TANESCO ina Kirusi gani kisichokuwa na dawa hicho?

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,625
3,141
Nimekuwepo maeneo ya Mji wa Makambako kwa takribani wiki tatu hivi mpaka sasa nikiporudi nyumbani kwetu.
Karibu kila siku umeme lazima ukatike kwa muda. Hii ni tofauti kabisa na kipindi cha JPM ambapo umeme haukuwa unakatika kabisa. Nililazimika kuahirisha baadhi ya shughuli zangu kutokana na tatizo la umeme.
Shida ni nini hasa?
 
Acha ujinga wako
 
Tangu nipo shule ya msingi 1996 nilikuwa najibu mabwawa ya kuzalisha umeme ni KABORA BASA, NYUMBA YA MUNGU, MTERA, KIDATU mpaka advance majibu yalikuwa yale yale inamaana mabwawa hayajaongezeka na mengine hayafanyiwi matengenezo yamejaa MATOPE. Ila cha kushangaza Kaya za kutumia umeme tangu nasoma hadi leo zimeongezeka mama kwa mamia zikihudumiwa na mabwawa yaleyale mpaka juzi JPM kaanzisha hilo bwawa jipya huko Rufiji na bado halijaisha.
HII inajieleza kabisa TANESCO inatakiwa isaidiwe imeelemewa hata kama serikali imeipa u MONOPOLY SUPLY.
Lingine Africa tuhame HEP ni chanzo hafifu cha umeme.
 
Tabora pamekua hovyo kabisa
Walianza kutoa taarifa kila siku eti kuna hitilafu sasa kibaya zaidi unakuta umeme unakatwa 7AM unarudishwa 06PM na rotation ikawa inafanana kwa maeneo
Hatimae waliamua kutoa ya upungufu wa umeme ratiba iliyoanza J3 inaenda mpka Jpili
 
Tangu nipo shule ya msingi 1996 nilikuwa najibu mabwawa ya kuzalisha umeme ni KABORA BASA, NYUMBA YA MUNGU, MTERA, KIDATU mpaka advance majibu yalikuwa yale yale inamaana mabwawa hayajaongezeka na mengine hayafanyiwi matengenezo yamejaa MATOPE. Ila cha kushangaza Kaya za kutumia umeme tangu nasoma hadi leo zimeongezeka mama kwa mamia zikihudumiwa na mabwawa yaleyale mpaka juzi JPM kaanzisha hilo bwawa jipya huko Rufiji na bado halijaisha.
HII inajieleza kabisa TANESCO inatakiwa isaidiwe imeelemewa hata kama serikali imeipa u MONOPOLY SUPLY.
Lingine Africa tuhame HEP ni chanzo hafifu cha umeme.

Kwa hiyo Billie hujui kama kuna umeme wa gesi kutoka mtwara? Au unataka wasaidiwe vipi? Na katika yote hayo sio maharage wala malope aliyewahi kulalamika kuhusu vyanzo vya umeme ila uchakavu wa mitambo na njia. Kwa hiyo umeme wa kutosha upo sana tu. Tatizo ni Tanesco uongozi na wafanyakazi wote wa tanesco
 
Umeshafuatiliaga story ya umeme wa gesi tangu tuambie utazalisha megawatt za kutosha na tutaanza kuuza nchi jirani mpaka sasa kipi kilikwamisha?
 
Nilimaanisha vyanzo vya umeme nchini sio maji tu. Kuna gesi pia hilo la ufanisi ndo hapo tuwaulize tanesco na uongozi wote wa tanesco. Hiyo tanesco kuanzia uongozi wa juu hadi mfanyakazi wa chini kabisa wote viazi tu.
 
bwawa ya kuzalisha umeme ni KABORA BASA

Tete, Mozambique
Ziara ya kihistoria ya rais Samora Machel wa Mozambique kwenye bwawa la umeme la Cabora Bassa jimbo la Tete, nchini Mozambique ambalo lilijengwa na wakoloni wa Kireno wakati wakiikalia nchi ya Msumbiji.

Source : Yassin Amuji
 
Back
Top Bottom