetambua ni upinzani tu ndio wanaotetea haki za wananchi
 
Ukawa hamna kitu kabisa,hawana strategies kabisa,sasa naamini Dr. Slaa ndo alikuwa kila kitu CHADEMA
Kwani mwenye jukumu la kuwatetea wananchi ni mbunge wa UKAWA pekee?
je wa CCM wenyewe kazi yao ni nin bungeni?

Kabla hujawawalaumu UKAWA angalia kwanza jimboni kwako mbunge wako ni wa chama gani afu uwakosoe
 
Unaposema wabunge wa ukawa wameshindwa, ina maana wabunge wa ccm wako pale kuitetea serikali?! Au unataka kuwaaminisha watu wabunge wa upinzani ndio wanaibeba Tanzania ya sasa bila kushirikiana na ccm, hoja ilikuwa wabunge wasiwe mawaziri ila ccm wakagoma, waziri wa habari ni mwana ccm kindaki ndaki, amaeamua kulinda maslahi ya serikali yake yasiumbuliwe hadharani, ungetumia busara kumkumbusha nape wana mtama wanataka umuona bungeni live akiwa tetea, sio kuja na story kinyume.
 
Kwani mwenye jukumu la kuwatetea wananchi ni mbunge wa UKAWA pekee?
je wa CCM wenyewe kazi yao ni nin bungeni?

Kabla hujawawalaumu UKAWA angalia kwanza jimboni kwako mbunge wako ni wa chama gani afu uwakosoe
nini maana ya upinzani?
 
Kama wamesema watatafutia kipind maalum sio mbaya tusubiri. Lakin kama wewe mtoa mada tukiangalia bunge mda wote tupo kideon kuanzia asubuh mpka litakapoisha kazi tutazifanya saa ngapi? Mbn hakuna tofaut na wacheza pooltable. Napenda tuangalie recorded tena muda iwe kuanzia saa 1 jion.haya ndo maon yangu
Mkuu samahani kidogo kwani watu wanaangalia bunge tu
Kama watu hawafanyi kisa TV unaonaje ushauri serikali wafunge tvstations zote ziwe on air wakirudi makazini
 
a great man will fly through the power of his mind not through the strength of muscles

This is practically possible in civilized societies where the conscience is alive and functional. But in barbaric societies like ours use of muscles is the only means to solutions. Keeping quiet and resting on the bench while pondering on how to go through then trying to push ur ideas verbally, in Africa is the sign of weakness.
Exchange of fists and throwing chairs to each other is the best way to make the rulers wake up early. Otherwise, we have to wait for two centuries ur theory to become workable.
 
Ukawa hamna kitu kabisa,hawana strategies kabisa,sasa naamini Dr. Slaa ndo alikuwa kila kitu CHADEMA

CCM ndiyo kuna kitu..??!! Nyie si kwamba mnatumia wingi wenu kupitisha mambo kwa maslahi ya chama?
 
Swali lako halina logic,unategemea wabunge wa CCM waende tofauti na serikali yao?katika hili suala la kutoonyesha bunge live?
Duh......
Kama swali langu halina logic hata lako halina maana huna nia ya kujua.

Mimi nikujibu tuu...
Kazi ya upinzani ni kukosoa serikali inapofanya vitu siyo pamoja na kushauri kwa manufaa ya wananchi! serikali ina wajibu wa kufuata ushauri au kutokufuata.
Mara nyingi serikali sikivu huwa inafanyia kazi ushauri wa upinzani maana mara nyingi huwa na maana sana lakini wonder enough serikali ya tanzania kwa kushirikiana na wabunge wake wanafanya juhudi za kudhorotesha juhudi za upinzani kuikosoa serikali! Hata wabunge wa chama tawala wanatakiwa kuikosoa na kuishauri serikali siyo UKAWA PEKEE YAO!

Kama jibu halijakuridhisha KOSOA PANAPO KOSELEKA!
 
Mimi sio UKAWA lakini ntawashangaa wabunge wa CCM wakikubali huu uamuzi, kwa nini wanafanya mambo kisiasa namna hii, maana hata Tv binafsi wamekatwazwa kurusha live isipokuwa kwa kupitia studio ya bunge. Tusikubali ubakaji huu..

Pole sana mkuu. Lakini hata siku moja usitegemee wabunge wa CCM kukutetea katika mambo ya msingi kama haya. Siku zote wanajificha kwenye mabawa ya chama chao. Na hiyo ndiyo tofauti ya CCM na vyama vya UKAWA.
 
Jamani wabunge wa ukawa, upinzani siyo kusema kwa Maneno tu. Hamuwaoni wabunge wenzenu wa Somalia, Kenya, Urusi na juzijuzi Brazil? Amkeni jamani.
Lakini pia na sisi wananchi tuwe wepesi kuwaunga mkono wabunge Wetu. Kama wanavyofanya wabrazil.
 
Mwisho hapo ndio umenena. Watanzania kila siku kulaumu tu wabunge , tunatetewa ila tunaotetewa tunawaacha watetezi wetu kuwa waajiriwa kwetu
 
Back
Top Bottom