Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 76,008
- 120,240
Nimepata private message ya Diallo on the matter, Magufuli na serikali yake wanachemka sana.Ada ya masafa na leseni ni shilingi milioni mia tano kwa mwaka?
seriously?
Diallo analipa hela nyingi kuliko the rest of media houses in the lake zone combined, amelipa 75% ya deni lake, na kulikuwa na makubaliano ya kulipa zote.Isitoshe, wanalipishwa kwa USD kinyume na maagizo ya BOT.
July to October tu mwaka 2015 wanadai wamelipa Sh 210 m.
Kwa kawaida, mtu anayefanya biashara na uongozi, mdeni hafungwi kwa kutolipa deni kama ameonyesha nia ya kulipa deni, analipa deni kila mwezi na kashalipa zaidi ya 75% ya deni.
Kama haya madai ni ya kweli, serikali ya Magufuli inazidi kuniaminisha kwamba inafanya kazi kwa pupa.
Zaidi, hizi ada ziko juu sana kiasi kwamba zinakuwa anti business. Katika structuring ya kodi na ada, ukiweka kodi na ada za juu sana unaweza kuua ng'ombe anayekupa maziwa kwa kumkamua mpaka damu. Isitoshe, ada za juu sana zinaweza kuwapa watu ushawishi wa kutafuta mianya ya kukwepa ada.