UMUGHAKA
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 2,652
- 12,521
Nsikuchoshe na usinichoshe, tusichoshane.
Mimi kwa upande wangu huwa nakerwa na kuudhika sana na tabia hizi kutoka kwa Watanzania wenzangu.
1. Kukojoa kojoa hovyo.
Unakuta jitu(Hasa wanaume) linakojoa hovyo hovyo maeneo yasiyotakiwa, kila sehemu za kupumzika kwa hapa Dar es Salaam ni lazima utakuta harufu za mikojo, huu ujinga hebu uacheni haraka.
2. Kutembea taratibu kama konokono.
Huwa nachukizwa na tabia ya baadhi ya watanzania kutembea taratibu hata mahali ambapo hupaswi kwenda taratibu, kiukweli huwa nachukia sana, sasa ukute jitu liko mbele yako halafu unawahi, utatamani ulitukane!.
3. Kutokujali muda.
Hii tabia nadhani ni kwa watanzania karibia asilimia 90 hawajali kabisa muda, unakuta umeongea na mtu kuhusu jambo fulani ambalo inapaswa mlikamilishe ndani ya wakati halafu mtu mwenyewe ndiyo kwanza mkikubaliana muonane saa 3 asubuhi, yeye anakuja saa 5 u 6 mchana na sababu kibao zisizokuwa na kichwa wala miguu, hebu badilikeni bhana!.
4. Chuki na Husda
Nadhani wanawake huku walishawaachia wanaume, hii tabia inaendelea kujengeka na inakuwa sugu sana kwa baadhi ya watanzania. Ukifanikiwa kidogo tu majungu na chuki yanaanza utadhani hata walikusaidia kuzitafuta, hebu acheni hizi tabia za kijinga.
5.Umbea na Uongo
Kuna tabia imejengeka hasa kwenye vijiwe vya bodaboda na saluni za kike, yaani unakuta mtu anazungumzwa hapo kiundani utadhani kawakosea nini! Kila mtu atajifanya huyo anayezungumzwa anamfahamu kama wamezaliwa tumbo moja, acheni uongo na umbea fanyeni kazi!.
6. Kukopa harusi kulipa matanga
Hii tabia ishakuwa sugu kwa baadhi ya watanzania, kama umekopa unapaswa ulipe, acheni hii tabia ya kijinga kama mnajua hamuwezi kurudisha, usipokuwa muaminifu kwenye suala la kulipa tafadhali usikope, hii tabia inakera sana na kuudhi.
7.Kuongea broken(Kiswanglish)
You know, Yes my, By that time, End of days, n.k yamekuwa maneno yanayotumika sana na watanzania wengi wapumbavu, amueni moja, kama unaongea kiswahili basi ongea kiswahili fasaha na kama unaongea kiingereza ongea kiingereza fasaha, Acheni huu ujinga wa kujifanya much knows nyingi.
8. Kutupa uchafu hovyo.
Hakuna tabia inayonikera na kuniudhi kama kuona jitu zima lililosoma na kuelelimika linakunywa maji likiwa kwenye gari halafu linatupa makopo hovyo nje ya gari,kwani ukinywa maji,Mo energy,azam energy,soda take away halafu ukatupa kopo ndani ya gari utapungukiwa nini?,Tunzeni mazingira acheni huu ujinga,yaani usafi mpaka serikali ikuwekee sheria msomi mzima?.
Mengine usiku ndiyo muda wa kutoa takataka na kuzitupa kwenye mitaro,acheni huu ujinga.
9. Kuvuta sigara hovyo mbele za watu.
Kwanini kama unataka kuvuta usikae pembeni kabisa kusiko na watu ukaanza kuvuta sigara yako?,aliyekwambia wengine tunapenda huo moshi wa sigara nani?,jaribuni kuwa na hekima bhana siyo tukianza kuongea tuonekane tuna gubu,acheni huu ujinga nyie ni watu wazima.
10. Kunywa pombe kupita kiasi.
Hili limeshakuwa sugu kabisa katika jamii,unakuta mtu anatamba eti "Mimi napiga chupa kubwa la K vant namaliza sembuse hako ka konyagi kadogo!",Hivi aliyekwambia kunywa pombe mpaka ujikojolee ni sifa ni nani?,kwanini usinywe tu kidogo ukachangamka ukajiondokea zako?,aliyekwambia hapo bar utapewa sifa baada ya wewe kunywa castle/Serengeti lite zaidi ya 10 nani?,kwani huwezi kunywa tu kidogo ukaondoka?,Wengine wakishalewa mpaka wanaanzisha na ugomvi kabisa,wengine miili imebaki na makovu kwasababu tu ya pombe,wengine wametengwa na familia zao kwasababu ya pombe,wengine wameacha na kuachwa kwasababu ya pombe.Kwanini msibadilike?,Acheni huu ujinga hata kama pesa ni zenu,narudia tena acheni huu ujinga!.
11.Wanawake kuvaa nguo za kuwachora.
Zamani ili uone tako la mwanamke ni lazima ufunue chupi yake kwanza,sikuhizi imekuwa kinyume chake,ili uone chupi aliyovaa ni mpaka ufunue tako,Hivi kwanini mnafanya hivi?,kuna mmoja nilikutana nae amevaa nguo hadi camel toe inaonekana kiasi kwamba mimi nikaona aibu,yeye alikuwa anatembea hana hata habari,utajua wewe!.
Wanawake vaeni nguo za kusitiri miili na maumbo yenu,acheni huu uzwazwa unakera na kuudhi!.
12.Kudharau magari ya watu.
Unakuta jitu linasema "Siwezi kununua ka-IST mimi", wakati huo halina hata gari linapambania echer za Chanika kila siku!.
Mtanzania mwenzako kapambana kanunua gari yake wewe unakuja mbele za watu na kuanza kudharau wakati huo hata kula na kulipa kodi tu ni changamoto.Hebu acheni hizi tabia za kudharau mali za watu,wewe pambana kivyako nunua V8 ila uache kudharau magari ya watu waliyonunua kwa kutoa jasho!.Acheni hizi tabia za kishenzi shenzi.
Ni hayo tu kwa leo, naachia line!.