Tanzania na kizazi cha wasomi wezi na wavivu!

Hilini tatizo. Linahitaji mjadala wa kitaifa.........ni la kimaadili...........litahusisha pia kuhuisha mitaala iwe na elimu ya kujitegemea
 
Halikadhalika Watz wanapenda AJIRA ila sio KAZI.

Ni kweli wengi hupenda Ajila tu Kwa Nia ya kujinufaisha binafsi si kufanya kazi ili kampuni ikue , Vijana wengi wanapenda kujionyesha hasa wale wapenda starehe na michepuko , lipo kundi jingine jipya limeibuka miaka ya karibuni hili kundi ni la Vijana wapenda wake za watu na Wanawake wenye pesa Kwa lengo la kujipatia pesa kiharamu , Vijana wa Tanzania ni shiiiida .
 
Hili limekuwa tatizo kubwa sana katika vijana sisi,wengi hatutaki kabisa kazi zozote za nguvu au za kujituma,wao wanataka na wanafikiria tu kupiga dili,ndio maana utaona kila kijana anataka kuwa mbongo fleva au bongo movie tu,pesa hawana mitaani vurugu tupu,tunalalamika sana wageni kuchukua ajira zetu,lakini tunasahaukuwa sisi sio watu wakazi ila wapoiga dili tu,mtu akipata kazi hakuna anachowaza zaidi ya kupiga dili kuibia kampuni tu,
bila kubadilika hata seriakli iliyoamua kututetea sasa itachoka na itagundua wenye makampuni wako sahihi
 
Hilini tatizo. Linahitaji mjadala wa kitaifa.........ni la kimaadili...........litahusisha pia kuhuisha mitaala iwe na elimu ya kujitegemea

Ni kweli mkuu , ukichunguza Elimu ya Tanzania Kwa kweli haiendani na soko la Ajila ndiyo maana wengi huwa na vyeti vizuri lakini kichwani hawana Taaluma kutokana na kusoma kijanja janja Kwa kukariri , kuiba mitihani , kununua majibu, Rushwa ya ngono nk, Vijana wengi ni wasomi Feki ikitokea waambiwe wote warudie mitihani iliyowapatia vyeti Dunia itashuhudia maajabu maana wengi watafeli vibaya kutokana na kutokuwa na Taaluma harisi bali hufanya kazi kijanja janja huku wengi hutumia fursa pindi wakiajiriwa wakawakuta wageni wanaojua kazi hujifunzia kupitia kwao kijanja faster baada ya kujua kazi ndipo mbinu za kuifirisi kampuni huanza hili ni Janga la kitaifa
Magufuli Hana budi awaige Uganda apige marufuku Uvaaji wa hovyo hovyo milegezo vimin na Ujinga Ujinga wote maadili yarejeshwe haraka, kinyume na hapo Maendeleo tutayasikia kwenye bomba tu.
 
Hili limekuwa tatizo kubwa sana katika vijana sisi,wengi hatutaki kabisa kazi zozote za nguvu au za kujituma,wao wanataka na wanafikiria tu kupiga dili,ndio maana utaona kila kijana anataka kuwa mbongo fleva au bongo movie tu,pesa hawana mitaani vurugu tupu,tunalalamika sana wageni kuchukua ajira zetu,lakini tunasahaukuwa sisi sio watu wakazi ila wapoiga dili tu,mtu akipata kazi hakuna anachowaza zaidi ya kupiga dili kuibia kampuni tu,
bila kubadilika hata seriakli iliyoamua kututetea sasa itachoka na itagundua wenye makampuni wako sahihi

Hata wakipata pesa kazi Yao ni kukaa bar na vijiweni kupiga majungu kujadili watu badala ya maendeleo Vijana siku hizi wamekuwa wambea balaa kila mtu wanamjua hawataki kufanya kazi kampuni zikue wao wanawaza matumbo Yao na starehe zao pekee .
 
Nina andika hii mada nikijuwa kabisa itaenda kugusa watu wengi na hasa ukizingatia jamiiforum inawasomi wengi. Ila ni bora tukalitumbuwa hili jibu ili vijana tukakumbuka tulipotoka na kule tutalipeleka hili taifa. Siku za hivi karibuni baada ya bwana mkubwa kuchukua nchi yameibuka mambo mengi ambayo yanatia mashaka makubwa ya nguvu kazi ambayo ndio gurudumu la maendeleo.
Vijana wa Tanzania kwakweli tunatia aibu nakuzuwa maswali magumu yasio kuwa na majibu ikiwa tunadhamira ya dhati kulipeleka taifa hili mahali fulani au tunawaza matumbo yetu tu.
Kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wanao ajiriwa ktk serikal na secta binafsi lakini pasipokujali thamani ya kazi na muda wa wao vijana wengi tumekuwa kero kwa waajiri even if utamlipa vizuri kias gani. Vijana wamekuwa wezi na walio kosa uwaminifu kwa waajiri wao jambo limefanya makampuni mengi kuajiri watu toka nje ilikupunguza hasara wanapata. Wakati serikal inapambana na waajiri wasilete watu wao kufanya kaz ndani ya taifa letu, waajiri wanapeleka ushaidi wa upotevu wa mamilion uliosababishwa na watu wao. Hili swala linatishia ajira za maelfu ya wazawa na mwisho wa siku wa tz tutakuwa makarani mwanzo mwisho, just b'coz tupo majizi.
Uvivu na uzembe hili ndio balaa tupu mtu anakuja muda anataka kazin, maudhuru yakutosha, kaz hafanyi mambo kibao yamelundikana alimradi siku iende. Mbaya zaid haya mavivu ndio malalamish mshahara hautosh na mbwembwe kibao, sim wasapp from asubuh jion.
Jamani vijana tubadilike au tusubirie kuwa makarani wakati wakenya na waganda wakija kuchukua nafasi zetu. Taifa hili linatutegemea ila sio kwakuwa wavivu na wategevu wakazi. Tafakarini 2016 itakuwa chungu kwa mijitu mizembe na mivivu.

Lakini pia ni wanafiki, wana majungu na ndumila kuwili

hawafikirii, hawana uwanja mpana wa kuwaza na kutatua matatizo yao.

Ndio maana wanaigana hata kununua magari kila mtu ni prado rav4 na harrier....hii ni indicator ya jamii iliyodumaa kiakili siyowaza nje ya yale maisha ya kuzoeleka

wasomi wengi sio trouble shooter, they can only connect a power cable na internet cable, but they can not see hidden things, they can not see 5 years from now, they dont have confidence

Infact wasiosoma Tanzania kama akina Diamond na ali kiba, akina wema sepetu are likely to be more creative and independent thinker kuliko a normal graduate wa UDSM

TATIZO

Mfumo wetu wa ualimu, aina ya ufundishaji na mindset za watanzania za kutoka ukoloni ndio zimetufikisha hapa
 
Mtu ukimiliki kampuni ndio utayaona haya.

Huitaji kuambiwa na wakiambiwa wanakuwa wakali.

Ila ukweli ni kwamba vijana wa Tanzania sasa hivi competency ni ziro.

Muda wote wapo whatsap, kuwaza kuchat, ngono na ujinga.

Ukiwapa kazi wanawaza kuiba tu.

Kila siku excuses, mara nimefiwa yani ujinga mtupu.

Tuna miliki makampuni tunayaona

bora umuajiri form 4 leaver ukampa seminar atadumu na wewe na atafuata maelekezo kuliko graduates wetu wengi ambazo wana akili za ki CCM na ki UKAWA hata kwa vitu visivyohitaji siasa
 
Mimi huwa najiuliza, hawa kweli ni wasomi au, maana unakuta kijani ana degree lakini kupambanua kitu kidogo tu, anashindwa duuu.
 
Inatakiwa utaratibu wakulipa watu kutokana na performance ulipwe kutokana na faida wanayoiingizia campuni, hapo watu watafanya kazi kwa bidii
 
Mtoto akuavyo umleavyo. Ccm imeleta yote haya na ndo maana urais uliona vituko na ccm ilijenga mazingira ya vijana kutafuta pesa kwanjia haramu ni sahihi.
Haya yote ni mfumo ccm na hao vijana ni matunda yake. Kutwa baba yao alikua anashinda nje kuzurula wategemea watoto watakuaje?
Elimu yote imevurugwa kiasi kwamba wanatoka vyuoni namaarifa kiduchu wategemea nini? Vija starehe nyingi kama alivyo kua mkuu wa kaya wao. Kwahio JPM anakazi kweli yakua nyosha.

Wapo mpaka leo wabunge na mawaziri ambao wanakesha bar na disco huku wakiwa na wapambe wao Vijana ni kweli mtoto umleavyo ndivyo akuavyo sasa imewadia mda wa Magufuli kurejesha maadili ya viongozi ndani ya kazi na nje ya kazi huku Vijana wote wakipigwa misasa kila kona uwajibikaji urejeshwe Kwa kasi , tumwige Mseveni wa Uganda kupiga marufuku Ujinga Ujinga Uvaaji wa hovyo hovyo ( milegezo) Kisha tuje na mikakati wa kuhakikisha watu wanasoma kweli wapate Taaluma vichwani si kuiba mitihani wala kukariri na kujipatia vyeti kijanja janja tu matokeo yake tumefuga Utitiri wa Vijana wezi wapiga dili .
 
Products Za Udsm Ndo Weziwezi

Tafadhal sana bro! Hapa ni vijana na sio product. Unauhakika kuwa huko kwenye vyuo vingine sio wez. Wangap tuko nao maofisisn kaz hawafanyi wanawaza tu kupiga hela . Mtu akija ata kama anashida ww huwaz hilo unawaza ujazilizie hela ya kwenda kuhonga baadaye. Pole kama ww ni kijana na unawaz Vitu ambavyo havipo . HILI NI JIPU LA VIJANA WOTE WA TANZANIA BILA KUJALI CHUO WALA SEHEMU ANAKOTOKEA.
 
Mimi huwa najiuliza, hawa kweli ni wasomi au, maana unakuta kijani ana degree lakini kupambanua kitu kidogo tu, anashindwa duuu.

Wengi huwa ni wasomi Feki husoma Kwa kukariri tu ili afaulu apate cheti wengine huiba mitihani au kununua majibu na Rushwa ya ngono, ikitokea Magufuli aseme kila kijana arudie mitihani upya utashangaa kitachotokea lazima baraza la mitihani watazimia wote .
 
Tafadhal sana bro! Hapa ni vijana na sio product. Unauhakika kuwa huko kwenye vyuo vingine sio wez. Wangap tuko nao maofisisn kaz hawafanyi wanawaza tu kupiga hela . Mtu akija ata kama anashida ww huwaz hilo unawaza ujazilizie hela ya kwenda kuhonga baadaye. Pole kama ww ni kijana na unawaz Vitu ambavyo havipo . HILI NI JIPU LA VIJANA WOTE WA TANZANIA BILA KUJALI CHUO WALA SEHEMU ANAKOTOKEA.

Ni kweli majipu yapo kila vyuo kote Nchini majipu yamejaa tele.
 
Elimu ya vitendo huwa inaeleweka sana kuliko elimu ya nadharia. Vijana wanajifunza wizi toka kwa viongozi wao.Wazee wetu wezi mno wanafundisha nn vijana sasa?
 
Lakini pia ni wanafiki, wana majungu na ndumila kuwili

hawafikirii, hawana uwanja mpana wa kuwaza na kutatua matatizo yao.

Ndio maana wanaigana hata kununua magari kila mtu ni prado rav4 na harrier....hii ni indicator ya jamii iliyodumaa kiakili siyowaza nje ya yale maisha ya kuzoeleka

wasomi wengi sio trouble shooter, they can only connect a power cable na internet cable, but they can not see hidden things, they can not see 5 years from now, they dont have confidence

Infact wasiosoma Tanzania kama akina Diamond na ali kiba, akina wema sepetu are likely to be more creative and independent thinker kuliko a normal graduate wa UDSM

TATIZO

Mfumo wetu wa ualimu, aina ya ufundishaji na mindset za watanzania za kutoka ukoloni ndio zimetufikisha hapa

Zamani watu walizoea Wanawake ndiyo wambea sana lakini siku hizi Vijana wamekuwa wambea balaa mda mwingi ni kukaa bar kujadili watu majungu Kwa wale viongozi wachapa kazi wanabuni mbinu za kuwakwamisha na kuiba pasipo kujulikana , karne hii ya kazi eti bado Vijana wanakaa vijiweni kujadili watu ! Sidhani Kama Taifa litapiga Hatua endapo Magufuli ataendelea kukumbatia Mfumo dili kwanza kazi baadae.
 
Hii kitu ina uhalisia mfano kila kwenye duja.mtaani basi asubuhi au jioni linageuka kijiwe cha vijana wa kiume, wakike kila saloon aua stationary inageuja kijiwe au duka linalouza pombe utakuta kijiwe. Tafsiri ya watu kukaa kijiwe ni umbeya na unafiki na kuzungumzia habari za watu. Nchi kama finland mazingira tuu yanakufanya unaacha kuwa muongo na mzushi. Lakini sio Tanzania jamani mtu anadanganya hata kama hanufaiki na huo uongo.
 
Lakini pia ni wanafiki, wana majungu na ndumila kuwili

hawafikirii, hawana uwanja mpana wa kuwaza na kutatua matatizo yao.

Ndio maana wanaigana hata kununua magari kila mtu ni prado rav4 na harrier....hii ni indicator ya jamii iliyodumaa kiakili siyowaza nje ya yale maisha ya kuzoeleka

wasomi wengi sio trouble shooter, they can only connect a power cable na internet cable, but they can not see hidden things, they can not see 5 years from now, they dont have confidence

Infact wasiosoma Tanzania kama akina Diamond na ali kiba, akina wema sepetu are likely to be more creative and independent thinker kuliko a normal graduate wa UDSM

TATIZO

Mfumo wetu wa ualimu, aina ya ufundishaji na mindset za watanzania za kutoka ukoloni ndio zimetufikisha hapa

Hapa Sio graduate wa udsm. hapa ni vijana . Una uhakika hao wa ifm, mzumbe ,tumain compitance yao ikoje? Tulipo fikia vijana ndio wa kufanya mabadiliko katika nchi hii habar ya uliko soma haiusiki ata kidogo kwenye mwonekano wako kama kijana
 
Hii kitu ina uhalisia mfano kila kwenye duja.mtaani basi asubuhi au jioni linageuka kijiwe cha vijana wa kiume, wakike kila saloon aua stationary inageuja kijiwe au duka linalouza pombe utakuta kijiwe. Tafsiri ya watu kukaa kijiwe ni umbeya na unafiki na kuzungumzia habari za watu. Nchi kama finland mazingira tuu yanakufanya unaacha kuwa muongo na mzushi. Lakini sio Tanzania jamani mtu anadanganya hata kama hanufaiki na huo uongo.
Mkuu Tanzania kuna watu wana PHD za majungu na kufuatilia maisha ya watu , wapo watu hawana pesa lakini badala ya kutumia huo mda kuchakarika anakaa kijiweni kutegea upite akuombe chochote na endapo utampatia pesa anashinda akikusifia sana, balaa huanza endapo utawanyima pesa hapo lazima ujadiliwe Kwa kila hali na kupakaziwa uongo mwingi sana, Vijiweni na bar story zilishakwisha siku nyingi kilichobaki ni majungu pekee na story za kijinga jinga , Vijana hawataki kujituma wanapenda sloppy sana.
 
Back
Top Bottom