Stori ya kweli iliyonitokea nikiwa mwanafunzi wa udaktari mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Muhimbili

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
821
2,078
Na Dr.Bernad

Hii ni stori ya kweli iliyonitokea mwaka 2016 nikiwa mwanafunzi wa udaktari mwaka wa tatu.

Mwaka 2016,nilikua mwanafunzi wa Udaktari mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Sitakaa nisaisahau siku ambayo ilikua mara yangu ya kwanza kuingia wodini kama daktari mwanafunzi kama ilivyo taratibu za vyuo vya Afya na Tiba vyote Duniani.

Ilikua majira ya saa 1 jioni, Siku hiyo nilivaa suruali nyeusi, sharti jeupe lenye madoa ya bluu (blue) na tai nyekundu yenye madoa meupe. Nilivaa koti langu jeupe jipya, nikaweka na stethoscope shingoni mwangu, HAKIKA nilipendeza sana kama Daktari na aliyeniona bila shaka alihisi mimi ni daktari bingwa, kumbe ilikua mara yangu ya kwanza kwenda kuwaona wagonjwa, nikabeba Faili langu kuelekea wodini nikiwa mwenye furaha sana, maana kwa mara ya kwanza nilijihisi Daktari Baada ya masomo magumu sana ya mwaka wa pili kuyavuka.

Hua ni Ada kwa wanafunzi wa udaktari kwenda kupata taarfa juu ya maendeleo ya wagonjwa ili kesho asubuhi waweze kuwaeleza wakuu wa vitengo(Madaktari),kama njia ya kujifunza na kukuweka karibu na kile unachokisomea,ndio maana nilielekea Wodini majira hayo,Moja kati ya Wodi za hospital ya taifa ya Muhimbili.

Kwa mbwembwe nyingi ikiwa mara yangu ya kwanza,niliingia wodini na nilimuona mama mmoja aliyekua ni mgonjwa, niliongea naye juu ya shida yake na nikamfanyia vipimo nilivyostahili kufanya kwa wakati huo. Niliagana naye nikawa naondoka wakati huo ilikua imefika majira ya saa tatu usiku.

Nilivyokua nataka kutoka, kuna mgonjwa aliita.
Doktaa, Doktaa, kwa kuwa nilikua bado sijawa Daktari niligeuka huku na huku kuona kama kuna mwingine anaitwa, sikumuona yeyote zaidi yangu, ndipo nilipoitika "NAAM",Nakuomba usogee hapa, alisema kwa sauti ya chini.

Nilijongea Kitandani kwake alipokua amelala,
Maongezi yetu yalikua hivi,

Mimi:Habari yako dada
mgonjwa:Nzuri.

Mimi pole
Mgonjwa :Asante.

alikohoa kidogo akaniomba nimpatie maji yaliyokua kwenye meza ndogo pembeni ya kitanda chake.nilimpa akanywa tukaendelea na mzungumzo.

Mgonjwa Daktari unaitwa nani?,
Mimi:Nilimtajia jina

Mimi: Kwani wewe unaitwa nani?
Mgonjwa: Mimi ninaitwa Faraja.

Mimi:Una umri gani na unatoke wapi?
Mgonjwa(faraja): nina miaka 22 natokea Magomeni (sehemu katika jiji la dar es salaam)

Nina mtoto wa miezi miwili ambaye hajawahi kunyonya maziwa yangu maana yamevimba mwezi wa pili sasa.,

Madaktari wamenifanyia vipimo ila bado wanasema hawajagundua tatizo ni nini.,

Nilimtazama kwa uwoga Maana Maziwa yake yalikua yamekua makubwa mithili ya kichwa cha mtoto wa miezi mitatu na kulingana na ugeni wangu wodini uoga ulizidi.

kwa kuwa nilikua naondoka kuwahi nyumbani nilimuuliza umeniitia nini?

Faraja alijibu,'MIMI NAONA LEO NITAKUFA, NAOMBA UNIOMBEE"

Alivoniambia maneno haya nilitabasamu kidogo kuonesha kutokukubaliana na mawazo yake, Halafu nikamuuliza,UMEJUAJE?

Yeye alijibu, nimeona hivyo. Aliendelea kusema, "namwone huruma mwanangu ambaye hata hajawahi kunyonya"

Nilingiwa na huzuni moyoni. Nikanyamaza kwa muda, huku faraja machozi yakimtiririka

Nilimfariji kua HATAKUFA kwa kuwa yupo Mikono salama maana madaktari wa Hospitali ya Taifa ni wenye Weledi mkubwa na Wamebobea kwenye Fani zao.

Faraja alisisitiza nimuombe.

Tatizo kubwa hata kuomba kwa wakati huo nilikua siwezi Maana nilikua nimeacha kusali yapata miaka miwili, sio kwenda kanisani tu,hata kusali wakati wa kula au kulala nilikua sifanyi hivyo.

Suala la kumuombea faraja likawa mtihani mkubwa sana kwangu.

Niliishia kumshauri asikate tamaa na kumchekesha maana Mungu amenijalia kipaji cha kuchekesha, Faraja alitabasamu lakini hakuridhika.

Nilimuaga kuwa naondoka na nikamwabia kesho mapema asubuhi nitakuja kumuangalia kabla ya Kwenda darasani KUMBE NISIJUE USIKU NI MREFU SANA. Alinipungia mkono akiongea kwa sauti ya chini "Usiku mwema" nikaitikia asantee,ugua polee.

Niliiondoka wodini,nikarudi nyumbani.
Nilivyofika nyumbani Nilianza kuumia moyoni.
Nikaanza kujiuliza maswali

"Hivi nilishindwa hata kumwamba MUNGU AKUPONYE?",
"Hivi nimekua mdhambi kiasi hiki kiasi kwamba hata kutamka sala moja tu kwa mtu nimeshindwa"?

Nikipata kigugumizi moyoni, Nikataka nirudi kumuombea, lakini tayari ilikua ni usiku saa nne kuelekea saa tano.

Nilijifariji nikasema kesho nitaamka asubuhi mapema" nikamuombee hata maneno mawili" ili afarijike.

Sikupata Ujasiri wa kumuombea maana nilijiona nina dhambi nyingi na Mungu hawezi kunisikiliza na nilikua naona hata Aibu kuomba.

Asubuhi niliamka nikajiandaa mapema kama kawaida kuwahi Wodini.

Nilivyoingia wodini moja kwa moja nilienda kwenye kitanda cha Faraja,

Wakati huo Faraja hakuwepo kitandani.

Mara Nesi alitoka chumba cha Manesi kilichopo Wodini, huku akiwa ameinama chini.

Mimi nilifikiri labda faraja ameenda Uwani mara moja, Au yupo chumba cha Manesi Anahudumiwa.

Nesi alisogea mpaka kitandani kwa Faraja akaanza kuondoa mashuka aliyokua akitumia faraja.
Nikishtuka maana hata hakunipa salamu.

Nikamuuliza vipi sister Pashenti (Patient), Kwa maana ya mgonjwa, aliyekuwepo hapa ameenda wapi?

Nesi alijibu kwa sauti ya chini, amefariki.
Mimi nikashtuka; Eeh
Nesi akurudia tena, nasema amefariki.

Miguu yangu ilikosa nguvu, Nikakaa kitandani kwa kujiangusha, Moyoni nikapata maumivu makali, Machozi yakanitoka.

Nesi akaniambia pole, vipi alikua ndugu yako?
Sikumbuki kama nilimjibu chochote, nilinyenyuka taratibu kushuka ghorofani.
Siku hiyo ilikua siku mbaya sana kwagu, niliondoka kuelekea darasani, nilikaa darasani huku vikifundishwa vipindi mbalimbali ambavyo sikuambulia kitu.

Kila mara sauti ya Faraja ilikua ikinijia kichwani kwangu"MIMI NAONA LEO NITAKUFA, NAOMBA UNIOMBEE"

Nimehangaika sana kujaribu kusahau tukio hili,
Miaka ikawa inaenda,Kila nikipoingia wodini nikipita pale alipokua analala Faraja lazima nikumbuke na siku hiyo napoteza furaha.

Nimekua nikijiuliza Kwa nini FARAJA alinisisitiza nimuombee nikapiga chenga?

Kuna muda nikawa nahisi aidha nilichangia katika kifo chake, Maana kama ningemuombea labda asingefariki

Lakini pia nikawa nahisi labda ningemuombea safari yake ingekua njema zaidi.

Ni maswali mengi nilijiuliza kwa kipindi cha zaidi ya Mwaka ambayo sikupata Majibu yake,

Lakini Mbele nimekuja kugundua kua huenda alitaka kuniachia somo kubwa maishani mwangu kua unapohitajika msaada utoe haraka bila kuchelewa.

Ni mengi natamani kuelezea,naona hapa hapatatosha.
Natamani kuandika kitabu.

KATIKA HILI NIMEJIFUNZA HAYA

1.Muombee ndugu yako wakati wowote maana wewe sio mwamuzi juu ya uhai wake.

2.Mtu akikuomba msaada msaidie kwa wakati hali bado ana uhitaji msaada huo.Maana hata mwenye shida kuna wakati shida huzidi kiasi asitake msaada tena.

3.Tuishi kwa Kumtegemea mungu maana siku zetu zinahesabika.

4.Kuwa mtakatifu wakati wote ili tuwe na nguvu ya kusaidia wengine pale inapohitajika.

Nimeshare na wewe stori hii ya maumivu,Ili ujifunze mambo hayo makuu Manne.

Sambaza ujumbee huu kwa wengine wajifunze kupitia mimi.

R.I.P FARAJA.(NITAKUKUMBUKA DAIMA)
 
So sad tunaishi mara moja tu wape faraja wanaohitaji faraja sote dunian tunapita
 
Tumaini The Genius,
Ni kweli inabidi tuwe tayari kila wakati kwani hatujui siku wala saa,maana kifo hutujia kama mwizi,hili tukio litakuchukuwa muda kusahau lakini kaa ukijua kuwa Mungu katika kila jambo ana mipango yake, kwahiyo ina wezekana hilo lilitokea ili wengine waweze kumjua na kumrudia Mungu kupitia wewe,ubarikiwe sana...
 
Habari imenigusa!
 
1577296765199.png
Dr Tumaini The Genius sikubaliani na wewe kabisa ingawa chozi limenitoka kwa huyu Faraja na kachanga kake kwa kushindwa kumpatia ushauri wa kitabibu labda useme ni Hadithi
  1. km Dr ulitakiwa umpe tiba hata km ni Dawa ya maumivu! na sio kumuombea
  2. mpaka leo ulichojifunza ni dawa gani inasaidia kupunguza maziwa kujaa kwanini usiruhusu Manesi au ndugu wamkamue, na ulichoandika kwenye kadi ni kipi ili madaktari waje wa Diagnosis
  3. Du katika yote umetoa utaalam wa kuombea tu mna wala sio Tiba
  4. usikute una element za kichungaji na sio kiDr
 
Soma msaidie mtu wakati anshitaji msaada wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom