Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Kama ulikuwa unafikiria kwamba baada ya umeme wa bwawa na Nyerere kuanza kupatikana basi matatizo ya mgawo wa umeme yatakuwa yamekwisha, basi sasa ni wakati wa kubadili mawazo yako.
Tanesco wanasema kwamba, mgawo wa umeme Tanzania kimsingi hautokani na ukosefu wa umeme wa kutosha, bali ni kwa sababu miundombinu ya kutawanya umeme iliyopo haitoshi kupeleka umeme kwa kila mtumiaji kwa wakati mmoja!
Kwa kifupi wanasema chakula kipo kingi ila vyombo vya kukupakulia chakula ndio hatuna, basi endelea kuvumilia kukaa na njaa! Kwa hiyo usiuze generator yako, bado unaihitaji.
Serikali hii inatunyoosha kwelikweli!
----
Mkoa wa Kitanesco Temeke wamesema kuwa hawana changamoto ya uchache wa umeme, bali wana umeme mwingi isipokuwa miundombinu haina uwezo wa kubeba wingi wa umeme uliopo hali inayopelekea wananchi kupata mgao
Meneja mkoa wa kitanesco Temeke Ezekiel Mashora amesema Serikali imeleta mradi wa Dharula wa ujenzi wa nyaya utakaosaidia kusafirisha umeme kutoka kituo kimoja kwenda kingine na kuondoa mgao wa umeme kwenye maeneo ya Temeke, Mbagala na Kurasini.