Hii hoja huwa siielewi kwa sababu kuna kipindi huko nyuma yaani mwaka jana tu kipindi cha sekeseke la Muungano wazanzibar wanadai tulio bara tunawanyonya sana wao na ndio maana walitaka wajitenge, lakini kuna mambo nafikiria naona kama wao ndio wanyonyaji.
Mfano MCC wamekata mifereji ya ka tirioni 1 anayeathirika ni nani lakini makosa ya zanzibar uchaguzi, vilevile rasilimali mfano gas, madini, mbuga za wanyama, bandari nyingi ziko bara (Tanga, Dar, Mtwara).
Chakula kiko bara, hata mapato ya TRA na ZRA yaani hayalingani hata kidogo sasa hawa wazanzibar tunawanyonya kivip labda kwa upeo wangu sielewi naomba kueleweshwa.
By 2030 asilimia 30 mpaka 40 ya wakazi wa dar watakua wazanzibar. Kwa sasa hivi nadhani ni asilimia 20 - 25. Huu muungano hauwezi kuvunjika tena kwa sababu damu ishavuka upande wa pili wa bahari. Tukisema leo wazenji wote warudi kwao basi vile visiwa viwili havitatosha.