Tathmini: Kuzuia shughuli za kisiasa mpaka 2020 haiwezekani

Jpm alikula kiapo kwa katiba ipi?msajili wa vyama vya siasa anatakiwa akutane na rais amwambie,sasa msajili anaongelea chumban hii itasababisha madhara makubwa huko mbele,ukizingatia wananchi wameanza kumchoka Jpm.
 
Dunia ya Leo yenye social media like Facebook, WhatsApp, Jamii forum, magazeti kibao, redio kibao siyo lzm uandamane au kufanya mkutano ndio ufikishe ujumbe kwa jamii.

Unaweza kuongea kwenye redio tu kila MTU akasikia ujumbe wako.

UKAWA kuweni wabunifu
 
JPM anaminya demokrasia anachotaka ni kusifiwa tu. Kweli atasifiwa kwa mema na busara lakini akiboronga lazima aambiwe tu, mzee (baba j) hapa umekunya
Cha kushangaza zaidi ni kuwa wafuasi wengi wa CCM wamekuwa wakitamba kuwa kwa utendaji kazi wa Magufuli, wapinzani watakosa hoja za kuwaeleza wananchi na hivyo kuifanya CCM iwe na mteremko mkubwa kwenye chaguzi zijazo.

Sasa swali jepesi la kuwauliza hao makada na wafuasi wa CCM, kama utendaji kazi wa Magu umewarahisisishia mno kuishinda kwenye chaguzi zijazo kwa kuwa wapinzani watakuwa hawana hoja.

Sasa ni kwa nini Bosi wao huyo ameingiwa na hofu kiasi cha kufanya mambo yafuatayo.

1. Kuzuia mikutano yote ya kisiasa ya vyama vya upinzani ikiwemo hata ile mikutano ya ndani, hadi Kuzuia Mahafali ya wanachuo, kama walivyofanya Dodoma, Moshi na Morogoro?

2.Kama CCM wanajiamini kupita kiasi ni kitu gani kilichowatia hofu hadi Kuzuia Bunge ambalo ni chombo cha uwakilishi wa wananchi kisirushwe LIVE kama yalivyo matakwa ya wananchi zaidi ya asilimia 90 ambao wanataka Bunge lirushwe LIVE?

3.NI kwa nini serikali ya CCM wamekuwa na woga wa kupitiliza hadi nyakati nyingine Kuzuia wafuasi wa vyama vya upinzani kuwazika wapendwa wao?

Mfano halisi wa hiyo hoja namba 3, ambapo wafuasi wa Chadema walizuiliwa na Polisi kumzika mpendwa wao Mawazo hadi pale chombo cha mahakama kilipotoa hukumu na kueleza kuwa wafuasi hao wa Chadema wana haki ya kumfanyia mazishi yanayomstahili kiongozi wao.

Kutokana na hofu kubwa mno waliyonayo CCM ya kuviogopa vyama vya upinzani, kunazua maswali mengi yanayokosa majibu na swali kubwa, je ni kweli kwenye uchaguzi mkuu wa October 25 mwaka jana walishinda bila goli la mkono?
 
Back
Top Bottom