TAHADHARI: Matangazo ya kazi "Santos Petroleum Corporation"

kakaamiye

Senior Member
Aug 5, 2009
179
90
Nimeona matangazo ya kazi zoom kwenye kampuni inaitwa
'Santos Petroleum Corporation' nafasi zinazotangazwa zipo zanzibar, sina uhakika kama ni ya kweli au la! kwani nimejaribu ku-google hiyo kampuni ya Santos haionekani kama ina project yoyote Africa hivyo ninawatahadharisha waombaji kazi wawe makini isije kuwa ni utapeli, wajiridhishe kabla ya kuomba na hasa wasije wakaambiwa watoe malipo kupata kazi. Hayo ni maoni yangu tu.

Pia kwa mwenye ufahamu zaidi juu ya kampuni hii wanaweza kutufahamisha ili tujiridhishe kabla ya kuomba kazi, huenda ikawa sipo sahihi labda ni wasiwasi wangu
 
Hamna kitu hapo ni ujanja ujanja tu huo. Hilo tangazo linaonekana Zoom tu na hamna source ya hilo tangazo
.
 
Hamna kitu hapo..hii njia wanayoitumia zoom kuvuta waangaliaji wengi.Yaani kukiwa hakuna kazi wanafanya hivi kuiweka website uptodate na refreshing with new vacancies..Hiyo na nyingine nyingi za aina hiyo kama Commercial corporation bank waliyopost kazi muda wa nyuma kdg ni makampuni hewa.Usijisumbue.
 
Kwa nini serikali huwa inalifumbia macho hili jipu. Nimebaini makampuni mengi ni ya kiutapeli na hayapo.
 
Huu ni utapeli grade one...atakuwa ni yule yule anayejiita Mr Kauga.....pumbavu kabisa
 
Hapo ukituma anakuja MTU anakwambia nimeona application zako so kama unataka kaz tuma 30,000 tu hapo mujue munatuma Wengi ukishatuma ukija kumpigia namba haipatikan hasa namba za Tgo na Voda
 
Kwa wanaotafuta kazi.. kwa nini msiende ofisi za zoom na kuwaambia kuhusu hili tatizo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…