Tafakuri: Vyuo vya hovyo hovyo ni vyuo gani?

Nampenda Magu,ila sipendi hulka yake ya ubaguzi. Sijui kwanini aliamua kudhalilisha sekta binafsi zilizowekeza kwenye elimu. Nadhani wahitimu wengi mtaani,ndo wanamnyima raha kwa kuhoji utendaji wa serikali. Asijisahau akaanza kudharau mchango wa mashirika ya dini kwenye afya na maji.
Kwa mawazo yangu huyu mtu inaonesha mazingira alokulia yamemfanya kua hivyo. Maisha yake ya utotoni yamesababisha hivyo yalivyo kutokana na wenye mali, aliwaona ni watu walisababisha awe alivyokua
 
Wakuu heri ya jumatatu ya pasaka

Naomba tushirikiane kuhusu mtazamo wa Rais

Mh.Rais anaamini UDSM ndio chuo pekee kinachostahili kuitwa chuo kikuu
Labda kwasababu naye kabahatika kusoma ud

Lakini kauli zake km kiongoz wa nchi kuvidhalilisha vyuo vingine kuwa ni vibovu na havina sifa je ni sawa?

Juzi wakat ana zindua hostel alisema haina haja ya kuwa na vyuo vingine ambavyo vinadahili wanafunz ilimrad wapate mkopo serkalini tu

Kiukweli Rais hakutakiwa kuvidhalilisha vyuo,
Yeye km kiongozi wa nchi alitakiwa azihamashe na kuzitia moyo taasis za dini na mashirika yaliyoamua kuwekeza katika elimu

Rais anaonekana Bado ana mitazamo ya 80's kwamba chuo kikuu ni UDSM pekeyake

Mh Rais ajue kuwa wanafunz wanaohitimu high school kwa sasa ni wengi sana tofaut na miaka ya nyuma

Hivyo alitakiwa awashukuru watu walioamua kuwekeza katika elimu ya juu badala ya kuwakatisha tamaa

Mh. Rais anatakiwa aelewe na atambue umuhimu wa sekta binafs ndio wenye mchango mkubwa katika Maendeleo ya Taifa

Mh Rais nchi ya Gambia yenye chuo kikuu kimoja tu ndio nchi inayoshikilia mkia kwa ujinga duniani

Mh. Rais jenga mazoea ya kuwatia watu moyo wanaojitolea kwa nguvu zao kusaidia kuijenga nchi yao

Mimi ni mluther, nakumbuka miaka ya 2000's kila jumapili kulikuwa na kikapu cha sadaka kwa ajili ya ujenz wa vyuo vikuu vya Tumaini Tanzania, sasa Tanzania Kuna vyuo vikuu vya Tumaini km viwili Hivi na branch mbili

Naamini hata saut kupitia kanisa Lao la Catholic walichanga ivyo ivyo

Mh. Rais jenga utamaduni wa kuwapongeza na kuwatia moyo wananchi, Usiwe mtu wakuwakatisha tamaa

Tunajua unamamlaka makubwa, lakini jamii inayoheshimiana huishi kwa upendo na Amani zaid

Nyerere mpaka tunamuimba na kumskiliza ni kwa sabab hakuwa mtu wa kujikwezwa

Nyerere angeweza kutumia elimu yake kubwa alyoipata makerere na uingereza kutuadhibu wananchi

Sijawahi kusikia kwenye hotuba zake akizungumzia elimu yake

Napenda nchi yangu Tanzania

Mwenyewe nimejiuliza sijapata jibu.
Kumbe tuna vyuo vya hovyohovyo, kwa nini tunakubali viwepo? Hii inaashiria nini kwa mustakabali wa elimu yetu? Hatuna mamlaka ya kuthibiti vyuo vya aina hiyo? Kwa kauli ya Rais jibu ni ndio.
Wito wangu kwa mheshimiwa Rais usiishie kuongea, vyuo hivyo unavijua ndio mana umevisema, vitumbue au tumbua mamlaka husika.
Kama wewe unalalamika majukwaani sisi tufanye nini?
 
Mkuu tunaogopa kukosoa elimu ya mkuu

Udsm wameweza kumpa PHD mtu asieweza kuongea kiingereza, chakushangaza alitumia lugha hiyo kujifunzia.

Udsm wameweza kumpa Phd ambayo alitakiwa asome kwa miaka 5 yeye kasoma miaka 3. Ni sawa na mtu apewe Degree ambayo alitakiwa asome miaka 3 yeye asome kwa mwaka mmoja.
 
Mkuu wetu kuna kauli anavunja sana moyo
Kiongoz anapokupriempt usitegemee jipya kwenye tasisi yako kiukweli

Mtu kasoma UDSM anaringa kama nini angesoma Harvard University au Oxford si tungekoma sisi tuliosoma sauti, halafu mtu mwenyewe alianzia diploma ndio akaenda bachelor na sisi tulioenda bachelor moja kwa moja mbona hatumringii, vitu vingine vinatia hasira sana
 
Anza na hiii kaka
92dabb12077f0f834aacb3c0a6c2e426.jpg
Asante mkuu
 
Ni ajabu sana mkuu, ukiangalia KCMC inayomilikiwa na wa Lutheran inachuana na muhimbili kutoa huduma lakin Bado mkuu anatoa maneno ya ku demorelize

Nampenda Magu,ila sipendi hulka yake ya ubaguzi. Sijui kwanini aliamua kudhalilisha sekta binafsi zilizowekeza kwenye elimu. Nadhani wahitimu wengi mtaani,ndo wanamnyima raha kwa kuhoji utendaji wa serikali. Asijisahau akaanza kudharau mchango wa mashirika ya dini kwenye afya na maji.
 
Vyuo vya serikali vimebaki na majina tu lkn taaluma na viwango vya elimu vimeporomoka sana.

Nadhani Rais amebaki na historia ya miaka ile ya Mlimani glory. Enzi zetu kusoma sekondari ya private ulionekana mtu aliyefeli, lkn sasa ukisoma shule za serikali unaitwa Kayumba. Taasisi za elimu ya juu zinazomilikiwa na serikali zinebakiwa na majina, na miundo mbinu mizuri tu lkn kitaaluma ziko sawa na vyuo binafsi au viko chini ya vyuo binafsi.

Vyuo vukuu vingi vya serikali vina majina yaliyo hai lkn vimeshajifia.

Vv
 
Na alisoma kipind kile bongo wasomi wa chuo kikuu hawazidi hata mia
Lkn yeye alitumia elimu yake kuwanufaisha wananchi

Nyeyere alipiga Makerere alafu Edinburgh na hakuwahi kusikika akijivunia chuo alichosoma!
 
Back
Top Bottom