STORY: Mfalme aliyefuga mbwa 10 ili kuua watumishi wake wakikosea

Man Middo tz

Senior Member
Sep 9, 2020
182
271
STORI FUPI: MFALME MWENYE MBWA 10 WA KUUWA WATUMISHI WAKE WAKIFANYA KOSA.

Aliishi mfalme mmoja aliyekua na mbwa 10. Mfalme muda wote alifikiri kila afanyacho yupo sahihi, Kama mtu yoyote akimpinga asemacho alimpa adhabu kali na kumtupa kwa wale mbwa aliwe hadi afe.
Wale mbwa waliwaua mamia ya watumishi wake waliofanya makosa.

Siku moja, mmoja wa watumishi wake alitoa wazo ambalo sio sahihi na mfalme hakupenda kabisa kile kitu. Hivyo mfalme akatoa amri yule mtumishi wake akatupwe kwa wale mbwa.

Yule mtumishi akamwambia mfalme

“Nimekutumikia kwa miaka 10, Na leo unanifanyia unyama huu? Tafadhali nipe siku 10 kabla hujanitupa kwa wale mbwa”
Mfalme akakubali.

Katika hizo siku 10 Yule mtumishi alizitumia kwenda kwenye banda la wale mbwa kuwangalia, akamwambia mfalme kuwa hizo siku 10 atazitumia kuwahudumia wale mbwa.

Yule mtumishi kaanza kuwapa chakula, kusafisha sehemu wanayokaa, kuwaogesha na kuwa karibu nao kuwapenda kama wa kwake.

Baada ya siku 10 kuisha, mfalme akatoa oda yule mtumishi wake akatupwe kwenye wale mbwa kwajili ya adhabu yake.

Pindi yule mtumishi alipotupwa kwa wale mbwa, watu wote walipatwa na mshangao usio wa kawaida baada ya mbwa wote 10 kumkimbilia miguuni kwake na kuaanza kuchezesha mikia yao wakifurahi.

Mfalme alikasirishwa hakuamini kile anachokiona, akasema

“Kipi kimetokea kwa mbwa wangu?” mhudumu akajibu kuwa

“Nimewahudumia kwa siku 10 pekee na hawajasahau huduma yangu, lakini wewe nimekuhudumia kwa miaka 10 yote, umesahau yote kwa kosa langu la kwanza kwako”

Hatimae mfalme katambua makosa yake, akaamuru mtumishi wake aachiwe huru, toka siku hiyo mfalme akajifunza kukosolewa ni sehemu ya kumfanya atambue michango ya watu na sio kosa kama alivyodhani hapo awali.

FUNZO: Siku zote sahau kosa kumbuka funzo, ukijikwaa inuka na uendelee na safari. Hata kwenye familia jenga mazoea ya kuwapa watoto wako watoe maoni yao na si kutoa amri kwa kila kitu, muda mwingine unakosea usemacho na watoto wako wanakucheka kwa mawazo yako ya kizamani.

Jenga demokrasia ndani ya familia yako kwanza, jenga uhuru kwa kujieleza kwa wanao usiwazibe midomo yao unawanyima haki. Wape nafasi ya kujitetea wafanyakazi wako iwe ni dada wakazi, wasaidizi wa mama ntile, hata wale wa maofisini.

Kumbuka kupewa nafasi ya kuongoza wenzako haimaanishi una uwezo mkubwa wakufikiria, au unaakili sana kuliko wale unaowaongoza. Tumia nafasi yako vizuri kwa manufaa ya wote.
****
Ni yule yule Man Middo tz
On Twitter @middotz_
 
SIMULIZI FUPI YA KUFUNDISHA NA KUELIMISHA.

VIJANA WAWILI KATIKA SAFARI JANGWANI

NA Man Middo tz

Siku moja marafiki wawili walikua wakitembea katika jangwa, Basi katika sehemu ya safari yao wakawa na mabishano kidogo na mmoja akafikia kumzabua mwenzake kibao cha usoo (Paa.)

Yule aliyepigwa kofi aliumia, Lakini bila kusema chochote akandika katika ule mchanga wa jangwani (Vumbi)

“SIKU MOJA RAFIKI YANGU MPENDWA ALINIZABA KOFI USONI”

Waliendelea na safari yao hadi walipofika sehemu yenye mto hapo waliamua kuoga kidogo, Yule aliyetandikwa kofi akanasa kwenye tope kaanza kuzama, Lakini rafiki yake akamuokoa.Baadae alivyopumzika kidogo baada ya kutaka kuzama akaenda kwenye jiwe akandika

“LEO RAFIKI YANGU MPENDWA AMEOKOA MAISHA YANGU”

Yule rafiki yake aliyempiga kibao na kumuokoa akamuliza rafiki yake

“Baada ya kukumiza ukandika kwenye mchanga na sasaivi umeandika kwenye jiwe, Kwanini?” Rafiki yake akajibu

“Pindi mtu akitumiza tunatakiwa kuandika chini kwenye vumbi, sehemu ambayo upepo wa msamaha unaweza kupita na kufuta, Lakini wakati mtu akifanya kitu kizuri kwetu lazima tuchonge kwenye jiwe sehemu ambayo upepo hauwezi kufuta”

Andika vipindi vyako vya machungu katika VUMBI.
Andika vipindi vyako vizuri katika JIWE.
Andika wasiwasi wako katika VUMBI.
Andika jinsi ulivyobarikiwa katika JIWE.

Andika HUZUNI yako katika MCHANGA na MEMA katika JIWE.

JIFUNZE KUANDIKA MAUMIVU YAKO KATIKA VUMBI NA KUANDIKA FAIDA ZAKO KATIKA JIWE.

KAMA UMEJIFUNZA KITU SHARE NA WENGINE.
On Twitter @middotz_
 
STORI FUPI: MKE WANGU HAKUPATA UJAUZITO KWA MIAKA 10 NA SIKUMONYESHA CHUKI.

Tulifunga ndoa miaka 10 iliyopita, Lakini Mungu hakutubariki mtoto. Sikuwahi kutaja au kuonyesha uhitaji wa mtoto mbele ya mke wangu, Najua ingemfanya awe na huzuni . Lakini kiukweli ndani ya moyo wangu ilikua ndoto yetu kubwa.

Siku moja mke wangu alikua hajisikii vizuri. Tukaenda kufanya check up ya mwili mzima, Na daktari akatupa habari tuliyokua tunaingojea kusikia kwa miaka kuwa mke wangu alikua mjamzito. Lakini nilichukia, pindi daktari aliposema

“Kutakua na matatizo wakati wa kujifungua”

KWANINI HAKUTOKUA NA FURAHA BILA YA HUZUNI?

Nilijiuliza lakini tulikua na furaha kupata mtoto, na kwamba mke wangu akakubaliana na kila hali. Alikua akihitaji mtoto, na hakika wote tulihitaji.

Basi nikamjali na kumlinda kama ua, Na kumpenda kusiko kuwa na kikomo. Sababu moja tu ni kuwa yeye ni maisha yangu, na alikua anaenda kutupatia mtoto wetu.

Nilikua na matumaini kuwa hakutakua na matatizo yoyote wakati wa kujifungua.

Nikaomba usiku na mchana kwajili ya familia yangu. Baada ya kujifungua mtoto wetu wa kiume, yani kamalaika ketu, mke wangu akanza kupoteza uwezo wake wa kuona.

Mke wangu hakuweza hata kufanya kazi za kawaida za kila siku, lakini alikua na furaha sana kwasababu alikua na kamalaika kake mikononi mwake.

Kwa kweli nisingeweza kusimama kumuona akiteseka nikaanza kufanya kazi usiku kucha, kazi za vibarua na kazi za mtandaoni nikafanya.

Kiukweli ni kama sikulala kwa mwaka mzima. Mwishowe nikaweza kuweka akiba kwajili ya upasuaji wa jicho. Akafanikiwa kufanya upasuaji, ninafuraha kumuona akifurahi kuhusu namna anavyoweza kuona vitu vizuri sasa.

Ilinichukua mwaka kufanya kazi kwa bidii, kupoteza usingizi na nguvu. Sijisikii vibaya kwajili ya hayo hata kidogo kwasababu anastahili kufanyiwa vyote hivyo.

Anastahili kila furaha ya hii dunia, Mimi ni mwanaume mwenye bahati kupata mke mzuri, mtoto na kupata familia pia. Maisha yangu yamekamilika sasa.

FUNZO: Pindi unapompenda mtu, unaweza kufanya chochote kwajili yake hata kama ni ngumu kwako. Hata kama mwenza wako yupo katika hali ngumu, msapoti yeye kuliko kumuacha akiteseka .

“UPENDO WA KWELI NI HALI AMBAYO FURAHA YA MTU MWINGINE NI NGUZO KWAKO”

JIFUNZE KUMPAMBANIA YULE UMPENDAE HAIJALISHI UPO NA HALI DUNI KIASI GANI, KAMWE USIKATE TAMAA JIFUNZE KUPAMBANA.

TUENDELEE KUSOMA SIMULIZI YETU PENDWA YENYE MAFUNZO MENGI INAYOKWENDA KWA JINA LA

“SABABU NI KIFO CHAKO BABA”

NDANI KUNA BURUDANI NYINGI SANA, HAYO YALIYOMO NDANI HUENDA YALISHAKUTOKEA USIACHE KUSOMA NDIO KWANZA TUPO MWANZO. USIKOSE EPISODE YA 6 NICHEKI KATIKA PAGE ZANGU

man Middo
Man Middo tz
Twitter ni @middotz_
 
SIMULIZI FUPI YA KUSISIMUA NA MAFUNZO MENGI.

Mwanamke mmoja alitoka nje ya nyumba yake, na akawaona wanaume watatu, wazee tena wenye ndevu zao ndefu nyeupe. Wale wanaume walikua wamekaa katika eneo lake kwenye benchi. Yule mwanamke akasema

“…sidhani kama nawajua, tafadhali ingieni ndani kuna chochote nitawapa mle”

“Mumeo yupo nyumbani?” waliuliza wale wazee

“Hapana, Ametoka” alijibu Yule mwanamke,

“Hivyo hatuwezi kuingia ndani kama hayupo” walijibu wale wazee.

Baadae mumewe alivyorudi nyumbani, akamuelezea kilichotokea

“Nenda kawambie nipo nyumbani, na uwakaribishe tena ndani” mumewe alisema.

Mwanamke alitoka nje na akawakaribisha wale wazee ndani

“Hatuendi ndani wote kwa pamoja” walijibu wale wazee,

“Kwanini?” aliuliza Yule mwanamke.Mmoja wa wale wazee akanza kutoa maelezo:

“Jina lake ni UTAJIRI”

Alisema huku akimnyoshea kidole rafiki yake, akamuelekezea mwingine kidole akisema

“Huyu ni MAFANIKIO, na Mimi ni UPENDO”

Akaongezea kusema

“Sasa rudi ndani na ukajadili na mumeo ni yupi miongoni mwetu mnamtaka nyumbani kwenu”

Mwanamke akarudi ndani na kumwambia mumewe alichoambiwa na wale wazee. Mumewe alijawa na furaha iliyopitiliza

“Ni uzuri ulioje” alisema Yule mwanaume “Ngoja tumkaribishe UTAJIRI, ngoja aingie ndani mwetu aijaze nyumba yetu utajiri”

Mke wake akakataa

“My dear, kwanini tusimkaribishe MAFANIKIO?”

Bint yao mpendwa akaingilia ule mjadala, nae akaja na mapendekze yake

“Je si ingekuwa bora tukamkaribisha upendo? Nyumba yetu sasa itakua imejawa na upendo”

“Hebu ngoja tuchukue ushauri wa bint yetu” alisema mwanaume kwa mkewe.

“Toka na umkaribishe Upendo awe mgeni wetu”

mwanamke akatoka nje na na akawauliza

“Ni yupi kati yenu ni Upendo, Tafadhali ingia ndani na uwe mgeni wetu”

Mzee upendo akaamka na kutembea kuelekea katika ile nyumba, wale wenzake nao waliamka pia na kuanza kumfuata mwenzao.

Kwa kushtukiza Yule binti yao akawauliza Utajiri na Mafanikio

“Nimemkaribisha Upendo pekee, kwanini mnaingia ndani?"

Wazee wakajibu kwa pamoja

“Kama ungemkaribisha UTAJIRI au MAFANIKIO sisi wengine tungebaki nje,
Lakini kwa kuwa umemkaribisha UPENDO, Popote aendapo tunaenda nae. Popote kwenye UPENDO, Pia kuna UTAJIRI na MAFANIKIO”

Like na shusha comment kama umenifunza kitu...
Twitter @middotz_
 
STORI FUPI: MTOTO ANAETAKA KULIPWA KILA ANACHOMSAIDIA MAMA YAKE.

Mama mmoja na mtoto wake wakiume wa miaka 8 walikua na mabishano kuhusu kufanya kazi za nyumbani.

Mtoto alikua akifoka kwa sauti kubwa pindi alipokua akiongea na mama yake.

Baadae jioni, yule mtoto alimfuata mama yake jikoni wakati akiwa anapika.
Alionekana kuwa mwenye chuki na hasira huku ameshikilia karatasi mkononi aliyokua ameandika.

Baada ya mama yake kuosha mikono yake, akakaa chini kuisoma ile karatasi ambayo iliandikwa hivi

“Kwa kufyeka majani kwenye bustani gharama yake sh 10,000. Kwa kufanya usafi wiki hii yote sh 5,000.

Kukufuatia vitu store sh 8,000. Kukaa na mtoto wakati umeenda sokoni sh 30,000.

Kutoa uchafu kwenye dustbin kupeleka kwenye gari la taka sh 5000.

Kwa kukuletea ripoti nzuri shuleni sh 25,000. Jumla sh 83000/=”

Mama yake alimuangalia sana, yule mtoto hakujua kipi kinaendelea katika ubongo wa mama yake.

Mama akakaa na lazima angemwambia jinsi alivyochukia, mama akachukua pen akageuza lile karatasi aliloandikia kijana wake, na hiki ndio alichokiandika yule mama

“Kwa miezi 9 niliyokubeba wakati unakua ndani ya tumbo langu: HAKUNA MALIPO.

Kwa machozi yote uliyonisababishia katika miaka yote: HAKUNA MALIPO.

Kwa kila usiku niliosimama hospitalini na nyumbani kuhofia kifo chako: HAKUNA MALIPO.

Kwa midoli, chakula, nguo na baiskeli nilivyonunua: HAKUNA MALIPO.

Kwa kila kiatu nisichokua nauwezo nacho wa kukinunua lakini bado nikanunua: HAKUNA MALIPO.

Pia kwasababu sikutaka uonekane mdhaifu mbele ya watoto wengine: HAKUNA MALIPO.

Kwa kila safari ya kwenda kutalii na wenzako ambayo hata sikua na uwezo nayo lakini bado ukaenda: HAKUNA MALIPO.

Kwa kila safari niliyoahirisha kwenda kuonana na rafiki zangu ili tu wewe na kaka yako mle kwa wakati: HAKUNA MALIPO.

Kwa kila maumivu katika viungo vyangu baada ya kuunganisha shift ili tu upate maisha mazuri ya baadae: HAKUNA MALIPO.

Kwa kila muda niliojificha bafuni na kulia kuhofia kama nitokuwa na pesa ya kutosha kulipia bili: HAKUNA MALIPO.

Kwa kila usingizi nilioupoteza kuhofia kama nakufanyia mazuri: HAKUNA MALIPO.

Kwa kila muda niliokuepo kwajili ya matatizo yako na mahitaji yako: HAKUNA MALIPO.

Kwa msaada wangu wote na ushauri wangu: HAKUNA MALIPO”

Mama akanyanyua kichwa chake nakumuangalia mwanae akasema

“Mwanangu, utakapo jumlisha vyote hivyo, gharama yake iyakua 0.00”

Pindi yule kijana alipomaliza kusoma ujumbe ulioandikwa na mama yake alikua akitokwa na machozi mengi sana machoni mwake, alisimama na kumtazama mama yake sawa sawa akasema

“MAMA, NINA UHAKIKA NAKUPENDA”

Akamkumbatia mama yake kwa upendo na nguvu.

FUNZO: Kamwe hautajua wazazi wako wanathamani kiasi gani mpaka uje kuwa mzazi wewe mwenyewe. Hebu kuwa MTOAJI, sio ANAEULIZA NIKUPE haswa ukiwa na wazazi wako.

Kumbuka, kuna vingi vya kutoa tofauti na pesa. Sasa kama mama yako yupo karibu yako, nenda ukamkiss na umuombe msamaha.

Kama yuko mbali mpigie simu na hakikisha anajua kuwa unajivunia kwa kila kitu alichokufanyia.

TUWAHESHIMU WAZAZI WETU, MSAIDIE KILA WAKATI.

HUNA HAJA YA KUMULIZA KAMA ANAHITAJI MSAADA AU KITU FULANI WEWE MPE KILA WAKATI.

On Twitter and Instagram @middotz_
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom