Tanzania katika ubora wa Afrika

TAECOLTD

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
1,051
1,835
Tanzania imepata headlines nyingine baada ya kupata mshindi msomi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Aneth David ambaye ameshinda tuzo ya Mwanasayansi mkubwa ajaye duniani akiwa bado ni Mwanafunzi wa sayansi kwenye chuo kikuu cha Dar es salaam.

Tuzo inaitwa Next Einstein Forum Ambassador na imeandaliwa taasisi ya Next Einstein Forum ambao wanaamini kwamba Einstein anaekuja ambaye alikua Mwanasayansi mkubwa wa Marekani atatoka Afrika, Mwanasayansi huyu aliweza kutabiri mambo yaliyokuja kutokea miaka 100 baadae.

‘Next Einstein Forum wanaamini kuna Wanasayansi wanaofanya mambo makubwa na mazuri na yanasaidia jamii zao lakini wamefichika wapo vichakani, kinachojulikana zaidi kutoka Afrika ni vita njaa na magonjwa’ – Aneth

Aneth amesema alipeleka maombi ya kushiriki tuzo hii July 2015 na baadae akapata majibu, kulikua na Watanzania kama watano aliowaona walioshiriki kama yeye lakini yeye ndio akatajwa mshindi, kulikua na Wawakilishi 54 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambapo kila nchi imepata mwakilishi wake, yeye ndio mshindi wa Tanzania.

March 2016 washindi walikutana Senegal kwenye mkutano mmoja na Mawaziri wa Sayansi Afrika na Marais akiwemo Rais Paul Kagame na kuwaleta pamoja na Wadau wa sekta binafsi, hii ni kama kuileta dunia pamoja na Washindi hawa wanapata nafasi ya kuonyesha project zao kuzisaidia nchi zao.
 
me nimecheka hapo tu kwenye wengine wapo vichakani, kwahiyo africa tupo vichakani??
 
Alichomainisha ni kwamba Africa ina wanasayansi wengi na wazuri lakini hawapati wasaa mzuri wa kufanyia kazi na vipaji vyao.sababu ya Vita kushamiri. Hivyo watu nje ya Africa hudhani kwamba Africa inajulikana zaidi kwa vita kuliko kazi zingine za maana
 
Ila kesho keshokutwa ukifuatilia habari za mwanasayansi huyu, utaambiwa yupo CCM ama CDM anafanya siasa badala sayansi.
Hahahahahha ndio Tanzania yetu mkuu watu wanaweka kando taaluma zao wanaangalia chekeli (pesa) mbele...
 
Ila kesho keshokutwa ukifuatilia habari za mwanasayansi huyu, utaambiwa yupo CCM ama CDM anafanya siasa badala sayansi.
Ndio tatizo.tamaduni zetu zimejengwa kwanamna hii mtu.ukiwa napesa ndio una heshimika , kuliko ku saidia vitu mbalimbali. Kama kubuni na kufumbua vitu.nakwakua kila mtu ana taka heshima , ndio.unakuta watu wana kimbilia kwenye pesa ili waheshi mike.
 
Ni kweli kabisa mkuu wataalam wetu wengi wanapotelea kwenye siasa wanakuwa waongo na mafisadi badala ya kuisaidia jamii kwa utaalam wao waliosomea

Ndicho kinachotutafuna Tanzania na Afrika kijumla, wataalam hawataki kujitolea Bali wanataka kulipa elimu yao, watu wanakimbilia kwenye uongozi wa siasa, Matokeo yake mpaka Leo nchi zetu haziwezi tengeneza hata baisekeli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…