Tanzania yatupilIa mbali madai ya Kenya kuhusu Amina Mohammed, yasema ilimuunga mkono kugombea AU

Na imeandikwa wapi kwamba lazima tumuunge mkono?

Tanzania ilimsaidia lakini kura hazikutosha. Akubali yaishe asonge mbele. Aendelee na uwaziri wake!
 
65e106ceea82987fa19e606de6514376.jpg
Tanzania imepuuzilia mbali madai kwamba baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki hayakumpigia kura mgombea Amina Mohammed wa Kenya katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muungano wa Afrika

Amina ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, alishindwa na mwenzake wa Chad Moussa Faki Mahamat, ambaye sasa ni Mwenyekiti wa AU

Akizungumza na BBC jijini Addis Ababa, Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Augustine Mahiga, amesema madai katika baadhi ya vyombo vya habari nchini Kenya kuhusu uchaguzi huo ni ya kupotosha, bali ilimuunga mkono mgombea wake wa AU

Mahiga alizungumza na mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza ambaye alianza kwa kumuuliza kuhusu shutuma hizo wakati wa uchaguzi wa viongozi wa AU.
Mambo mengine ni aibu tupu katika ulimwengu wa sasa
 
Si sahihi kwa Kenya kumlaumu yeyote kwa waziri wake kushindwa; ijilaumu yenyewe.

Ilikuwa ni kichekesho kwa Kenya kutarajia kushinda uchanguzi huo bila kuhakikisha kwanza inaungwa mkono kikamilifu na nchi za mashariki na kusini mwa Afrika hasa kwa kuzingatia mgawanyiko uliopo AU kati ya nchi zinazozungumza Kiingereza na zile zinazozungumza Kifaransa. (Karibu nchi zote za kanda za mashariki na kusini mwa Afrika zinazungumza Kiingereza).

Kihistoria, Kenya imekuwa na sera za uhusiano wa kimataifa zinayolenga katika kujiangalia yenyewe (inward looking). Na ndio maana Kenya haikuunga mkono wala kusaidia harakati za ukombozi kusini mwa Afrika; na pia haikipiga kelele kupinga sera za ubaguzi wa rangi Afrika Kusini. Hiki ni kigezo muhimu kwa nchi kuwa na ushawishi hasa kusini mwa Afrika. Hivyo si ajabu kwamba, pamoja na ukweli kuwa Kenya ina uchumi mkubwa, ushawishi wake katika siasa za hii kanda ya Afrika ni mdogo sana.

Somo muhimu kwa Kenya ni kwamba kushinda nafasi kama hiyo ya uwenyekiti wa sekretariati ya AU hakuhitaji tu kufanya loobing bali kunahitaji uwekezaji wa muda mrefu katika mahusiano ya kikanda.
 
Wana jamii
Salaam

Tanzania imepuuzilia mbali madai kwamba baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki hayakumpigia kura mgombea Amina Mohammed wa Kenya katika uchaguzi wa mwenyekiti wa Muungano wa Afrika.

Amina ambaye ni waziri wa mambo ya nje wa Kenya, alishindwa na mwezake wa Chad Moussa Faki Mahamat, ambaye sasa ni mwenyekiti wa AU.

Akizungumza na BBC jijini Addis Ababa, Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Augustine Mahiga, amesema madai katika baadhi ya vyombo vya habari nchini Kenya kuhusu uchaguzi huo ni ya kupotosha.

Mahiga alizungumza na mwandishi wetu Emmanuel Igunza ambaye alianza kwa kumuuliza kuhusu shutuma hizo wakati wa uchaguzi wa viongozi wa AU.

Chanzo: BBC Swahili
 
Nchi za kiafrika ni wanafiki ndio maana hata huu umoja wao ni wa mashaka, hakuna nchi inapenda kiongozi wa nchi moja awe kwenye anga za kimataifa wanapenda kushindana kwa mambo ya kipuuzi tu, wenyewe kwa wenyewe hawaaminiani, ki offer kidogo tu kutoka nchi za magharibi tunapigana vikumbo kuumizana ili nani apte nani asipate.
 
Kwani, mbona mimi sielewi? Tulienda kupigia kura kanda zetu au tulienda kuchagua Mwenyekiti wa Kuiongoza AU kwa mafanikio?

Unafiki jambo baya sana. Hata mimi sioni tija kwa East African kushika usukani kwani tunaendekeza sana unafiki. Mambo ya kina Nkurunzinza yanaundiwa tume mwenyekiti Museven, tuna haja kweli ya kupewa uongozi?
Teh teh teh teh teh teh, hapo mwizi ni teja hakimu muuza unga, askari pusher. Dhahiri bloc ya east africa inamajambazi wengi, nkurunzinza, museveni ,kagame ,salva kiir. Hawa wawili waliobakia they are one milimeter from the redline
 
Wana jamvi

Salaam

_93900799_amina-mohamed.jpg


Waziri wa maswala ya nchi za kigeni Kenya Amina Mohammed
Mgombea wa wadhfa wa mwenyekiti kutoka Kenya katika tume ya Umoja wa Afrika AU Amina Mohammed ametaja usaliti miongoni mwa mataifa jirani ya Afrika Mashariki kuwa sababu ya yeye kutoshinda wadhfa huo.

Balozi Amina ambaye alipoteza wadhfa huo kwa mpinzani wake kutoka Chad Moussa Faki Mahamat alilaumu kushindwa kwake kulitokana na uwongo wa majirani za Kenya na siasa zinazoendelea kati ya mataifa yanayozungumza Kifaransa Francophone na wale wanaozungumza kizungu Anglophone.

Akiongea na vyombo vya habari vya kimataifa mjini Addis Ababa Amina alisema kuwa alipoteza wadhfa huo kutokana na usaliti wa majirani za Kenya ambao walikuwa wameunga mkono harakati zake.

_93900796_eala.jpg
Bendera za mataifa ya Afrika
mashariki

''Baadhi ya majirani zetu hawakutuunga mkono, walisikika wakizungumzia swala hilo'', Amina alisema bila ya kutaja majina. Nadhani hofu kwamba pengine Kenya ingeshinda ndio iliowafanya kutotuunga mkono''.

''Nadhani sisi Wakenya ni watu waaminifu sana kwa hivyo ni vigumu kushirikiana na watu wanaohadaa.kwa hivyo nadhani walijiondoa''.

Tukisonga mbele ni funzo zuri kwetu sisi. Katika raundi ya tano ya kura hizo Amina alikuwa anaongoza kwa kura 27 dhidi ya za Mahmat 25'',aliongezea Amina Taifa moja halikupiga kura.

Ni wakati huo ambapo mataifa mawili kutoka shirika la IGAD yaliamua kumpigia kura mpinzani wa Amina na hivyo basi kumpatia kura 28 zaidi ya 26 zilizohitajika ili mgombea kuibuka mshindi.

Chanzo: BBC
 
Kenya waache kulia lia. They need to up their diplomacy. In Africa (just like anywhere else) diplomacy is simply mafia like game. Hata Kenya wenyewe hawaaminiki. Again, kila nchi inaangalia maslahi yake. Sasa kama Tanzania our interests were best served with Chad, then so be it. But I believe we voted for her. Uganda na Burundi ndo walimtosa!
 
Msimamo wa Tanzania ulikuwa very clear from the beginning kuhusu hilo. Hope ujumbe wa Tanzania haukuyumba kimsimamo kama anavyodai Balozi Amina baadhi ya nchi kuyumba kimsimamo.
 
Msimamo wa Tanzania ulikuwa very clear from the beginning kuhusu hilo. Hope ujumbe wa Tanzania haukuyumba kimsimamo kama anavyodai Balozi Amina baadhi ya nchi kuyumba kimsimamo.

Mkuu kwani msimamo wa Tanzania ulikuwa upi?

Wengine hatukufuatilia hili suala.
 
Wao ndio walianza.Tanzania tulipotaka kuuza shehena ya meno ya tembo wao walisimama kidete kuona zoezi hilo halifanikiwi.Sasa hivi serikali ya Tanzania inatumia fedha nyingi kutunza shehena hiyo.Mwenzako akimwaga ugali wewe mwaga mboga ,sasa tutaheshimiana.
 
Back
Top Bottom