Wakuu
MsemajiUkweli na
jingalao, kiukweli tunatofautiana sana humu jf katika uwezo wa kusoma bandiko la mtu, kila anayejua kusoma na kuandika, anaweza kusoma chochote na kuandika chochote, tatizo ni kuandika kitu cha maana na kiwango cha uwezo wa uelewa wa kuelewa kilichoandikwa kwenye bandiko fulani na kubaini lengo na maana halisi ya bandiko husika lina maana gani na lengo lake ni nini, yaani "the motive behind".
Sasa kama mmeshindwa kuelewa kitu simple na straight forward kilichoandikwa humu na
BAK, mtaweza kweli kusoma mabandiko kama yetu tunaokuja na vitu complex na vigumu kuelewa kama we were hutafikirisha ability yako?!.
Rais ndio mkuu wa nchi, with all info tips from "his" reliable "sources" ziko at his finger tips!, hivyo he is expected to be the one and only who should have known better than anybody else!, sasa inapotokea mkuu wa nchi anajitokeza kwenye public ya watu au kadamnasi ya watu na kuanza kutoa kauli za guess work, kama hizi,
hamuoni kuwa ni tatizo?!. If rais wa nchi is unsure about allegations fulani ya ufisadi kwenye taasisi nyeti kama jeshi la polisi!, then who will be sure?!, kiukweli we have a serious problem here!, ambayo saa hizi haiwezi kuonekana kwa sababu bado ni mapema mno kumfanyia assessment lakini akiendelea hivi, for sure, taifa litakuwa in deep trouble!, nyie endeleeni tuu kumuimbia nyimbo za sifa na mapambio ila mwisho wa siku wakati wa suffering utakapowadia, tuta suffer wote, nyie mnaoshangilia na sisi tunaopinga, na ndipo mtakapogundua kumbe he is not only just a real dictator, but also a comedian!, stabbing you while making look like a joje!, kama Tanzania kama nchi tunachotaka ni comedy, then, tutapata na rais tumempata!.
Tangu mwanzo kuna kina sisi ambao we don't believe in one man show za hizi shows za comedy kama ziara za kushtukiza, tunataka a real and serious changes in systems!, tukitaraji rais wetu kama mkuu wa nchi to be perfect kuongoza mabadiliko haya!, akipata tip ya ufisadi popote, kabla hajatamka chochote, kwanza ajiridhishe kwa kutumia vyombo vyake, ajue for sure what is it exactly!, watu wameiba bilioni 20, 40 au 60, ni kina nani, na ni kiasi gani?!, hii ya "eti nimesikia, kuna watu!, wamekwapua eti sijui ni bilioni 20, 40, 60, etc", atuachie sisi watu wa kawaida tukiwemo wana jf tusio na source, lakini yeye mwenye all the sources hana haja ya kuharakisha!, anaharakishia nini kama hii
Magufuli: Kuna mtu alikuwa anahamisha kati ya Tsh milioni 7-8 kila dakika...
ikaja kutokezea jumla ya fedha zote kwa miaka yote hazifiki hata bilioni 100!. Alipokwenda pale BOT aliingia kwa mkwala kumtetemesha Gavana na kuongea kwa confidence kuwa ana taarifa na anakijua anacho zungumza! , hadi leo kiko wapi? ,hizi ziara siku hizi zimeishia wapi? ,ukisikia nguvu ya soda utatofautishaje na hii. Tunataka mrejesho wa kila anachokifanya rais sio kuvamia tuu mahali au kutoa tuhuma then nothing!.
Hapa kazi tuu, tunataka kazi kweli kwenye changing the systems, mifumo, changing the mindset za watendaji, mabadiliko ya how we do things yaonekane na tuambiwe matokeo chanya ya mabadiliko hayo kwa maeneo yote na sio hizi shows za ze comedy za one man show zinazoebdelea!.
Paskali