Tanganyika (Tanzania) Ingekuaje kama Wajerumani wangeshinda WW II

Deutsche Ost Afrika(German East Africa) ni Nchi tatu Tanganyika, Rwanda na Urundi(Burundi), Makoloni mengine yalikuwa ni Namibia(Deutsche Süd West Afrika); Kamerun na Togo.

Mwingereza hakuja tu kwa hiari au kwa kushinda vita bali, alikabidhiwa Tanganyika na Umoja wa Mataifa( League of Nation) aisimamie kama baba mlezi mpaka itakapokuwa na uwezo wa Kujitawala.
Rwanda na Urundi alikabidhiwa Ubelgiji(Ubeleji) , Togo na Kamerun alikabidhiwa Ufaransa.
Ujerumani akaachiwa Namibia pekee.
Hongera kwa jitihada zako mkuu. Hata hivyo naomba nikuweke sawa wewe, mleta mada na wasomaji wengine kuhusu mambo mawili.

Jambo la kwanza ni kwamba Togo na Kamerun hakukabidhiwa kwa Ufaransa pekee. Ukweli ni kwamba kila moja ya makoloni haya mawili iligawanywa katika pande mbili yaani mashariki na magharibi. Sehemu ya mashariki ya kila koloni walipewa Wafaransa huku sehemu ya Magharibi wakipewa Waingereza (kama kumbukumbu zangu zipo sahihi). Hapa sitaelezea jinsi makoloni haya mapya yalivyotawaliwa.

Jambo la pili ni kwamba Namibia haikubaki kwa Wajerumani bali ilikuwa chini ya uangalizi wa League of Nations ambapo baadae wakaiweka chini ya uangalizi wa serikali ya Umoja wa Afrika ya Kusini ( South African Union government) ambayo ilianza mwaka 1910. Hatua ya kuikamilisha Namibia kwa serikali ya Afrika ya Kusini iliambatana na masharti kadhaa. Hapa pia sitaendelea zaidi.

Asante.
 
Wajerumani walikuwa na mipango mikubwa sana na Dutch East Africa, mipango hiyo yote ilizimika baada ya kushindwa kwao katika vita kuu ya pili ya dunia (II WW). Makoloni ya Mjerumani Afrika ilikua Tanganyika na Namibia, lakini mapenzi yao makubwa yalikua Tanganyika na waliamua kuifanya ndio makao yao makuu ya Afrika. Ulishawahi kufiikira tungekua wapi kama wangeshinda wajerumani.
Mkuu, tena mji waliokuwa wakiependa naambiwa ni Tabora na ndio mji wa kwanza katika Afrika Mashariki kutengenezwa pesa ya noti.
 
Mkuu, tena mji waliokuwa wakiependa naambiwa ni Tabora na ndio mji wa kwanza katika Afrika Mashariki kutengenezwa pesa ya noti.
Tabora, Dar es Salaam na Tanga waliipenda sana miji hii. Lushoto na Iringa pia walipenda hali ya hewa.
 
Hongera kwa jitihada zako mkuu. Hata hivyo naomba nikuweke sawa wewe, mleta mada na wasomaji wengine kuhusu mambo mawili.

Jambo la kwanza ni kwamba Togo na Kamerun hakukabidhiwa kwa Ufaransa pekee. Ukweli ni kwamba kila moja ya makoloni haya mawili iligawanywa katika pande mbili yaani mashariki na magharibi. Sehemu ya mashariki ya kila koloni walipewa Wafaransa huku sehemu ya Magharibi wakipewa Waingereza (kama kumbukumbu zangu zipo sahihi). Hapa sitaelezea jinsi makoloni haya mapya yalivyotawaliwa.

Jambo la pili ni kwamba Namibia haikubaki kwa Wajerumani bali ilikuwa chini ya uangalizi wa League of Nations ambapo baadae wakaiweka chini ya uangalizi wa serikali ya Umoja wa Afrika ya Kusini ( South African Union government) ambayo ilianza mwaka 1910. Hatua ya kuikamilisha Namibia kwa serikali ya Afrika ya Kusini iliambatana na masharti kadhaa. Hapa pia sitaendelea zaidi.

Asante.

Mkuu, umejaribu kuelezea lakini naomba nikuweke sawa hapo kwenye mgawo.

Mimi sitasahau historia maana wengine humu kama mmeisoma vizuri huwezi kusahahu huu mkataba wa Varsailles.

Pia nakumbuka kulikuwa na suali katika A level la kuhusu kufafanua mkataba huu wa Versailles.

Ni mkataba mreefu unaojumuisha sehemu mbalimbali duniani lakini ntaelezea kwa Afrika.

Huu ulikuwa ni mkataba baina ya Ujerumani na nchi za magharibi wakiongozwa na Uingereza katika kuhakikisha vita haitokei tena.

Hivyo ukasainiwa tarehe 19 juni mwaka 1919 na mwezi October mwaka huohuo wa 1919 mkataba huu ukarekodiwa na League of Nations ambayo baadae (1945) ilikuja kuwa United nations.

Sasa mkataba ulikuaje?

Kipengele cha 119 kilitaka Ujerumani itangaze kwamba inaachia makoloni yake yaliyokuwa yakitunzwa na kampuni yake ya Germany East Afrika.

Baada ya hapo kipengele cha 22 kikatangaza kuwa makoloni hayo sasa yatakuwa chini ya jumuiya ya kimataifa au league of nations.

Hapa Uingereza akajitwalia kampuni ya Germany East Afrika (Tanganyika) ambayo mwanzo ilijumuisha koloni lililounda Tanganyika, Rwanda na Urundi, lakini sasa Rwanda na Urundi akapewa Ubelgiji.

Mfaransa akapewa Togo (Togoland) na Cameroon (Germany Kamerun)

Germany South West Afrika ambayo leo ni Namibia akapewa Afrika Kusini.

Pia katika kulipa fidia kwa Ujerumani kuivamia ardhi ya Ureno ambayo ilikuwa ikiitwa Portugese Afrika, Wajerumani wakany'ang'anywa sehemu moja ya Msumbiji inaitwa Kionga Triangle ambayo ipo kaskazini kwa msumbiji na ilikuwa pia chini ya kampuni ya Gremany East Afrika.

Wamakonde wa hapo Kionga wengi wao wanazunguza kireno lakini kuna makabila mengine kama ya Wamakua na Wamwani.

Sehemu hiyo ilikuwa kubadilishwa jina na kuwa inaitwa Cabo Delgado na makao yake makuu yanaitwa Pemba ambao ndio mji mkuu.

Wakuu historia ipo na ni sisi tu watanzania kuendelea kuelewa khasa hizi historia kwani historia inahusu jana, leo na kesho.

Nikurudi kwa mleta mada kuhusu kama leo tungekuwa wapi ni kwamba ilitegemea na malengo ya mkoloni lakini leo hii ukifika Windhoek Namibia utashangaa jinsi ilivyopangwa na haina tofauti sana na mji wa Tanga.

Wajerumani bado wapo pale na wanajihesabu kama ni wanamibia.
 
Inawezekana Mfaransa alipewa Togo (Togoland) na Cameroon (German Kamerun) kwenye maandishi tu. Lakini in practice, Togo na Kamerun zote ziligawanywa kati ya Waingereza na Wafaransa. Fuatilia tu utaona.
 
Hii sehemu ilikuwa ikijulikana kama Togoland na ilikuwa maarufu kwa kuuza watumwa, lakini wajerumani walikuwa wakimiliki sehemu hii pamoja na Kamerun baada ya mkutano wa Berlin au Berlin Conference uliofanyika kati ya 1884-1885.

Pia hii Togoland haitofautiani sana na Tanga kwa miundombinu kama reli na madaraja na walikuwa wakizalisha mazao ya biashara kama pamba, kahawa na kokoa, na mjerumani alileta mbinu za kilimo cha kisasa zaidi kwa mazao haya matatu.

WW1 ilipoanza mwaka 1914 Uingereza na Ufaransa (ambao walikuwa wakiimezea mate hii sehemu) wakavamia Togoland na kuifanya ni sehemu yao lakini baadae mwaka 1916 Muingereza na Mfaransa wakagawana sehemu hii na ikawa na tawala mbili yaani British Togoland na French Togoland.

Sasa katika mkataba wa Versailles Mjerumani kwa kuwa bado alikuwa akitajataja hili eneo kwamba bado ni lake ndio akaambiwa afute mawazo hao kwamba hii ni sehemu yake yaani "denouncing" kwamba Togoland si mali wala koloni lake tena.

Tusome Historia ya Afrika wakuu, ni somo zuri na muhimu sana.
 
Inawezekana Mfaransa alipewa Togo (Togoland) na Cameroon (German Kamerun) kwenye maandishi tu. Lakini in practice, Togo na Kamerun zote ziligawanywa kati ya Waingereza na Wafaransa. Fuatilia tu utaona.
Nilitaraji uzi huu ungekuwa na hits nyingi, lakini naona nyuzi za udaku ndo zinatia fora. Hii historia tuliyoshuka hapa ni muhimu sana, hasa mtu akitaka kujua kwa nini Mwingereza hakuwekeza sana kwenye miundombinu na uchumi hata Tanganyika ukilinganisha na nchi jirani, ukizingatia kwamba alikaa Tanganyika kwa zaidi ya miaka 40.
 
Dada. Mada yako imenikubusha Chuo. Miaka rundo ilopita. Kuliwahi kuwa na swali Why D. Cameron is known as architect of modern Tanzania.

Haha hiyo jamaa Ndo aliweka un tarmac road za kufika Tabora, ujiji Arusha Mza Mbeya na nk
 
mji wa kwanza kutengeneza pesa sio kilwa?
Tatizo la wasomi wetu ni kujikita kwenye kujua mambo ya Ulaya tu, wanapaswa kufanya utafiti wa kweli na kuandika historia ya nchi yetu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
 
Nilitaraji uzi huu ungekuwa na hits nyingi, lakini naona nyuzi za udaku ndo zinatia fora. Hii historia tuliyoshuka hapa ni muhimu sana, hasa mtu akitaka kujua kwa nini Mwingereza hakuwekeza sana kwenye miundombinu na uchumi hata Tanganyika ukilinganisha na nchi jirani, ukizingatia kwamba alikaa Tanganyika kwa zaidi ya miaka 40.
Mkuu, tuna fikra finyu mno sie. Utakuta mtu hafahamu jambo lililoandikwa ila atarukia tu ku'comment' tena basi atatoka nje kabisa kwa kuleta masuala ya siasa.
 
Sasa Wakuu Jacobus na Idimi, mchango wenu ni nini hapa?

Maana ili kuja kuanza kufafanua maendeleo ambayo mjerumani angeleta Tanganyika, kuna wakuu wengine waliingilia kwa kuchanganya timeline ya WW1 na WW2, hivyo kuna kuwekan sawa katika hilo huku tukijadili mada iliyoletwa na mkuu Sky Eclat.

Hivyo inabidi sasa tujadili maendeleo ambayo yangekuwepo leo kama kule Windhoek na sio katika miji ya Tanga, Dare-es-Salaam na Lome mji mkuu wa Togo.

Haya tuendelee je Tanga na Dar pangekuwaje leo hii kiuchumi endapo wajerumani wangeendela kuwepo?
 
Ni dhahiri mkuu tusingekuwa hivi kama Mjerumani asingefurushwa, huyu hana longolongo na maneno mreeeeeeefu! Na tatizo tunakingwa kuwa na mahusiano ya moja kwa moja na Ujerumani.
 
Wakuu Sky Eclat na Mndengereko One, hii nimeikokotoa humuhumu kwenye Jukwaa hilihili lisemalo - Historia ya Sarafu Yetu Tanzania ya Kichuguu. Kifupi tu kaandika - 'Sarafu ya rupie 15 ilikuwa ya dhahabu, ilijulikana kama "Tabora Pound." Ni kati ya sarafu ambazo zilikuwa ghali sana katika historia ya nchi. Kwa bahati mbaya siyo sarafu nyingi zilizoingia kwenye mzunguko kutokana na vita, kwa hiyo nyingi ziliishia kwenye minada ya wakusanya sarafu. Sura yake ilikuwa kama ifuatavyo

rupien 15
15rupien.jpg
'.
 
Wajerumani walijenga reli ya Kati naTanga kwa mikono kwa miaka mitatu tuu,sisi miaka 50 ya uhuru tunawaomba wachina wa-upgrade iwe SGR
Rafiki yangu ametoka Cameroon ananiambia bibi yake alimwambia kama unaolewa na mzung awe Mjerumani, wale watu ni wachapa kazi sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom