SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MAENEO YA MKOA WA ILALA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Ilala kuwa line za Umeme za TOL,
D7, D11 na Ilala kwenda Kurasini zimezimwa leo Machi 10,2016 asubuhi kwa ajili ya kuhamisha wateja wote walioungwa kwenye ya TOL ili kufanya matengenezo. Maeneo yanayokosa umeme ni Ilala yote, Buguruni, Msimbazi na Mchikichini. Umeme utarejeshwa saa 11.00 jioni baada ya kukamilika kwa kazi hiyo.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utajitokeza.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu