polokwane
JF-Expert Member
- Dec 16, 2018
- 3,361
- 5,836
Kuna Halmashauri nyingi hapa nchini zimetoa maelekezo kwamba vifaa vya ujenzi watanunua wao wakati huo pesa imeingizwa kwenye accounts za shule, TAMISEMI kama mmetoa maelekezo haya basi wekeni utaratibu mzuri kabisa ili wasije wakazidisha bei ya vifaa maana halmashaur zetu huko kuna shida sana na matokeo yake pesa isitoshe, maana kuna dalili za wizi hapa na tuhuma zitaelekezwa kwa walimu wakuu.
Kuna kipindi ujenzi huuhuu kuna halmashauri zilitumia njia hii matokeo yake baadhi ya shule wakajikuta wanapelekewa malipo ya saruji Tsh 18,500/ kwa mfuko wakati bei ya sokoni kwa mfuko ni Tsh 15,500/ na mifuko bado haikutosha na pesa zimeisha na ujenzi ukakwama.
Kama TAMISEMI mmeliweka katika utaratibu huu ambao ukifanyika kwa uzalendo kabisa ni mzuri sana ila tu usimamizi uwe wenye umakini ili kuepusha wizi wa kuongeza gharama na kusababisha pesa kuto tosha.