Tanzania ndio iliyosaidia mpaka Vietnam kuendelea, sasa wametupita

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Kwa upande wa kilimo, Vietnam ni ya kwanza kwa kuuza kahawa aina ya robusta na korosho duniani.Mbegu za mazao hayo walizichukua Tanzania kwenda kuanzisha kilimo hicho.

Aidha, Vietnam ni maarufu duniani kwa kuuza samaki aina ya sato ambao walichukuliwa kutoka Ziwa Victoria na kwenda kuanza ufugaji wake kule

Sasa hivi wametupita mbali mno kwenye kilimo na ufugaji wakati miaka 50 iliyopita walikuwa maskini kama sisi.

SOURCE:Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania

Watu waliokaa serikalini muda mrefu kama akina Kingunge,Lowasa,Sumaye na Pius Msekwa na wengineo inabidi watupe maelezo ya kueleweka kwa nini tuko hali mbaya kama nchi.

yehodaya123@gmail.com
 
Huwa kiukweli huna akili. Kumbe unajua kuwa nchi imevurunda kwa miaka hamsini iliyopita? Ila wewe badala ya kuhoji Sera za chama kilichoshika madaraka kwa nini zimeshindwa una hoji watu? Tena unahoji wale waliozikimbia Sera hizo mbovu na kusema haziwezi kuleta mabadiliko?
Kweli ccm ina hazina kubwa ya wajinga wanaodhani wana akili. Hongera kwa kipaji hicho, ujinga nacho kipaji
 
Yes we demand maelezo ya kina vipi nchi iliyokuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe zaidi ya miaka ishirini imetupiku kiuchumi Tanzania iliojaliwa rasilimali na amani zaidi ya miaka hamsini. CCM jipu.
 
Hata mimi nabaki na maswali ni wapi tumejikwaa, kwani kama ni vita wao ndo wamepigana muda mrefu. Mimi nadhani kuanzia utawala wa awamu ya pili tulikosea kuset uchumi wetu.
 
Kuna wakati waziri mkuu aliyepita akiitwa M.Pinda alikiri kuwa kuna mapungufu makubwa katika serikali hasa mfumo wa serikali,hapo alikuwa katika joto la kuwajibishwa na wakina Zitto.Lakini aliondoka bila ya kutaka kuifanyia kazi hiyo changamoto.Kwa jinsi ilivyo,tuna mapungufu makubwa sana katika mifumo yetu ya kiuongozi,utendaji na mifumo ya kiutawala.Hatuna utaratibu wa kuwapata viongozi walio bora,wenye uwezo na makini.Kuna Katiba na sheria nyingi zimepitwa na wakati au kuna loophole katika Katiba na Sheria ambazo zinawapa wanasiasa na watendaji waandamizi wa serikali ku-bypass na hakuna cha kuwafanya.Tusishughulike na watu,bali kusuka mifumo,sheria na katiba bora kabisa then tuone kama kuna upuuzi utakaojitokeza.Hakuna vipaumbele,sijui katika baraza hili,kila mmoja akigumgiwa peke kwa wakati mmoja akiulizwa vipaumbele vya serikali na namna ya kuvitekeleza,sijui kama wote watakuja na majibu yaliyosawa.

Mifumo,katiba na sheria zilizosukwa vyema vinatuchelewesha sana maana vyote hivyo hatuna.
 

Ninaposema CCM imeifilisi nchi hii na kuifanya nchi hii maskini mnabisha....CCM is responsible for all corrupt issues in this country

Bila Kuwasahau Kikwete,Mkapa,Mwinyi,Warioba ,Magufuli na Kinana

Hasa hawa niliowataja kwa sababu wao ndio walezi wakuu wa MAJIPU
 

Tatizo kaka unakumbuka shuka kumekucha.Mara nyingi wapinzani wakihoji unakuja juu kama moto wa kifuu leo imekuwaje umeliona hilo???

Kama Taifa tunatakiwa kuwahoji viongozi wetu,tusiende kama mataahira.Kuna vitu vinafanyika vinatakiwa vihojiwe.Mfano sioni sababu ya kumfukuza kazi Dakatri kisa ameomba utoe pesa kidogo akanunue vifaa.Nilitegemea Waziri atafight hospitali zipate dawa na vitendea kazi.Halafu tunakaa tunapiga makofi hatuhoji.
 
kivipi fafanua

CCM kama chama tawala imekuwa ikikusanya kodi kupitia serikali yake na imepewa jukumu la kuzitumia hizo kodi za wananchi ili wananchi kujiletea maendeleo.

Badala yake CCM kama chama kimeshiriki moja kwa moja katika kuzitumia vibaya kodi hizo za wananchi na hivyo kufanya sekta zote za maendeleo mfano kilimo kudumaaa

Pia CCM kupitia serikali yake Imelea vitendo vya ubadhirifu na wivi wa mali ya umma ,vitendo vilivyofanywa na maafisa wake na kusimamiwa na wakuu wa serikali ambao pia ni viongozi wa chama cha CCM.

CCM haijawahi kuchukua hatua thabiti za kuwawajibisha wahusika waliohusika na wizi huo mkubwa wa kodi za wananchi...Badala yake imekuwa ikiwalea.

CCM imeshiriki kuhodhi mali za Umma kama vile viwanja vya mpira na maeneo ya wazi ambavyo vilipaswa kumilikiwa na serikali

CCM kama chama kimeshiriki moja kwa moja katika Ufisadi wa MEREMETA,KAGODA na ESCROW
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…