Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 460
- 1,132
Maombi ya Watu takribani 371 waliokua katika mchakato wa kujaza fomu za kuiomba Serikali ya Switzerland iwaruhusu kujiua kupitia sanduku jipya maalum kwa ajili ya kujiua liitwalo ‘Sarco Euthanasia’ yamesitishwa baada ya Mwanamke mmoja wa Marekani kutumia kifaa hicho kujiua akiwa Switzerland.
Florian Willet ambaye ni Rais wa Kampuni ya The Last Resort iliyotengeneza sanduku hilo pamoja na Watu wengine kadhaa wamekamatwa na Polisi kufuatia kifo cha Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 64 ambaye jina lake halijatajwa hadharani ambaye alijiua September 23, 2024 kwa kutumia sanduku.
Tukio hilo la kutisha lilifanyika katika msitu uliopo kaskazini mwa Mkoa wa Schaffhausen, Uswizi ambapo Willett aliyeshuhudia tukio hilo aliviambia Vyombo vya Habari kuwa Mwanamke huyo alikufa kwa amani, haraka na heshima zote, kitendo ambacho kimelaaniwa vikali na Wabunge wa Nchi hiyo.
Soma Pia: Shirika la Exit International la Marekani limezindua mashine maalumu la kujiua iitwalo ‘Sarco Pod’
Waziri wa Afya wa Uswizi, Elisabeth Baume-Schneider ameliambia Bunge la Uswizi kuwa matumizi ya sanduku hilo hayapaswi kuruhusiwa kuwa halali Nchini humo kutokana na wingi wa Wananchi wanaoishinikiza Serikali iwaruhusu kujiua kwa kutumia sanduku hilo ambapo tangu kifo cha Mwanamke huyo kitokee, maombi yote ya kutaka kujiua ya Watu takribani 371 yamesitishwa.
Sanduku hilo la kifo linaundwa kwa kutumia teknolojia ya 3D ambapo linamruhusu Mtu kuingia ndani yake na kubonyeza kitufe mara moja ili kuruhusu hewa ya nitrojeni kuingia na kumuondolea uhai ndani ya muda mfupi