Songwe: Watu 5 wapoteza maisha katika ajali ya Lori na Bajaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,713
13,464
Kuna ajali mbaya imetokea Tunduma mkoani Songwe, ambapo watu watano hadi sasa wamepoteza Maisha.

Ajali imetokea maeneo ya Sogea kwenye mteremko wa Mlima Chengura.

Taarifa za awali zinadai Kati ya Watu waliopoteza maisha, Watatu ni Familia moja ambao ni Mama na watoto wake wawili mapacha waliokuwa kwenye Bajaji, Mwingine Wawili waliopoteza maisha bado hawajatambulika.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Theopista Mallya amethibisha kutokea kwa ajali hiyo.

"Gari namba T 468BUM yenye Teller namba T 262 CBR Scania, iligonga Toyota Vanguard yenye namba T500 DWN Mali ya Elika Kayungilo, pia ikagonga Bajaj yenye namba MC 574 DLW na kusababisha vifo vya watu 5 ambapo wawili hawajatambulika.

Waliotambulika ni Faustina Hala Mwanamke mwenye Umri wa Miaka 50, Venance Faustne Mwanaume mwenye umri wa miaka 25 na Vincent Faustne Mwanaume mwenye Umri wa miaka 25". Amesema ACP Theopista Mallya.

Jitihada za kiitambua miili mingine zinaendelea.

Miili imehifadhiwa Kituo cha Afya Tunduma
-723902831.jpg
-957361576.jpg
65215666.jpg
-1738313507.jpg
 
Back
Top Bottom