Tatizo la kuhara damu

Tajirimsomi

JF-Expert Member
Jan 12, 2017
4,824
5,580
Naombeni ushauri wataalamu wa afya. Nilikunywa maji ya mvua zimepita kama siku nne nimeanza naharisha tangu siku hiyo, sikwenda hospital maana nilifikiri ni mchafuko wa kawaida sasa kuanzia leo asubuhi nahara damu mfululizo.

Naombeni ushauri nichukue hatua gani na tatizo laweza kuwa ni nini nipo hospital ila ila mi ni mvivu wa kumeza madawa.
 
Nenda hospital mara moja. La sivyo ukanunue Ciprofloxacin 500 mg mara mbili kutwa kwa siku tano mpaka saba
 
Kuhara damu kwa kitaalamu tunaita 'dysentery' na hii inaweza kusababishwa na mambo mbalimbali aidha mchubuko kwenye mfumo wa chakula (gastrointestinal injury) au Inaweza kusababishwa na vidonda vya tumbo au aboeba, hivyo unahitaji uchunguzi wa haraka.

Swala lakuharisha damu sio la simile wala la kununua dawa madukani bila kujua tatizo.

Wahi hospitali
 
Kwa maelezo yako tu haya wewe utakua ni CO, hongera kwa kumpa msaada sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…