Mr mutuu
JF-Expert Member
- Jan 27, 2023
- 2,848
- 14,295
Aisee Kuna kisa kimoja Cha utapeli nikikumbuka huwa nacheka sana, japo sio changu kilimtokea mshkaji wangu mmoja.
Jamaa anadai walikuwa na kijiwe Chao wanakutana washkaji wengi tu, kulikuwa na pool table na vile vimashine vya kubet, anadai kijiwe kilikuwa na vijana wengi matozi tu na smart phone zilizoshiba.
Kuna siku walikuja wazee wawili wamevaa mashati ya tigo... Wakamvuta jamaa mmoja pembeni wakamuambia kuna mchongo wa pesa wanahitaji kama vijana 14 wanatakiwa kuchimba mashimo kwa ajili ya minara mipya. Jamaa kusikia vile akachomoa akamwambia kwa kijiwe hiki sidhani kama Kuna mtu atakubali kazi za kuchimba mashimo
Wale wazee wakamwambia kijana tunakupa fursa ujue, hizi ni kazi za kampuni... Wanalipa 100,000 per day ila tunatafuta watu tuwalipe 60 per day sisi Tule 40 Cha juu, baada ya kusikia vile jamaa kama kashawishika akaenda kwa wenzake akawapa mchongo. Wakashauriana weee baadae wakawarudia wale wazee kwa sharti la kulipwa 80k kwa siku na chakula mchana wapewe.
Jamaa akawa ananiambia kijiweni kwao sio kwamba watu Wana njaa sana ila waliona ni uzembe kukataa kazi jioni unarudi na 80k yako safi kabisa... Basi wale wazee wakawakubalia ila kwa sharti kuwa vifaa vya kufanyia kazi watatafuta vijana wenyewe.
Watu wakatafuta vifaa wakakutana meeting point asubuhi, wazee wakaja wakawa wanalalamika kuwa gari ya ofisi imepata shida kidogo ila mpaka jioni Itakua sawa, hivyo wakakodi virikuu viwili vijana wakapanda wakawapeleka maporini huko
Sasa sijui wale wazee walifanya scout ya eneo maana anakuambia hakuna watu Kule yaani ni pori kweli... Basi Kila mtu akapewa eneo lake la kuchimba shimo, halafu wakatenganishwa yaani huwezi kumuona mwenzako... Kazi ikaanza bana, jamaa anakuambia wamekomaa kuchimba mashimo kuanzia saa 4 mpaka saa 8 yaani ni kazi kazi, saa 8 Kuna Mzee mmoja akapita kuanzia kwa mtu wa kwanza anachukua order ya chakula kuulizia wanakula nini. Sasa Mzee ukishampa order yako anakuomba umuazime simu apige yake imeisha chaji.. sasa kumbe huu mtindo alikuwa anafanya kuanzia kijana wa kwanza mpaka wa mwisho..na kumbuka hapo mpo mbalimbali hamuonani
Jamaa wamepiga kazi mpaka kufika saa 10 Wanaona mbona msosi haufiki, ikabidi mmoja atoke kumuuliza mwenzake, sasa katika kuambiana wakaja kugundua kuwa wote simu zao wamempa Mzee, ndo kuanza kuwazungukia wenzao kuwauliza... Aisee Mzee alipita na simu zote 14...
Ndiyo kugundua kuwa washapigwa, angalia huku na Kule wazee hawapo...jamaa ikabidi wachukue vifaa vya watu waanze kurudi kwa mguu, yaani jamaa anasema hapo wamechafuka vibaya sana na bado umebeba vifaa vyako barabarani mpaka kuja kupata usafiri ni kama kilomita 7....
Jamaa njiani wakawa wanatukana ila anasema inafika mahali wanakaa chini wanaanza kuchekana.... Jamaa alinihakikishia waliapa wakikutana na wale wazee watawaua, sio kwa kuwaibia simu.... Bali kwa mashimo Yale waliowachimbisha