Tatizo tuliruhusu Elimu kuwa Biashara, hilo ni kosa kubwa sana!

Kuna siku nikiwa nasoma nchio fulani miaka kadhaa ilopita katika kufanya assignment nikatoa mfano wa ku privatize fire services....kuanzia mwalimu hadi wanafunzi wengine walidhani nimetunga...
Ndio nikajua only in Tanzania...ambako kuna private fire services...
Mi nilikuwa nachukulia poa...wakaanza kufocus discussion yao kwenye topic yangu...
Waliuliza maswali magumu na kweli yalinifanya ni reflect na kuona hatari tuliyo nayo...

Waliniuliza nani anawalipa? nikasema mwenye janga...
Wakahoji, hawawezi kuwasha moto ili wapate biashara? (maana private sector wao cha kwanza ni profit)
Hawawezi kukataa kuzima moto sababu mwenye property hana hela? (na kweli baadae nikaja sikia stori sijui kama ni kweli walienda mahali wakawa wanataka hela kwanza hili wazime moto...

SI kila kitu ni cha kuendesha kibiashara...ndio nilichojifunza...serikali ilikosea sana kuachia hizi shule zijiendeshe zitakavyo...ila chimbuko ni conflict of interest...kuna waziri wa Elimu alikuwa mmiliki wa shule binafsi...

Na kipindi chake ndio shule za umma zilipoteza umaharufu (nasikia...maybe we need research on that)
 
Miaka ya Nyuma ilikuwa sifa kuchaguliwa shule za serikali,sijui mdudu gani kaingia hapa kati
 
mu
nchi zote duniani Elimu iko ya bure na ya gharama hiari yako uende wapi.
Lakini elimu ya gharama haikuruhusiwa kuua elimu ya bure...
Hivi shule za serikali zingekuwa za viwango kama enzi zile nani angekuwa anafanyia kazi hawa wanyonyaji...maana mshahara wote unaenda kwenye ada
 
Basi wakaguliwe na TRA na walipe kodi...
Siyo kujificha kwenye mgogo wa 'tunaisaidia serikali' kumbe watu wanapiga ma bilioni kwa mwaka
Shule binafsi wanasaidia Serikali tena sana chukulia mtoto wa shule binafsi ya msingi kafaulu kwenda shule ya sekondari ya kata hakwenda akaenda private kaisaidia Serikali kwani ile nafasi aliyoacha itajazwa na mtoto wa maskini ambaye asingekanyaga sekondari kama huyo aliyeenda private aNGEENDA SHULE YA KATA.. Shule za private zinaisaidia Serikali kusomesha watoto wengi zaidi Kwa kuipunguzia mzigo wa watoto ambao wasingekanyaga sekondari kama shule za private zisingekuwepo Kwa kawaida hizo shule zingetakiwa zidai ruzuku kwa Serikali kuwa tunakupunguzia mzigo ambao wewe Serikali ulitakiwa ubebe.kumsaidia mtoto wa maskini ni pamoja na kuruhusu shule za private ziwepo. Wakifunga maskini wengi watoto wao hawaji kanyaga sekondari
 
hakuna mtu anayelazimishwa kumepeleka mtoto wake huko kuna shule za serikali pia hata za binafsi zipo za mihula miwili badala ya kulalamika angalia unaweza mdu wapi.
 
Shule sasa hivi za serikali ziko nyingi wewe...sema ubora...
Nadhani kuna haja ya kuanzisha mkakati wa kitaifa wa kuinua ubora wa shule zetu za umma badala ya sisi middle class kuzikimbia...tunakimbia tatizo badala ya kuli face...

Hivi sie tunaopeleka watoto private schools tungekomaa na shule za kata zetu na kuwapa motisha walimu say kila mzazi mwenye uwezi ajitolee (voluntarily) kiasi kadhaa kumwongezea mwalimu kama motisha unadhani hizi shule zingefanya vibaya...

Mbona Mzumbe and the like bado wako vizuri...maana serikali ina best teachers (qualified) only that hawako motivated...
 
hakuna mtu anayelazimishwa kumepeleka mtoto wake huko kuna shule za serikali pia hata za binafsi zipo za mihula miwili badala ya kulalamika angalia unaweza mdu wapi.
Usilazimishe kwamba kila mteja wa hizi shule yuko happy kulipa ada za hizi shule...
Only that hatuna option...wewe... mbona sie ni zao la shule za serikali...nini kimefanya zionekane hazifai?
Lakini nikipinga usinambie eti mwanangu asome shule ya kata...usikimbie ukweli hata kama na wewe ni mmiliki
 
Elimu yetu haikugeuzwa biashara kwa bahati mbaya Bali ni mkakati wa makusudi wa IMF ndio maana tuna vyuo vingi feki ambavyo vinazalisha wasomi wasiokidhi viwango lakini ndio hao waliopewa nafasi kuongoza idara nyeti
 
Ukweli utabaki kuwa hizi Shule kutosimamiwa na serikali ni janga kubwa
Uwepo ushirikishwaji wa wazazi katika shule husika ili kupandisha hizo ada
Mfano kuna shule hapa magomeni iitwayo Hazina international wamepandisha ada 3.8m hadi 6m kwa wanafunzi wa darasa la saba
Shule hii ina lipi la ziada kupandisha hiyo ada kwa Kiwango hicho kwa kweli hawastahili kwa hili ni uonevu uliopindukia
Serikali irudi kuangalia hili
 
Jukwaani yalijitutumua turarejuleti baada ya mda kidogo na kupata kile walichokuwa wanataka , aaaa hatutajihusisha na kutoa uelekezi wa ada. Ha haaa kwanini msijue hilo kabla na kwamba hamna ubavu wa uthibiti wa mambo mengi tu nchini? Maana ninyi na wao ni wale wale yaani mafisadi.
Mtoto aliyepo shuleni kwa huu mwaka magufuli aliokuwa madarakani wameongeza laki tano juu ya ile iliyokuwepo.
Halafu kwa jeuri wanakuambia kama vipi iambie serikali ya kizalendo imtolee ruzuku.
 
Kuna mtu kakulazimisha kulipa hizo ada kubwa....high sasa hivi maana ujinga sitaki
 
Hapa naongelea Elimu, tena ya Msingi na Sekondari hakuna nchi iliyoendela ambayo Elimu ni Biashara kama hapa kwetu, na sababu ni kwamba Elimu ni Huduma kwa jamii!
Ndugu yangu biashara nyingi zinazofanyika hapa nchini ni huduma za kijamii ikiwemo vyakula, fikiria maduka yote yangefungwa unadhan maisha yangeenda? Kimsingi wafanyabiashara wanafanya biashara at the same time wanatoa huduma za kijamii. Ukitazama elimu inayotolewa shule binafs na hata ukiangalia ufaulu utaona kabisa tofauti na shule za umma,kitu cha msingi ni turud ktk misingi itakayoboresha shule za umma hawa private watafunga tu mashule yao endapo shule zetu za umma zitaboreshwa kuanzia miundombinu hadi walimu. Tusipofanya hvyo hatuna haja ya kulalamika shule binafs wanna ada kubwa.
 
Kwahiyo unapingana na sera ya elimu bure?
 

..matokeo ya mitihani ya kitaifa yanaonyesha kwamba vijana wetu hawajifunzi.

..kama utakumbuka miaka miwili iliyopita matokeo yalikuwa mabaya kiasi cha kulazimisha serikali kuingilia na "kufanya-fanya" ili ionekane watahiniwa wamefaulu.

..hali ni mbaya kiasi kwamba kuna mwanafunzi aliripoti kidato cha kwanza akiwa hajui kusoma na kuandika vizuri.

..sipingi kwamba kuna UTAPELI ktk baadhi ya shule za watu binafsi. Hilo wala halina ubishi.

..Lakini ni imani yangu kwamba elimu yetu ina matatizo mengine makubwa zaidi ya yale ambayo mtoa mada ameyajengea hoja.
 
Ukitaka kuendelea, ni sahihi kutaja udhaifu wako badala ya kutaja ubora wako. Suala la elimu linahitaji uangalifu. Tunashabikia shule za binafsi kwa family-level assessment. Mtu akiona mtoto wake anafaulu anajua elimu huko iko safi. Hebu tuulizane kwa ufahamu wetu wa Dunia hii, je, kuna nchi yoyote ile duniani ambayo elimu yake iliinuka kwa kutumia private schools? jibu ni HAKUNA! Elimu ni kitu cha kusimamiwa na serikali, FINITO! Nje ya serikali, ilikuwa enzi hizo za dini/kanisa kusimamia elimu.

Kama wewe ni msomaji kama mimi, UK ya Tony Blair ilikuwa na kilio cha elimu sana, lakini Britons hawakuona kama Blair alikuwa mtu sahihi wa kurekebisha elimu yao. Sababu, alisoma private! Hata uchaguzi wake kuwa PM ulileta shida wakiwa hawaamini uwezo wake kwa kusoma private schools! Sisi hapa tunadhani kuna watu wanaijua elimu huko private kuliko serikali kweli?

Utapeli shule za binafsi umejaa! Takriban zote. Shule za madhehebu zilikuwa nje ya upuuzi huo lakini nazo sasa zimeingia.

btw. Elimu siyo mtihani tuu! Ndo maana kila mwanafunzi bora wa mwaka kwa form 4, akienda form 6 mara nyingi huwa hatumsikii tena.
 
Mkuu unaishi kwenye Dunia ya Kijamaa kwa nadhalia huku ukiwa kwenye Dunia ya Kibepari kiuhalisia...Capitalism
 
Huu upuuzi mnaofanya na shule za binafsi madhara yake mtayaona.
Mnadhani mnawakomoa wakati shule za serikali hata madawati tu, na matundu ya vyoo ni changamoto.
Acheni huu upuuzi, mtaiangamiza jamii.
 
Acha tu nusu saa iliyopita nimetoka kulipa ada ya primary watoto wawili kila mmoja 1.2m×2 maana ukisema utegemee za bure kizazi kitafia utumwani...
Sidhani km kuna mtu analazimishwa kupeleka watoto hulo mnakodai elimu ni biashara. Kingine ktk hizo shule mnazopeleka watoto mmefanya tafit mkagundua ni bora kuliko hizi za bure? Wengi mnapeleka ili watoto wajue kingereza tu na mnadhani kingereza ndio ujuzi. Kitafiti watoto wa shule za bure wanauwezo mkubwa(ujuzi) kuliko za magari ya njano
 
Naomba web site ya city of London corporation ili nipeleke pendekezo Na miji yetu iwe Kama London
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…