Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Wakuu, ni kitambo sasa tangu habari itoke kwamba Ziwa Nyasa (ambalo jirani zetu wanaliita Ziwa Malawi) lina dalili la kuwa na wingi wa mafuta. Tetesi za kuwapo mafuta katika ziwa hili ndilo hasa lilikuwa kiini cha Malawi kuanza kusisistiza kuwa lile ziwa lote liko upande wao na upande wetu Tanzania tukasema mpaka uko katikati ya ziwa. Mgogoro huu wa mpaka ulikuja kuwa kaa la moto lililofikishwa SADC na kina Mbeki kuambiwa watafute suluhu kati yetu na Malawi. Malawi ilipotaka kuweka kampuni ya uchimbaji ziwani, Tanzania ilitishia kuchukua hatua dhidi yao, na shughuli hizo za utafiti wa mafuta zikasimamishwa.
Sasa nauliza, hivi hili suala limeishia wapi? Hivi tunaacha huu mtifuano wa mpaka uendelee kutunyima fursa ya kuchimba haya mafuta? Mara kadhaa nilipendekeza humu JF, kwamba kwa nini Tanzania na Malawi wasikubaliane kuweka bifu ya mpaka kando na kuamua kwamba, kwa kuwa eneo la ziwa ni dogo, mafuta yoyote yatakayopatikana kwenye hili ziwa yatachimbwa kama mradi wa pamoja (joint venture) ili faida yake igawanywe kati ya Tanzania na Malawi kwa uwiano wa 50:50?
Tatizo la mgogoro kati ya Tanzania na Malawi sio mpaka, ni mafuta. Sasa tusahau mambo ya mpaka uko wapi tugawane chochote kinachopatikana ndani ya ziwa nusu kwa nusu, bila kujali kinapatikana wapi ndani ya ziwa. Sisi ni jirani.