Tahadhari na maduka ya kuuza simu mitandaoni location inasoma Pemba Zanzibar

Mngoni asiyepiga gambe

Senior Member
May 4, 2017
139
286
Miezi kadhaa nyuma wife alikuwa anahitaji kununua simu baada ya survey za hapa na pale mitandaon tukakutana na page za kuuza simu mitandaoni location Pemba ila wanatuma mzigo popote.

Bei zake zinaonekana za chini sana kuliko bei za maduka mengi sasa picha linaanza kwenye picha zote kwenye page wamezuia comment.

Tukaamua kabla ya kutuma hela tumtume mtu akathibitishe uwepo wa hilo duka huko Pemba (ni mtu tunayemfaham anaishi huko) kwa zile namba za simu zilizo kwenye instagram kila akipigiwa na mwamba amuelekeze duka lilipo kona kona nyingi mara mwisho akazima simu kabisa akaona pilau litaingia mchanga.

Baadae tukaja kukutana na duka jingine nalo location inasoma pemba story ikawa hivyo hivyo na tukaja ku connect dots kwanza kwann Pemba?

Jibu jepesi Pemba ni sehemu strategic kiutapeli ( mbali kufikika na watu wengi hawapo familiar nayo).

So ni rahisi mtu kuopt kutuma pesa atumiwe mzigo kuliko ku take trouble ya kufuatilia zaidi, lucky for us tulikuwa na mtu kule beware
 
Nakumbuka kipindi iko UDOM pale kuna mwamba alikua ni room mate wangu. Jamaa nae ni mzanzibar.

Akawa ananishawishi ninunue simu kwa hawa wenzake.
Nilichofanya nikampa pesa yeye ili amalizane nao..

Alichofanyiwa daah ni hudhuni ila baada ya hapo nilichomfanyia mimi ilikua hudhuni mara 8..

Maana wapemba sijui wanzanzibar wabishi sana..
Najua huko alipo anasemaga mi ni mtu katili sana 😂😂😂🙌🙌🙌
 
Back
Top Bottom