SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MAENEO YA MKOA WA ILALA.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa baadhi ya maeneo ya Mkoa wa
Ilala kuwa line namba D10 imezimwa leo Februari 13, 2016 saa 3.00 asbh kwa ajili ya kubadili nguzo na kukata matawi ya miti yanayogonga line hiyo. Maeneo yatakayokosa umeme ni Muhimbili , mtaa wa Kalenga, Mindu, Jangwani na Azania Sekondari.
Wateja wote walijulishwa kupitia vyombo vya habari. Magazeti, Redio na kupitisha gari la Matangazo. Umeme utarejeshwa saa 11 jioni baada ya matengenezo hayo.
MATENGENEZO HAYO YANALENGA KUONDOA KERO YA UMEME KUKATIKA MARA KWA MARA KATIKA MAENEO HAYO.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu.