Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,917
Ukweli ni kwamba, hawa Bwana wakubwa wamefanikiwa sana katika kupandikiza hofu na uoga katika jamii yetu na hata katika vyombo vyetu vya habari lakini wamefeli sana katika azima yao ya kutaka umma usipate habari wanazotaka zisifike kwa umma.
Kwanini nasema hivi?
Kuna mambo/matukio ambayo yakitokea, vyombo vyetu vya habari havithubutu kuandika, kuhoji wa kujadili kwa hofu ya kushughulikiwa lakini mwisho wa siku wao wenyewe wanachukua nafasi ya media kutangaza jambo husika kupitia media hizo hizo wanazozidhibiti
Kwa namna gani hali hii inatotokea?
Panapotokea jambo kubwa na zito ambalo wao hawataki wananchi walijue, watu kupitia mitandao ya kijamii, huanza kuliibua na kulijadili jambo husika usiku na mchana kiasi kwamba huwalazimu wao kama wenye mamlaka kujitokeza kulitolea ufafanuzi jambo husika.
Nini hutokea baada ya hapo?
Kitendo cha wao kujitokeza hadharani na kujibu au kutolea ufafanuzi jambo husika,hutoa nafasi kwa vyombo vya habari kuripoti jambo husika kwa umma na hivyo kuibua mijada zaidi.
Kwahiyo, kinachotokea au kinachofuata baada ya hapo, hua ni kufungua mijadala kuhusu jambo hilo katika vyombo vya habari , na matokeo yake ni kuwafanya hata wale wanaoishi gizani kujua nini kinaendelea na hapo kunakuwa hakuna tena siri/kuficha habari kwa umma.
Kwahiyo, katika hili, utagundua work done ni zero or almost equal to zero.
Wanaangamia kwa kukosa maarifa!