Supu mapupu, Kichwa Mbuzi Kiria Bar na Euro Pub

babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
14,054
17,723
Enzi hizo mnatoka Jolly mnakesha Las Vegas Casino au Billz kunakucha sa kumi na mbili kijua hichoo, mko nyanganyanga mnachomoka hadi kino wale tuliokaa mitaa hiyo Mnaishia Kiria Bar.

Sufuria kuubwa lina supu mabichwa ya mbuzi, bandama, mikia, mapupu, ulimi
Linachemka Unapewa waya, unachomoa unachotaka.

Wanakukatia pale pilipili na ndimu kibao unapewa. Pembeni kuna mmaza anapika chapati moto. Ukitaka ndizi imoo kwenye msufuria unapewa
Mnatwanga supu hatari. Mpk sa mbili asubuhi huku mnazimua na biere.

Mkitoka hapo mmeshiba. Mmelewa mnaenda kulizima tu home. Unafika home Maza mwenye nyumba anapika vitumbua kibarazani. Anakuona unapiga hatua tatu mbele tano nyuma.

Anakwambia "mwanangu umependezaaaaa mwenyewe". Unamwambia nipishe hapo kabla sijabutua sufuria hilo
"Tunakula nini"?

Unampa teni amri "nikiamka ugali kabichi nyama" Sawa mume wangu. Hapo utaamshwa sa kumi msosi huu hapa😅😅😅

No stress. Yale maisha yalikua safi sana
Ulikuwepo? Toa ushuhuda hapa.
 
Beer asubuhi mkuu ndio maana tunakufa masikini sasa akili itafanya kazi saa ngapi kama mtu analalia pombe anaamkia asubuhi na mapema pombe tena
 
Back
Top Bottom