TAKUKURU yaanza kuchunguza jinsi Waziri Lukuvi alivyokataa rushwa ya bilioni 5

Lukuvi alikurupuka kwa kauli yake hiyo, tena alitakiwa apandishwe kizimbani akaseme ni kwa vipi yeye kama kiongozi wa serikali alishindwa kuwachukulia hatua ya kisheria watu waliojaribu kumuhonga pesa akiwa kwenye wadhifa wa kiserikali? Kama kiongozi mwandamjzi wa serikali alitakiwa kushiriki kikamilifu kauli mbiu ya kutotoa wala kupokea rushwa kwa vitendo na sio maneno.
 
1.jpg

Takukuru imeanza kuchunguza taarifa kwamba Waziri wa Ardhi, William Lukuvi alikataa kupokea rushwa ya Sh5 bilioni iliyotaka kutolewa na wafanyabiashara wawili wakubwa ili kuwapitishia mradi wa Sh84 bilioni.

Katika mahojiano na gazeti la Mwananchi hivi karibuni, Waziri Lukuvi alisema kwamba lengo la wafanyabiashara hao ilikuwa ni kufanikisha mpango wao wa kuiuzia Serikali ardhi kwa bei kubwa kwenye eneo linalotakiwa kujengwa mji wa kisasa wa Kigamboni.

Licha ya kukataa kutaja majina ya wafanyabiashara hao, Lukuvi alisema mtandao huo wa wafanyabiashara ni hatari na unaweza kusababisha mtu ashindwe kufanya kazi ya wananchi iwapo ataendekeza rushwa.

Jana, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Valentino Mlowola alisema kutokana na taarifa ya kiongozi huyo, ofisi yake iliamua kuchukua chanzo hicho na kuanza kazi ya uchunguzi.

Hata hivyo, Mlowola hakutaka kuweka wazi kazi ya uchunguzi huo imeanza lini wala ilipofikia.

“Kueleza tumeanza lini hilo ni suala la kiufundi, tumeshaanza kushughulikia,” alisema Mlowola ambaye Rais John Magufuli amemuidhinisha rasmi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo baada ya kukaimu kwa miezi kadhaa.

Katika ufafanuzi wake, kamishna huyo wa zamani na mkurugenzi wa Intelijensia ya Makosa ya Jinai katika Jeshi la Polisi, alisema taasisi hiyo kwa sasa imekuwa ikichukua tuhuma yoyote ya rushwa kutoka chanzo chochote baada ya kuripotiwa.

Katika mahojiano hayo, Waziri Lukuvi alisema wafanyabiashara hao waliwaeleza marafiki zake wa karibu kuwa wangempa rushwa.

Mji huo mpya wa Kigamboni unajumuisha kata za Kigamboni, Tungi, Vijibweni, Mjimwema, Kibada, Somangila na eneo lote hilo lina ukubwa wa takribani ekari 6,000.

Awali mradi huo ulitarajiwa kugharimu Sh13 trilioni ambazo zingetolewa na Serikali, lakini ikaamua kushirikisha sekta binafsi ili kuujenga na Serikali ishughulikie uwezeshaji wa awali.

Lukuvi ambaye alihamishiwa Wizara ya Ardhi mapema mwaka jana na kubakizwa katika wizara hiyo na Rais Magufuli, alisema amegundua kuna mtandao mkubwa wa rushwa unaoanzia ngazi ya halmashauri mpaka wizarani ambao unahusisha maofisa wa Serikali na viongozi wa wizara.

“Kama ukiwa na tamaa huwezi fanya kazi uliyotumwa. Kuna wakati walikuja ni wafanyabiashara wawili wakubwa na kutaka wanipe Sh5 bilioni ili nikubali kupitisha mradi wao wa mabilioni ya shilingi na walitangaza kwa marafiki zangu kuwa wangenipa fedha, lakini hapa hawawezi,”alisema Lukuvi.

Aliongeza: “Wakati naingia tu wizara hii nilikuta harakati za kukamilisha mradi wa Kigamboni ukiwa katika hatua za mwisho na kila kitu kilikuwa kimekamilika. Lakini nilipopitia vizuri nilikataa kuwalipa wafanyabiashara hao. Cha ajabu hazikupita siku mbili walipata taarifa wakaja mbio kutaka kuniona.”

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, wafanyabiashara hao walitaka walipwe Sh141 milioni kwa kila ekari wakati wao walinunua ardhi kutoka kwa wananchi kwa Sh5 milioni kwa ekari, jambo ambalo alisema lilishapitishwa awali.

“Niligundua pale kuna udanganyifu na wizi mkubwa. Haiwezekani mwekezaji anunue kutoka kwa wananchi ekari moja kwa Sh5 milioni, kisha Serikali tumlipe Sh141 milioni kwa ekari kwa kuvuka pantoni tu. Ni wizi mkubwa.

"Kama kweli Serikali ina fedha hizo kwa nini tusimlipe mwananchi moja kwa moja?” alihoji.

Waziri Lukuvi alisema endapo njama hizo zingefanikiwa, Serikali ingetumia zaidi ya Sh84 bilioni kuwalipa wawekezaji hao hewa kwa kuwa mmoja anamiliki takribani ekari 200 na mwingine 400.

“Niliwaambia Serikali haiwezi kuwalipa fedha hizo na badala yake waende kuiendeleza ardhi wenyewe kulingana na mradi unavyotaka. Walitaka kutajirika kwa ujanja ujanja,” alisema Lukuvi na kuongeza:

“Eti walidai wamekopa fedha benki kwa ajili ya mradi huo. Haiingii akilini mtu utumie Sh5 milioni, halafu uje uvune mabilioni ya fedha kwa kuvuka pantoni tu.”

Chanzo: Mpekuzi
hiyo kazi kama tukipewa sisi kina gogo la shamba tutaifanya kwa siku mbili tu, na kupata jibu maana ni kiasi cha kumuuliza Lukuvi ni kina nani waliotaka kumpa rushwa na hatua ya pili ni kuwauliza hao waliotaka kumpa rushwa wakukubali tunatoa ripoti wakikataa tunatoa ripoti kwamba Lukuvi ni muongo, hivyo ni kazi ya siku mbili tu,
 
Takukuru si mngeanza na huyo bwana February marope...maana kimambi alisema anaushahid kabisa. Wachen maigizo
 
Aliriport TAKUKURU? Kama hakuriport ni kwanini hakufanya hivyo, huyo ana nia ya dhati kweli kupambana na rushwa au alikuwa anasoma upepo akaona hausomi vizuri ndiyo akaipotezea! Suala kama hilo siyo la kuja kubwabwaja kwenye vyombo vya habari bila kureport!
 
Mmezoea kuona maigizo huko kwenu, Lowassa akila na mamantilie wakati wa kampeni, leo kwanini asile nao? Hapakazitu.
Sijui una umri gani ila punguza ushabiki na kujikomba unajidhalilisha..
Hivi ni mangapi yanapita kwa rushwa kama hizi na wala hayasemwi iweje hili muone ndio dili.. Ndomana unaambiwa haya ni maigizo kwa ajili ya kuwahadaa wajinga ila werevu wanestuka siku nyingi..
 
Huu ni usanii.Viongozi wetu nadhani wana shida kubwa.Lukuvi ni kiongozi aliyepewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Ardhi na nadhani anajua sheria za nchi.Kama wame-attempt kumhonga hao ni watuhumiwa,angewaripoti TAKUKURU au Polisi straight away,yeye awe shahidi.If he doesn't want to do that he should keep quiet or else tutamuona pwagu.Kubwabwaja hakutatusaidia sana.
1.jpg

Takukuru imeanza kuchunguza taarifa kwamba Waziri wa Ardhi, William Lukuvi alikataa kupokea rushwa ya Sh5 bilioni iliyotaka kutolewa na wafanyabiashara wawili wakubwa ili kuwapitishia mradi wa Sh84 bilioni.

Katika mahojiano na gazeti la Mwananchi hivi karibuni, Waziri Lukuvi alisema kwamba lengo la wafanyabiashara hao ilikuwa ni kufanikisha mpango wao wa kuiuzia Serikali ardhi kwa bei kubwa kwenye eneo linalotakiwa kujengwa mji wa kisasa wa Kigamboni.

Licha ya kukataa kutaja majina ya wafanyabiashara hao, Lukuvi alisema mtandao huo wa wafanyabiashara ni hatari na unaweza kusababisha mtu ashindwe kufanya kazi ya wananchi iwapo ataendekeza rushwa.

Jana, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Valentino Mlowola alisema kutokana na taarifa ya kiongozi huyo, ofisi yake iliamua kuchukua chanzo hicho na kuanza kazi ya uchunguzi.

Hata hivyo, Mlowola hakutaka kuweka wazi kazi ya uchunguzi huo imeanza lini wala ilipofikia.

“Kueleza tumeanza lini hilo ni suala la kiufundi, tumeshaanza kushughulikia,” alisema Mlowola ambaye Rais John Magufuli amemuidhinisha rasmi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo baada ya kukaimu kwa miezi kadhaa.

Katika ufafanuzi wake, kamishna huyo wa zamani na mkurugenzi wa Intelijensia ya Makosa ya Jinai katika Jeshi la Polisi, alisema taasisi hiyo kwa sasa imekuwa ikichukua tuhuma yoyote ya rushwa kutoka chanzo chochote baada ya kuripotiwa.

Katika mahojiano hayo, Waziri Lukuvi alisema wafanyabiashara hao waliwaeleza marafiki zake wa karibu kuwa wangempa rushwa.

Mji huo mpya wa Kigamboni unajumuisha kata za Kigamboni, Tungi, Vijibweni, Mjimwema, Kibada, Somangila na eneo lote hilo lina ukubwa wa takribani ekari 6,000.

Awali mradi huo ulitarajiwa kugharimu Sh13 trilioni ambazo zingetolewa na Serikali, lakini ikaamua kushirikisha sekta binafsi ili kuujenga na Serikali ishughulikie uwezeshaji wa awali.

Lukuvi ambaye alihamishiwa Wizara ya Ardhi mapema mwaka jana na kubakizwa katika wizara hiyo na Rais Magufuli, alisema amegundua kuna mtandao mkubwa wa rushwa unaoanzia ngazi ya halmashauri mpaka wizarani ambao unahusisha maofisa wa Serikali na viongozi wa wizara.

“Kama ukiwa na tamaa huwezi fanya kazi uliyotumwa. Kuna wakati walikuja ni wafanyabiashara wawili wakubwa na kutaka wanipe Sh5 bilioni ili nikubali kupitisha mradi wao wa mabilioni ya shilingi na walitangaza kwa marafiki zangu kuwa wangenipa fedha, lakini hapa hawawezi,”alisema Lukuvi.

Aliongeza: “Wakati naingia tu wizara hii nilikuta harakati za kukamilisha mradi wa Kigamboni ukiwa katika hatua za mwisho na kila kitu kilikuwa kimekamilika. Lakini nilipopitia vizuri nilikataa kuwalipa wafanyabiashara hao. Cha ajabu hazikupita siku mbili walipata taarifa wakaja mbio kutaka kuniona.”

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, wafanyabiashara hao walitaka walipwe Sh141 milioni kwa kila ekari wakati wao walinunua ardhi kutoka kwa wananchi kwa Sh5 milioni kwa ekari, jambo ambalo alisema lilishapitishwa awali.

“Niligundua pale kuna udanganyifu na wizi mkubwa. Haiwezekani mwekezaji anunue kutoka kwa wananchi ekari moja kwa Sh5 milioni, kisha Serikali tumlipe Sh141 milioni kwa ekari kwa kuvuka pantoni tu. Ni wizi mkubwa.

"Kama kweli Serikali ina fedha hizo kwa nini tusimlipe mwananchi moja kwa moja?” alihoji.

Waziri Lukuvi alisema endapo njama hizo zingefanikiwa, Serikali ingetumia zaidi ya Sh84 bilioni kuwalipa wawekezaji hao hewa kwa kuwa mmoja anamiliki takribani ekari 200 na mwingine 400.

“Niliwaambia Serikali haiwezi kuwalipa fedha hizo na badala yake waende kuiendeleza ardhi wenyewe kulingana na mradi unavyotaka. Walitaka kutajirika kwa ujanja ujanja,” alisema Lukuvi na kuongeza:

“Eti walidai wamekopa fedha benki kwa ajili ya mradi huo. Haiingii akilini mtu utumie Sh5 milioni, halafu uje uvune mabilioni ya fedha kwa kuvuka pantoni tu.”

Chanzo: Mpekuzi
 
Sijui una umri gani ila punguza ushabiki na kujikomba unajidhalilisha..
Hivi ni mangapi yanapita kwa rushwa kama hizi na wala hayasemwi iweje hili muone ndio dili.. Ndomana unaambiwa haya ni maigizo kwa ajili ya kuwahadaa wajinga ila werevu wanestuka siku nyingi..
wewe ndio tukuulize umri na umesoma shule gani maana kukuuliza darasa tutakosea labda hulijui hata darasa, maana ungeingia darasani ungeshaona mambo mazito anayouyafanya Mh Rais na viongozi wake hadi sasa na kuappreciate(kuyakubari kwa nguvu),ikiwa hata nchi za nje wasio watanzania wanayakubali who are you to call them maigizo??!!!?!!!@#$%^!:"::(:! jitambue, jiulize jiongeze....
 
Bil 5 kati ya 85 hivi 10% angalau 8 au 9. Hata kama ni mimi nakataa na kurongosha, yaani wanidhulumu bil 3 au 4 halafu ni wape deal? Haiwezekani
ilo deal litakuwa la tiba , ndio maana halikataa kujiuzulu uwaziri
 
na mimi nilitaka kuuliza hilo ghorofa nani kamjengea?

Ndiyo anatakiwa kutueleza.Maana asiwe kama wale wengine ati mwanaume huyu alitaka kunihonga nikakataa,kumbe alitaka zaidi mwanaume akamute.Sijui na yeye alitaka zaidi wahindi wakagoma..................
 
wewe ndio tukuulize umri na umesoma shule gani maana kukuuliza darasa tutakosea labda hulijui hata darasa, maana ungeingia darasani ungeshaona mambo mazito anayouyafanya Mh Rais na viongozi wake hadi sasa na kuappreciate(kuyakubari kwa nguvu),ikiwa hata nchi za nje wasio watanzania wanayakubali who are you to call them maigizo??!!!?!!!@#$%^!:"::(:! jitambue, jiulize jiongeze....
Hivi kumbe kipimo cha akili ni kuangalia maoni yanayotolewa na watu wa nje..
Hv hujui watu wa nje wengi wao ni wanafiki.
 
Back
Top Bottom